Hivi Moto ya Jeshi letu la Polisi ni nini?

Hivi Moto ya Jeshi letu la Polisi ni nini?

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,367
Reaction score
9,119
Juzi tu hapa nilikuja na uzi wa kuhoji weledi wa Jeshi la Polisi haswa nililenga tukio la kumpiga risasi Mtu aliyenyoosha mikono juu..ingawa baadae naona Mods waliuunganisha uzi ule na uzi uliotangulia.

Nimejifunza mengi kupitia baadhi ya comments za Wachangiaji...nimejifunza ya kuwa bado tupo Wananchi wengi tunaoshindwa kutofautisha kati ya weledi na utashi binafsi.

Mtu ukishaapa kutumikia taasisi fulani unawajibika kwa miiko na miongozo ya taasisi husika hata kama una mitazamo yako binafsi...kutamani kwako tu kumuona Mtu amekufa hakufanyi kazi kama si sehemu ya mipango ya taasisi unayoitumikia hata kama wewe binafsi unatamani iwe hivyo.

Ndio maana baadhi ya Taasisi hizi hulazimika hata kuweka hadharani miongozo(moto) zinazowaongoza...tukichukulia mfano wa kule Marekani ambapo idara kama LAPD moto yao inasema TO PROTECT AND TO SERVE...yaani wao wapo kuwalinda na kuwatumikia Wananchi, na maneno hayo yapo kwenye Uniforms zao, Magari wanayoyatumia n.k...tunaweza kudhani hilo ni jambo dogo tu lakini ukitafakari kwa kina ni jambo linalobeba uzito mkubwa sana.

Kama vile haitoshi ni juzi tu Kiongozi Mkubwa wa Jeshi letu hili alitoa matamshi yaliyonifanya muda wote nisubiri kama atakuja tena kurekebisha lakini naona bado haijawa hivyo.

Ingawa sioni cha ajabu sana kwa alivyotamka ukichukulia utendaji wa 'Vijana' wake wengi huku mitaani...lakini basi walau kwa Kiongozi alipaswa kujitahidi kuonesha msimamo tofauti na utendaji wa baadhi ya Vijana wake wanaochafua taswira ya Jeshi zima.

Weledi wa Polisi hauishii tu kwenye vitendo, bali hata kauli zao zinapaswa kutolewa kwa weledi tofauti na Wavunja sheria tu wa Mtaani wanaoamua kutishana kwa maneno makali.

Wenzetu wameenda mbali zaidi na Polisi huvaa camera ndogo(kwenye badge) ili kuhakikisha wanatenda haki na wanapolazimika kutumia silaha au nguvu ya ziada basi camera hizo ndio zitatumika kuwatoa kwenye hatari ya kushtakiwa...huwa haijalishi Mtuhumiwa kafanya kosa gani au ana hatari kiasi gani..kinachoangaliwa ni Polisi anatumia busara kiasi gani kutatua tatizo.

Tujifunze na turekebishe tunapokosea.
LAPD-01.jpg
LAPD-badge.jpg


 
Back
Top Bottom