Hivi mpunga una mashudu?

Hivi mpunga una mashudu?

WABALLA Inc

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2014
Posts
2,711
Reaction score
1,018
Huwa naona usukumani wakikoboa mpunga mabaki yale yamelundikwa bila kazi. Ila leo nimemsikia Waziri wa Kilimo akisema watu wasiuze nje ya nchi mpunga waukoboe ili wapeleke mchele na wabaki na mashudu.
 
Huwa naona usukumani wakikoboa mpunga mabaki yale yamelundikwa bila kazi. Ila leo nimemsikia waziri wa Kilimo akisema watu wasiuze nje ya nchi mpunga nje waukoboe ili wapeleke mchele na wabaki na mashudu
Mashudu yanatokana na pumba zililzopitia kwenye mchakato (processed)
 
Mpunga unamashudu na mapumba.ie.pumba laini na pumba ngumu.pumba laini hutumika kulishia mifugo,pumba ngumu hutumika kuchomea tofali,mbolea nk.
 
Mpunga unamashudu na mapumba.ie.pumba laini na pumba ngumu.pumba laini hutumika kulishia mifugo,pumba ngumu hutumika kuchomea tofali,mbolea nk.
Hivi hiyo pumba ikiwa ina libonge likuuubwaaa lile lililoshikana!!hivi wakuu nikiliita" lipumba"hivi itakuwa nimekosea kiswahili kweli!!!!
 
Mpunga unamashudu na mapumba.ie.pumba laini na pumba ngumu.pumba laini hutumika kulishia mifugo,pumba ngumu hutumika kuchomea tofali,mbolea nk.
Hivi mnaelewa mnachokiongelea nyie mbwiga? Tangu lini mpunga ukawa na mashudu? Mpunga una pumba tu hakuna kitu inaitwa mashudu hapo! Mashudu yanatokana na mbegu za mafuta, kama vile pamba, alizeti, karanga, ufuta, korosho, nazi, n.k. mara baada ya kukamuliwa mafuta. Pengine hata mahindi yanaweza kutoa mafuta maana huwa yanakamuliwa mafuta pia! Pumba laini (rice polishing) ndo hutumika kulishia mifugo na lile gamba la juu (rice husks) hutumika kuchomea matofari huku Usukumani au kuwekwa kwenye mabanda ya kuku na kuwa mbolea safi kabisa mara yanapozolewa kutoka kwenye mabanda hayo!
 
Huwa naona usukumani wakikoboa mpunga mabaki yale yamelundikwa bila kazi. Ila leo nimemsikia waziri wa Kilimo akisema watu wasiuze nje ya nchi mpunga nje waukoboe ili wapeleke mchele na wabaki na mashudu
Mkuu na mie nilimsikia alijing'ata kwanza ndo neno mashudu likamjia. Mabaki ya mpunga yanaitwa pumba ila mashudu ni ya pamba. Watanzania wapo makini sana siku hizi viongozi wajipange wanapotoa maelezo
 
Huwa naona usukumani wakikoboa mpunga mabaki yale yamelundikwa bila kazi. Ila leo nimemsikia waziri wa Kilimo akisema watu wasiuze nje ya nchi mpunga nje waukoboe ili wapeleke mchele na wabaki na mashudu
Uchochezi huu, defender iko nje hapo inakusubiri
 
Back
Top Bottom