Hivi mfumo wa elimu kwa ulivyo sasa unatofauti ipi na pyramid schemes?!

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,627
Habari wadau?!

Hivi katika hali ya kawaida, mimi nikitazama mfumo wetu wa elimu tokea vidudu hadi chuo kikuu ni uwekezaji mkubwa sana wa pesa ambao hauna guarantee ya uhakika na ile hali wazazi wanawekeza mamilioni ya pesa kwaajiri ya watoto wao kipindi chote hicho lakini mwisho wa siku hakuna kinachopatiakana zaidi ya kuongeza umasikini wa kaya.

Hivi uwekezaji katika elimu kwa kaya masikini na ule msemo wao wa elimu ni ufunguo wa maisha, mbona ni kama kusema elimu ni kifungo cha maisha?!

Hivi kumwambia mtoto asome kwa bidii aje kufanikiwa, atapata kazi nzuri ya mshahara mnono na atasaidia kila mtu na kupata heshima kwenye jamii na ataishi maisha ya furaha, amani utulivu bila stress imeanza kuwa ni uongo mtakatifu?! Mbona ukweli ni kuwa wasomi ndio watu wanadharaulika katika jamii kwasasa kuliko kada nyingine, maisha yao ni ya wasiwasi sana, wamastress na mchango wao ni mdogo sana katika maisha ya wengine na ndio kada ya jamii inayoongoza kwa msongo wa mawazo na kukosa amani ya akili?!

Hivi sitakuwa sahihi kusema Mfumo wa elimu wa Tanzania ni largest pyramid schemes a.k.a Ponzi scheme ya karne?!

Mfumo wa elimu unatofauti gani na maswala D9, sijui Forever living, na zile network business zingine za kitapeli ambazo huwanunulisha watu bidhaa na kuwaahidi kujakuwa mabilionea...?!

Eti?!
 
Back
Top Bottom