Hivi mnaonesha picha gani kwa nyaraka kama hizi. Si uchochezi huu?

Status
Not open for further replies.

KINGKOMANDO

Member
Jan 4, 2013
22
2
KANISA KUELEKEA RASIMU YA
KATIBA MPYA




2013
KANISA KUELEKEA RASIMU YA
KATIBA MPYA




2013

Imetolewa na Jopo la Biblia ni JIbu







BIBLIA NI JIBU
P.O.Box 25535
DAR ES SALAAM
TANZANIA

Email:biblianijibu@gmail.com au biblianijibu@ymail.com

WANAJOPO BIBLIA NI JIBU
Moses .D. Ndimbo - Mwenyekiti Taifa 0713 541 712
Veran Mushi 0753 212 799
Eleutery Kobero 0755 087 926
Desmond Hassan 0718 884 849
Damian Ndimbo 0755 238 159

biblia ni jibu 2013





Haki zote zimehifadhiwa




"MFANO KTK VIPENGELE HIVI"
Changamoto za mchakato wa Katiba
Wakristo wote inatupasa kujua kwamba, tangu kutangazwa na hatimaye kuanza kwa Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba, zimetokea changamoto za matakwa ya makundi mbalimbali ya kijamii, ambayo yanataka mambo yao ya itikadi za kisiasa, kijamii na kidini zizingatiwe kwa kuingizwa katika Katiba.



Katika kipindi hiki pia tumeshudia baadhi ya wanasiasa wanaopita kwenye nyumba za ibada za dini ya Kiislamu yaani misikiti, wakitaka mambo yahusuyo dini ya Kiislamu kama suala la Mahakama ya Kadhi na Tanzania Kujiunga na OIC yaingizwe kwenye Katiba.
Tumeshudia pia jamii ya Kiislamu kupitia Jukwaa la Waislamu la kuratibu Mabadiliko ya Katiba likitoa Kitabu maalumu kiitwacho Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Tanzania. Katika kitabu hicho yametolewa maelekezo mengi zaidi ya 30 yanayohusiana na dini ya Kiislamu kama vile madai ya Mahakama ya Kadhi, suala la kujiunga na OIC, Kupumzika siku ya Ijumaa, kutambuliwa Kikatiba kwa ndoa za Kiislamu, mavazi ya Kiislamu ya hijabu kwa wanawake yavaliwe kama sare za wanajeshi wa jeshi la Polisi na pia Jeshi la wananchi wa Tanzania, dai la kutaka Katiba itamke uwepo wa viti maalumu vya uwakilishi wa kidini Bungeni na Baraza la Madiwani, Urais uwe wa kupokezana kati ya waislamu na Wakristo, pia kutaka sheria ya ugaidi ifutwe nk. Si hivyo tu, Masheikh wa Kiislamu wamenukuliwa wakisema, Mabadiliko ya Katiba ni vita, wakimainisha vita ya kupigania masuala ya Kiislamu yaingizwe kwenye Katiba ya Muungano.
Kwa kuzingatia uzito wa Changamoto zote hizo, inafaa sana Wakristo kuyajua hayo mapema ili tusije tukawa na Katiba yenye mlengo wa Uchama, ukabila, urangi, ujinsia au Udini. Na tukifanya kosa hilo tukatengeneza Taifa la kitabaka na ubaguzi ambao hatimaye itasababisha vurugu na umwagaji wa damu.
SURA YA TATU
MAMBO AMBAYO TUPIGANIE YASIINGIE KABISA KATIKA KATIBA MPYA


  1. Mahakama ya Kadhi
  2. Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani O.I.C
  3. Katiba kuruhusu utoaji wa mimba
  4. Ndoa za watu wa jinsia moja
  5. Vyama vya kidini
  6. Kupokezana madaraka ya Urais kwa zamu
Mfano:
i) Rais akimaliza katoka Tanganyika anayefuata atoke Zanzibar
ii) Akimaliza Rais Muislam aje Rais Mkristo
SURA YA NNE
MAMBO AMBAYO HAYAMO KWENYE RASIMU YA KATIBA HII YA KWANZA LAKINI YANATAKIWA YAWEMO KWENYE KATIBA MPYA

