The king mswati
JF-Expert Member
- Jun 20, 2020
- 787
- 820
Waafrika bhan mimi sijui Genes zetu zilitoka kwa watu gani maana:
Bara maskini kuliko yote duniani ni Afrika.
Maendeleo ambayo yako chini (kiuchumi, kijamii, kisiasa n.k) kuliko mabara yote duniani ni Afrika.
Lakini my take ni kwamba, Hivi tunakumbuka kauli mbiu ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2005 alikuja na kauli mbiu ya kutuambia kwamba "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" vipi hii kauli mbiu ilifanikiwa au ndiyo iliishia kuwa ya propaganda ya kisiasa ?
Mimi nina imani haikufaulu na kuishia kuwa propaganda za kisiasa.
Hivyo basi kama haikufanikiwa, kuna hii ya Tundu Lissu kwamba ataleta "MAENDELEO YA WATU SIYO VITU" hii nayo itakuwa ya kisiasa tu haiwezi kufanikiwa chini ya Lissu hata iweje labda aiuze nchi 😁😁😁 kitu ambacho kitaleta majanga zaidi.
My take "Tufanyeni kazi kwa ajili ya kuboresha hali za maisha yetu na si kutarajia ahadi za wanasiasa kuwa watatuboreshea maisha yetu, that will be a mere dream"
Serikali jukumu lake siyo kukupa wewe hela mkononi.
Serikali jukumu lake siyo kukujengea wewe nyumba ya kuishi.
Serikali inatakiwa ishushe bei ya cement na mabati ili sisi tujenge.
Iboreshe miundo mbinu kama bara bara na umeme ili uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa zetu kwenda masokoni iwe rahisi.
Itafute masoko ya uhakika ya mazao yetu kama pamba,korosho na Mengineyo wanayolima wakulima ili wakulima wauze mazao yqo kwa bei za uhakika na waboreshe maisha yao.
Inabidi ijenge viwanda ili kuimarisha utengenezaji wa bidhaa za ndani sisi wenyewe na siyo kila kitu ni kuagiza china na kwingineko
Inatakiwa iboreshe sekta za afya madaktari wawepo wa kutosha, madawa yawepo ili kupunguza vifo visivyo vya lazima.
Sasa mshangilieni Lisu anae ponda maendeleo yanayofanywa na magufuli ambayo nyie mnaita ni maendeleo ya vitu,
Mpeni kura Lissu maana chini ya Lissu ni kweli haki tutaipata, uhuru tutaupata ,usawa tutaupata na katiba mpya pia tutaipata maana yeye si mwanasheria aliyebobea mnamwita hivyo.
Ila nna imani ndani ya miezi mitano tu ya mwanzo kuna watu mtarudi kulalamika hapa kuwa alituahidi maendeleo ya watu mbona mambo bado ni yale yale.
Hakuna Serikali duniani inayogawaga hela kwa watu au kuwajengea watu majumba ya kuishi bure.
Haipo hiyo Serikali kwa sasa.