Mramba na Yona kutumikia kifungo cha nje. Kufanya usafi hospitali ya Palestina, Sinza

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Mawaziri wa zamani wakati wa awamu ya Tatu, Basil Mramba (Waziri wa Fedha) na Daniel Yona (Nishati na Madini) sasa kutumikia kifungo cha nje hadi Nov. 5 kwa kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Palestina Iliyopo Sinza.

Ikumbukwe Julai 6, 2015 mawaziri hao walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya milioni tano kila mmoja kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara.

===========
Habari kamili:

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia waliokuwa Mawaziri wastaafu Basil Mramba na Daniel Yona kutumikia adhabu ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza Palestina.

Hatua hiyo inatokana na Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, kupitia Mawakili wao kuwasilisha barua mahakamani hapo kutoka Magereza kuhusu kutumikia kifungo cha nje.

Mawaziri hao wa zamani waliwasilisha barua hiyo ya kuitaarifu mahakama yenye kumbukumbu namba 151/DA/3/11/223 ya Desemba 5, mwaka jana, wakiongozwa na jopo la mawakili wao watatu Peter Swai, Cuthbert Nyange na Elisa Msuya.

Katika barua hiyo waliyoiwasilisha kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho ‘Wafungwa wenye sifa ya kutumikia vifungo vyao chini ya Mpango wa Huduma kwa Jamii”.

Hakimu Mkeha alisema mchakato huo ulianza baada ya Magereza kuwasilisha barua hiyo mahakamani hapo kwa kupeleka majina ya watu wanaotumikia kifungo cha nje ikiwemo mawaziri hao.

Alisema mahakama haihusiani na mchakato huo, kwani ilishamaliza kazi yake ya kuhumu, hivyo jukumu la kutumikia kifungo cha nje ni kazi ya Magereza.

“Baada ya kuleta barua hiyo kisheria mahakama inaishinikiza Ustawi wa Jamii ili ifanye uchunguzi kutokana na majina yaliyowasilishwa mahakamani,”alisema.

Hakimu Mkeha alisema kupitia barua hiyo, Mawaziri hao wa zamani wamepangiwa kutumikia adhabu ya kufanya usafi kwenye Hospitali ya Sinza Palestina kwa saa nne za kila siku.

Alisema awali kabla ya mahakama kuridhia adhabu hiyo, iliwaita Mawaziri hao kwa ajili ya kuwahoji kama wameridhia na adhabu watakayopangiwa sambamba na vipengele vinavyowahusu.

“Kutokana na barua hiyo mahakama ikaona ni vyema kuwaita wahusika wenye ambapo tuliwahoji kama wanaridhia kutumikia adhabu hiyo, ambapo walikubali ndipo tukaridhia,”alisema.

Kuhusu masharti yaliyotumika kuwapatia kifungo hicho, alisema kinatokana na sheria ya Jamii namba 6 ya mwaka 2002, kifungu cha 3(1).

Alisema baadhi ya vigezo vinavyotumika kwa wafungwa kutumikia adhabu ya nje ni muangalio wa ripoti yao ilikuwa inasemaje, umri, washtakiwa kama walishawai kutiwa hatiani, makosa namna yalivyo, kama wanafamilia, pia kama wanakubali kuitumikia jamii, kama wana ajira, tabia za mshtakiwa na umbali wa eneo analokaa na anapofanyia adhabu hiyo.

Inakumbukwa kuwa Oktoba 2, 2015 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilitoa hukumu ya rufaa dhidi ya mawaziri wastaafu, Basil Mramba na Daniel Yona ambapo Jaji Projest Rugazia, alikubaliana na hoja kwamba kwa mujibu wa mashtaka yaliyowatia hatiani kwa matumizi mabaya ya Ofisi na kwa mujibu wa kifungo cha 35 cha adhabu PC ambacho Mahakama ilikitumia walipaswa kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka miwili na si miaka mitatu.

Katika rufani hizo, Mramba na Yona, waliwasilisha hoja tano kupinga hukumu iliyotolewa Julai 6, mwaka jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na jopo la Mahakimu watatu, likiongozwa na John Utamwa.

Aidha DPP alipinga adhabu waliyopewa mawaziri hao kwa madai ni ndogo, pia hakimu alikosea kumuachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja na pia iliiomba mahakama iamuru washtakiwa walipe fidia ya fedha walizosababisha hasara.

Katika uamuzi huo Jaji Rugazia alikubali hoja ya kina Mramba kuwa walipewa adhabu mbili kwa kosa moja.

“Haikuwa sahihi kuwashitaki kwa kosa la kusababisha hasara wakati kosa hilo lilishakuwa kwenye makosa mengine ambayo ni la tano hadi la 10,” alisema.