  1. Ardhi iwe mali ya Mwananchi.
  2. Suala la uchinjaji wanyama na ndege kwa biashara liwe huru kwa watu wa dini zote na hata wasiokuwa na dini.
  3. Mavazi yanayowakilisha dini yasiruhusiwe katika taasisi za serikali mfano, Hijabu mashuleni.
  4. Kipindi cha muda wa Sensa ya Taifa kitajwe na Katiba.
  5. Dodoso la Sensa lisitaje Dini/Kabila.
  6. Katiba itamke wazi kuwa kuhubiri au kutangaza Dini Tanzania hakuna kuomba kibali Polisi isipokuwa ni kutoa taarifa serikali ya Mtaa/Kitongoji au Kijiji
  7. Mkaguzi na mdhibiti wa mahesabu ya serikali akishathibitisha kuwa kuna ufujaji wa fedha za umma apewe mamlaka ya kuwapeleka watuhumiwa Mahakamani
  8. Uchaguzi Mkuu wa Kitaifa upangiwe siku maalum Kikatiba lakini isiwe Ijumaa, Jumamosi wala Jumapili.
HISTORIA FUPI YA MIHADHARA YA DINI:
Mihadhara ya dini linganishi ilianza rasmi hadharani 1985 na mpaka sasa inaendelea. Wakristo tulianza kujibu hoja za Waislamu rasmi hadharani mwaka 1996 muda wote huo hakuna tukio la uvunjifu wa amani lililosababishwa na mihadhara hiyo kiasi cha kuitikisa Nchi. Ni juzi tu kwenye mkutano wa siasa limepigwa bomu na limeuwa watu watatu, Je wahusika ni wanaofanya mihadhara ya kulinganisha Biblia na Quran?





5.
WACHOCHEZI WA UVUNJIFU WA AMANI:
Waliochochea uvunjifu wa amani nchini ni baadhi ya Masheikh waliopita nchi nzima kufanya Makongamano waliyoyapachika jina la HATARI YA MFUMO KRISTO TANZANIA. Katika listi ya Masheikh hao hakuna hata mmoja anayefanya Mihadhara ya kulinganisha Biblia na Quran. Serikali hadi sasa inaogopa kuwakamata Masheikh hao wanaohatarisha amani ya nchi, wanasingizia mihadhara ya dini hali ya kuwa mihadhara hiyo haina hata chembe ya matendo ya kigaidi na uchochezi wa kuvuruga amani ya nchi. Masheikh wanaohatarisha amani kwa kufanya uchochezi kwa kuwaagiza Waislamu wawauwe Maakofu, Mapadri na waumini wa dini ya Kikristu na hata kudiriki kusema iwe kufa au kupona kanisa Katoliki mizizi yake itang’oka Tanzania maneno ambayo hapana ubishi wowote kuwa ni ya uchochezi na ndiyo yanayopekea chuki za kidini na uvunjifu wa amani Tanzania. Ushahidi wote huo upo. Masheikh hao ni hawa wafuatao:

  • Ilunga Hassan Kapungu
  • Muhamed Isa
  • Isa Ponda
  • Juma Kundecha
  • Ali Basaleh
  • Bilal Rehan Waikera
  • Isa Ramadhani Kiombwe
  • Kondo Bungo
  • Imamu Hamza
  • Azan Harith
  • Nassoro Muhamed Majid
  • Viongozi wa kundi la uamsho Zanzibar
Masheikh hao wanafanya Makongamano ya kuchambua Serikali, Ukristo, kutukana Viongozi mfano Mwl. Nyerere, Mzee Mkapa, Rais Kikwete na Maaskofu. Kupitia kitabu hiki ninawaomba Wakristo nchi nzima tuingie katika maombi ili Mungu asambaratishe hila zao.

ZAID UNAWEZA UKAJIPAKULIA RASIMU HII AMBAYO BADALA YA KUWAELEKEZA WAUMINI WAFANYE NINI INATAKA KUUNDA KATIBA YA MAPAMBANO JUU YA WENZAO WANATAKA NINI. TUACHENI UBAGUZI TUPATE KATIBA INAYOFAA.
 

Attachments

  • RASIMU KATIBA..docx
    38.5 KB · Views: 154
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom