Kesi ya Ditopile, Mramba, Yona na Babu Seya, nani alaumiwe hakimu au mpelelezi?

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,647
12,215
leo nimekaa nyumbani nikakumbuka mbali sana enzi za nyuma novemba 4 mwaka 2006 aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora ndugu DITOPILE MZUZURI alimuua kwa kumpiga risasi dereva wa daladala huku chanzo kikiwa ni kuonyeshwa dole la kati lakini DITOPILE aliachiwa baada ya kuonekana aliua bila kukusudia,

Niliendelea kuwaza mengi sana ikiwemo kesi ya MRAMBA na YONA ambao walishitakiwa kwa zaidi ya makosa 11 ya kutumia vibaya madaraka na ikiwemo kuitia serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 11.7 lakini hukumu yao ilikuwa kifungo cha miaka 3 na faini ya milioni 5 baadae wakapewa kifungo cha nje kumalizia hukumu yao ambayo ilibakia miaka miwili hivyo walitakiwa kufanya kazi ya kufagia hospitali pale sinza palestina. hasara bilioni 11.7 kifungo cha miaka 3 na faini ya milioni 5 kweli zinaendana?
yona-na-mramba.jpg

machozi yalinitiririka sana nilipoikumbuka kesi ya BABU SEYA na wanae ambao walihukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya kunajisi watoto wadogo, tofauti kubwa sana niliiona kipindi naendelea kuwaza nilichogundua DITOPILE MZUZURI alikuwa karibu sana na familia ya mkuu wa kaya kipindi kile nadhani ndio maana hakukaa sana gerezani akaachiwa, MRAMBA na YONA walikuwa na heshima kubwa kwa taifa na pengine nao walikuwa na urafiki na viongozi wenzao nao pia wakaachiwa imekuaje kwa BABU seya kesi yake kuyumba muda wote au kwakuwa yeye hakuwa na urafiki na yeyeyote?
babu+seya+px.jpg

nakumbuka kipindi nipo darasa la nne kuna bwana mmoja kutokana na wivu wa mapenzi alimuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali, kesi ya huyu bwana ilidumu kwa takribani miaka 8 alihukumiwa kunyongwa akakata rufaa akashinda lakini vigezo vilivyo sababisha ashinde ilikuwa ni kukosekana kwa ushahidi wa kitu kilichotumika kufanyia mauaji, hapakuwepo karatasi ya dokta kuonyesha kuwa mtuhumiwa alifanya kitendo akiwa na akiri timamu ama lah. rufaa ikamuachia huyo mtu lakini DITOPILE ambaye aliua kwa silaha kesi yake mpaka kuachiwa haikudumu ata mwaka mmoja, tatizo nini? watu wanaitia hasara serikali zaidi ya bilioni 11.7 wanaachiwa tumlaumu nani hapo HAKIMU au WAPELELEZI?
3.jpg

KUMBE MUDA MWINGINE UMAARUFU NA PESA HUVUNJA SHERIA
niliingia ndani sana nikatafakari ivi itakuwaje leo mimi nikiingizwa gerezani si ndo nitaozea uko uko maana sina anae nijua na ali jinsi ilivyo pasipokuwepo na mtu wa kukushika mkono ndo basi tuna kupoteza, ndugu zetu wengi sana masikini wasiojiweza leo hii wapo wengi magerezani pengine kesi zao zimefutiwa dhamana kabisa,

Nimejiuliza mengi nikagundua kuwa kuna haja kubwa sana ya kuwa maharufu lakini wazo hilo lilifutika ghafra baada ya kukumbuka kuwa hata BABU SEYA nae alikuwa maarufu lakini umaarufu wake haujamsaidia kitu. nikaiambia nafsi yangu kuwa umaarufu, pesa na kuwa karibu na viongozi wakubwa kunaweza kukasababisha sheria ivunjwe ili uonekane huna hatia.

Askari anapokea kesi ya yule muuaji, muuaji anakamatwa akiwa na kisu kikubwa yeye na maiti yake wakiwa wameloa damu mwisho wa kesi mahakamani ushahidi unakosekana hakimu anaamua kumuachia muuaji, askari anajisifu kwa kazi aliyoifanya lakini muuaji huyo huyo anaenda tena kuua ushahidi unavurugwa. HAKIMU ajiulizi kwanini ni mtuhumiwa yule yule kwa kosa lile lile tena anaamua kumuachia huru kabisa nani tumlaumu hapo askari au hakimu?
 
Mh.. Mpwa usiumize kichwa kwa mambo ambayo unajua mtiririko wake....

Ww amka asubuhi mshkuru muumba kwa kuamka salama kapange mitumba yako mjini uuze utafute mkate wa kila siku hayo mengine waachie wenyewe.

Utaumiza kichwa buree kwa mambo ambayo yak I wazi kabisa
ASANTE KWA USHAURI...JE TUNAWAJENGEA TASWIRA GANI WATOTO WETU KAMA WAZAZI WAO TUTAKUWA TUNAONEWA HARAFU TUNANYAMAZA.
 
Ushauri mzuri sana kwa mpwa wako, kwa hoja yake hio pia imenipa tafakuri ya kufikiria kuhusu kesi maarufu ya "samaki wa Magufuli", samaki na meli vilikamatwa, tena ndani ya eneo la nchi, sasa imekuwaje serikali ishindwe ile kesi? And nasikia sasa tunatakiwa kuvilipa vyote.

HALI INASIKITISHA SANA AISEE SIJUI WATOTO WETU WATAISHIJE HAPO BAADAE.
 
Dunia ni mapito tu,kuna watu wengi wamepita dunia hii na wengine tunatamani hata kuwaabudu kwa kuwaona ni watukufu sana lakini leo mbele ya muumba wao na wanachokipata huko ni siri yao na muumba wao
TUTAPITA NASIKITIKA SANA SIJUI WAJUKUU ZETU WATAISHIJE HAPO BAADAE
 
ASANTE KWA USHAURI...JE TUNAWAJENGEA TASWIRA GANI WATOTO WETU KAMA WAZAZI WAO TUTAKUWA TUNAONEWA HARAFU TUNANYAMAZA.
UTAKAPOPAZA SAUTI KWA NGUVU ILI NAO WAKUSIKIE KWAMBA HUPENDI UONEVU,

WATAKOSA NAFASI YA KUKUSHAURI, KWAMBA.BABA UNGEACHA TU,MAANA KUNA HATARI KUBWA HUTAKUWA NAO KWA NAMNA MBALIMBALI.
 
ASANTE KWA USHAURI...JE TUNAWAJENGEA TASWIRA GANI WATOTO WETU KAMA WAZAZI WAO TUTAKUWA TUNAONEWA HARAFU TUNANYAMAZA.
Watatuelewa baadaye, mbona mimi nimemuelewa vizuri baba yangu mzazi alikua fundi selemara nikiwa mdogo niliona mtu kamkunja shati na kumfokea kwa kumcheleweshea kazi yake lakini mzee hakutaka kufurukuta aliomba msamaha akaachwa maana angepambana lolote lingeweza kutokea angetuacha hatuna msaada wowote, hii ilitokana na kwamba alipata kazi nyingine ya haraka alishindwa kuikataa kazi mpya kwasababu kazi zilikua ni za shiida. Sijawahi kumkumbusha hili ila namheshimu sana kwa busara zile.
 
asante mkuu kumbe busara inahitajika sana
 
Back
Top Bottom