Aidha, alisema Yona aliunganishwa kimakosa katika shtaka hilo, hivyo alifuta shitaka hilo pamoja na adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milioni tano iliyotokana na kosa hilo.

“Ninaondoa shitaka la kusababisha hasara, ninafuta adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milioni tano, hivyo Yona na Mramba watatumikia kifungo cha miaka miwili kwa kila kosa,“ alisema.

Katika uamuzi huo, Jaji Rugazia alisema, “Nakubali Kifungu cha 6 cha Kanuni ya Adhabu kinachotaka mahakama itoe amri washitakiwa walipe fidia, lakini siwezi kutoa amri hiyo.”

Pia alikataa hoja za kina Mramba kuwa hati ya mashtaka ni batili, pia alisema hakukuwa na njama zozote kwa upande wa Jamhuri kutoita mashahidi waliosaini mkataba huo ili kuathiri upatikanaji wa haki, kwa kuwa utetezi walikuwa na haki ya kuomba watu hao wawe mashahidi wao.

Alisema wasitumie maelezo ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kuficha kosa kwa kuwa alitoa maelekezo kutokana na barua aliyoipata kutoka kwa Mramba na hakujua kama tayari Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ilishatoa angalizo la kutokutoa msamaha huo.

Kwa upande wa Mgonja, Jaji Rugazia alisema anahalalisha kuachiwa kwake huru baada ya kutopatikana na hatia. Alisema, “Siwezi kuilaumu mahakama kwa kumuachia huru”.

Katika hukumu hiyo, mawaziri hao walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh milioni tano, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.

Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani mwaka 2008, wakikabiliwa na mashtaka ya kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.
 
Mramba na Yona sasa kutumikia kifungo cha nje hadi Nov. 5 kwa kufanya usafi wa mazingira katika Hosp. Ya Palestina Iliyopo Sinza.
Yona kumpeleka kufanya usafi Sinza ambapo alikuwa anakwenda kuoneshea pesa yake ni adhabu kubwa kuliko kumfunga Segerea. Huyu aliyekuja na hii adhabu ana akili sana.
 
Jamani siyo lazima waende jela. Unajua kwa watu kama wale hata kupewa adhabu kama ile ni fedheha tosha kabisa mbele ya jamii! The point is they have been convicted! Inatosha.
 
Nashauri waachwe bila kufanya kazi maeneo yaliyotajwa ila wawe wanaenda kuripoti kila wiki kunakohusika .Wamepata adhabu tosha.Leo kwake kesho kwako.
 
Kama mtu unaiba billions unakaa jela miezi Sita halafu unatoka, unafanya fanya usafi Hospitali huku wanajamii wanakuonea huruma ya hali ya Juu na kukuombea wepesi kwa Allah, ni dhahiri kwamba waliopo kwenye power sasa watapata motisha KUU ya kuiba...
There is no good point kushawishi eti kifungo cha nje ni kigumu kuliko cha ndani... Craziness.
Watu wamesingiziwa kesi wanakaa jela Miaka tisa majalada Yao yamefichwa hayaonekani... Wengine wanapiga billions wanafungwa kihuni huni tu... Aseeh!! Pole sana Mama Tanzania
 
Jamani siyo lazima waende jela. Unajua kwa watu kama wale hata kupewa adhabu kama ile ni fedheha tosha kabisa mbele ya jamii! The point is they have been convicted! Inatosha.
You are right. Kwa watu waliokuwa na nyadhifa kama hizo ile hukumu tu ni adhabu tosha. Unajua kama mtu husafiri na kujaza jaza fomu za aina mbali mbali huwezi kujua adha ya adhabu kama hizi. Swali utakaloumizwa nalo kila mara ni:
Have you ever been convicted of an offence and sentenced to punishment?
If yes:
Which offence?
In what country and when?
What was the punishment?
 
Wafagie kuanzia saa moja na nusu mpaka saa nane halafu wachukuliwe na prado zao kwenda nyumbani kwao
 
Ahsante...namuomba ALLAH akusamehe makosa yako kama yapo na mimi pia..Aaamin
Watu kama hao wangekuwa china wangenyongwa. We watu walete hasara ya 3 bilioni kodi zetu jasho letu hlf unaongea ujinga funga bakuli wewe unakera
 
Mkapa alimfunga Nalaila Kiula Waziri wa Mzee Mwinyi kwa Rushwa, Jakaya kawafunga Yona na Mramba na still mahusiano kati ya Rais mtangulizi wake hayakuathirika Nasubiria kuona wakifungwa at least Mawaziri watatu ili twende na speed. Alianza mmoja then wawili sasa iwe watatu
 
Back
Top Bottom