Hivi mnajua tiba mojawapo ya kansa ya tezi dume ni pamoja na mwanaume kuhasiwa!

Papa Mobimba

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
1,153
1,359
Kwanza kabla sijaenda mbali nieleweke kwamba leo la thread hii sio kukuogopesha. Ama uogope au usiogope huo ndio kweli, kwamba tiba ya kansa ya tezi dume ni pamoja na mwanaume kuhasiwa (castration)

Hatari ya kupata kansa ya tezi dume huongezeka kadri umri unavyoongezeka. Vitu vingine vinavyomuweka mwanaume katika hatari ya kupata kansa hii ni pamoja na uvutaji sigara, pombe na kitambi.

Iwapo utawahi kugundulika kama una ugonjwa huu, ambao ni kansa ya pili kusababisha vifo miongoni mwa wanaume, matibabu yake ni kuondolewa tezi dume yote. Katika hatua kubwa za ugonjwa hasa ukishasambaa mgonjwa atahasiwa ama kwa kutolewa korodani zake au kuchoma dawa ya sindano.

Nina kushauri ufanye vipimo vya tezi dume hasa kuanzia miaka 50.
 
Back
Top Bottom