Hivi mnakumbuka kauli mbiu ya JK "Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania"?

Mr Lyanga

JF-Expert Member
Jun 20, 2020
502
500
Waafrika bhan mimi sijui Genes zetu zilitoka kwa watu gani maana:
Bara maskini kuliko yote duniani ni Afrika.

Maendeleo ambayo yako chini (kiuchumi, kijamii, kisiasa n.k) kuliko mabara yote duniani ni Afrika.

Lakini my take ni kwamba, Hivi tunakumbuka kauli mbiu ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2005 alikuja na kauli mbiu ya kutuambia kwamba "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" vipi hii kauli mbiu ilifanikiwa au ndiyo iliishia kuwa ya propaganda ya kisiasa ?

Mimi nina imani haikufaulu na kuishia kuwa propaganda za kisiasa.

Hivyo basi kama haikufanikiwa, kuna hii ya Tundu Lissu kwamba ataleta "MAENDELEO YA WATU SIYO VITU" hii nayo itakuwa ya kisiasa tu haiwezi kufanikiwa chini ya Lissu hata iweje labda aiuze nchi 😁😁😁 kitu ambacho kitaleta majanga zaidi.

My take "Tufanyeni kazi kwa ajili ya kuboresha hali za maisha yetu na si kutarajia ahadi za wanasiasa kuwa watatuboreshea maisha yetu, that will be a mere dream"

Serikali jukumu lake siyo kukupa wewe hela mkononi.

Serikali jukumu lake siyo kukujengea wewe nyumba ya kuishi.

Serikali inatakiwa ishushe bei ya cement na mabati ili sisi tujenge.
Iboreshe miundo mbinu kama bara bara na umeme ili uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa zetu kwenda masokoni iwe rahisi.

Itafute masoko ya uhakika ya mazao yetu kama pamba,korosho na Mengineyo wanayolima wakulima ili wakulima wauze mazao yqo kwa bei za uhakika na waboreshe maisha yao.

Inabidi ijenge viwanda ili kuimarisha utengenezaji wa bidhaa za ndani sisi wenyewe na siyo kila kitu ni kuagiza china na kwingineko
Inatakiwa iboreshe sekta za afya madaktari wawepo wa kutosha, madawa yawepo ili kupunguza vifo visivyo vya lazima.

Sasa mshangilieni Lisu anae ponda maendeleo yanayofanywa na magufuli ambayo nyie mnaita ni maendeleo ya vitu,

Mpeni kura Lissu maana chini ya Lissu ni kweli haki tutaipata, uhuru tutaupata ,usawa tutaupata na katiba mpya pia tutaipata maana yeye si mwanasheria aliyebobea mnamwita hivyo.

Ila nna imani ndani ya miezi mitano tu ya mwanzo kuna watu mtarudi kulalamika hapa kuwa alituahidi maendeleo ya watu mbona mambo bado ni yale yale.

Hakuna Serikali duniani inayogawaga hela kwa watu au kuwajengea watu majumba ya kuishi bure.

Haipo hiyo Serikali kwa sasa.
 

Mr Lyanga

JF-Expert Member
Jun 20, 2020
502
500
Kwa hiyo kama hakuna serikali nzuri duniani chaguzi hizi ni kwa ajili ya nini?
Na gharama zake ni upumbavu au siyo?
Mkuu, unataka kusema nini funguka wazi usizunguke.
Maana yangu ni kwamba "Tutoe fikra kwenye vichwa vyetu kuwa tunataka maendeleo ya watu siyo vitu kwa sababu vitu ndivyo vitaleta maendeleo ya watu

Serikali haiwezi kupa wewe hela bali itakuandalia mazingira ya wewe ufanye kazi upate hela, kwa hiyo tuache na dhana potofu kuwa bara bara zitatusaidia nink, ndege zitatusaidia nini, viwanda vitatusaidia nini. It is actually very worse
 

Mr Lyanga

JF-Expert Member
Jun 20, 2020
502
500
Mtu anayejielewa hawezi kuwepo Chadema

Chama kilichoruhusu mgombea analiyetetea ushoga

Watoto wetu watakuwa salama kiasi gani?
Ana kipaji cha kuwadanganya watu tu ila hana la maana kwa maslahi ya taifa hili
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
24,657
2,000
Kwakweli kaulimbiu za Kikwete kama 'Kulimo kwanza' ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa
Ile ya 'Maisha bora' pia ilifanikiwa kwa asilimia fulani
 

Mr Lyanga

JF-Expert Member
Jun 20, 2020
502
500
Angalao kulikuwa na mzunguko wa fedha
Mzunguko wa fedha ulikuwepo lakini pia uliambatana na mfumuko wa bei vibaya mno.
Yani hakuna awamu ambayo bidhaa zilipanda bei kama awamu ya JK ingawa yeye alikuwa akiulizwa anasema mfumuko wa bei ni mfumo wa dunia nzima, so nafuu haikuwepo kwa sababu mzunguko wa pesa ulikuwepo ndiyo lakini gharama za maisha zilipanda pia na ndiyo maana maisha bora kwa kila mtanzania haikuonekana
 

Rizaq Hussein

Member
Nov 24, 2019
20
75
Wewe unaejielewa tunakuona huu ni mwaka wa 50 lakini unajengewa barabara unamsujudia kana kwamba miaka yote iliyopita haikuwa ni wajibu wake kufanya hivyo kwanzia kitambo hicho bali ni sasa anakushangaza Dah! ..... Msomeshe sana mwanao aje akuokoe asije na yeye akawa limbukeni wa Flyover baada ya miaka 50 yakuchagua watu wasiojua wajibu wao na bado ukaendelea kuwangan’gania kwaajili tu ya historia. Aliokupigia babu yako
 

Mr Lyanga

JF-Expert Member
Jun 20, 2020
502
500
Hivi kwa akili yako unadhani maendeleo ya miaka 50 unaweza ukayageuza ama ukayafanya kwa miaka mitano au kumi ?
Unafikiri kwamba serikali ndiyo inakumbuka kujenga miundo mbinu sasahivi ? Unafikiri awama zilizopita hazikuwahi kujenga ? Development ni progressive & gradual process broo ?
Fanya uchunguzi mwaka 1961 bara bara za lami tanzania zilikuwa ngapi na sasa ziko ngapi
 

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
30,904
2,000
Maana yangu ni kwamba "Tutoe fikra kwenye vichwa vyetu kuwa tunataka maendeleo ya watu siyo vitu kwa sababu vitu ndivyo vitaleta maendeleo ya watu

Serikali haiwezi kupa wewe hela bali itakuandalia mazingira ya wewe ufanye kazi upate hela, kwa hiyo tuache na dhana potofu kuwa bara bara zitatusaidia nink, ndege zitatusaidia nini, viwanda vitatusaidia nini. It is actually very worse
kwa akili fupi kama hizi zinajua maendeleo ya watu ni serikali kugawa hela. Muwe mnapitia pitia kujipa maarifa kabla ya kuleta pumba humu
 

Mr Lyanga

JF-Expert Member
Jun 20, 2020
502
500
kwa akili fupi kama hizi zinajua maendeleo ya watu ni serikali kugawa hela. Muwe mnapitia pitia kujipa maarifa kabla ya kuleta pumba humu
Wenye akili fupi na mgando ni nyie
😏😏😏 mnaopiga kelele kuwa tunataka maendeleo ya watu siyo maendeleo ya vitu.
Kwani maendeleo ya watu yanaletwa na serikali au na wewe mwenyewe.
Fanya kazi upate hela ujenge maisha yako, uache kuilaumu serikali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom