Hivi mbona Tanzania kuna ombaomba sana

Hivi mbona Tanzania kuna ombaomba sana

Kiongozi mkuu anaomba,wananchi wake je?

Tulinganishe na nchi gani unataka wewe?
Hata somalia hawaombi kama sisi,hii ni dalili ya watanzania kuwa ni wakoma japo wanaonekana na viungo
 
Nenda India utasahau bongo, tena India wanakuja na watoto wachanga yani wana style za ajabu huruma itakujia tuu..
 
Haswa viongozi wa nchi na wakati nchi ina kila kitu ?

Kuna jamaa yangu alimua kudeal na issue ya omba omba miaka fulani uko nyuma, aliyokutana nayo....mh Mungu anajua..yani kuna tawala kuwaona omba omba mitaani ni furaha kwao kuwa wamefanikiwa.Hakika naamini Rais ajae imani yake haitakuwa ni ile ya kufurahi akiona omba omba barabarani.Rais ajae ni yule ambae akipita barabarani akiwaona anakwazika anajisikia roho/nafsi kukwazika na kukereketa kuwa kuna jambo aliko sawa na kuomba utatuzi ufanyike mara moja na suruhisho lipatikane wasikae mitaani ikawa mwisho.

Japo ni jambo la kihistoria kweli, lakini jambo hilo ukilifuatilia kuanzia nyuma lina mambo makuu Matatu
1: Ni Swala la Kiimani ndani yake
2: Swala la Kifamilia [Migogolo Mingi ya Kifamilia]
3: Swala la Kiuchumi- [Wengine Wamegeuza ni vitega Uchumi Vikubwa sana]
4: Mwenye wajibu wa Kulinda/Kuzuia na Kuelimisha atimizi wajibu.

1: Swala la Kiimani [Spirtual Feelings]

Hapa kuna mtoaji ambae anapita barabarani kwa mazingira ya kiiimani [Dini/Madhehebu] anakuwa na huruma /tashititi au fukuto la kuhisi kuwa kwa utoaji wake huo anajiweka karibu na Mungu wake kwa kuwasaidia maskini na wenye uitaji.Kwa kuendelea kuwapa walioko Mitaani basi wapewaji wanaongeza idadi ya waombaji wengine toka kwenye familia zao na marafiki wakiwemo majirani pia.Kama aliyekaa leo kwenye viunga vya Kariakoo na Fire-Dar au Makoroboi-Mwanza ataondoka na Shilingi elfu 30,000/= tegemea kesho ndugu yake mwingine ambae yuko karibu atavutika kuingia sehemu hiyo kwa kuwa tayari kwa jicho la pili ni chanzo cha mapato kisicho na mawaa na hivyo basi tegemea takwimu za omba omba kuongezeka maradufu kama sio mamilioni.

Katika swala hilo juu la kiimani mtoaji msaada ndiye mwenye imani kuwa anatoa ili katika fungu lake la kuhesabiwa na Mungu wake atamsikia na kumwesabia.NI kweli kiimani tunapaswa kufanya hivyo...lakini tushawahi kujiuliza Je kama unae mpa anaenda kununua ngono Ambiance Bar-Kijotanyama au ananunua na bangi mitaani kwa ile pesa uliyompa Mungu kupitia kwake. Je ni Kweli Umemepa Mungu au ...?. Nadhani nikatika kujiuliza tu!!! Sie watoa pesa mitaani tumekuwa wachochezi wakuu wa omba omba sana tena sana wazidi kuongezeka mitaani. Kwani ukitaka kutoa msaada na ukaamua kufanya utafiti wa kutafuta familia fukara isiyojiweza moja yenye shida za dhati toka mtaani kwako au eneo lolote la Tanzania na kila unapojisikia Utoaji wako ili unganike na Mungu wako kama Ibada basi ni vyema mtu akapeleka kwenye eneo halisi na sio hivi tunavyogawa pesa mabarabarani...ukweli tunachochea sie wenyewe.

Kuna namna nyingi ya kupata wahitaji wa kweli wa kuwasaidia kwenye maisha yetu huko mitaani...mfano kupitia Makanisani, Misikitini na Wazee wa Jadi tunaweza kupewa familia za kuzisaidia na hivyo kuwa na uhakika wa uhalisia ikibidi kuhakiki kile mtu alichotoa.Pia kupitia Serikali hasa Watendaji wa mitaa mtoaji anauwezo wa kupewa kaya maskini kwa kipato akazi udumia kama vile Wajane na Watoto yatima, vilema na wagonjwa.

Pia kwenye imani hiyo...michezo ya utamaduni wa Mwafrika usio mzuri, wa michezo ya kuchezeana kwa kufanyiana mambo mabaya katika kumtakia mwingine masahibu yasiyo pendeza kwa Wanadamu na Kwa MUngu.Hayo yanatendeka kwa nia tu ya kumkomoa.mtendewa na akiwa hana imani dhabiti katika Dini yake basi kombora litakalo lushwa kwa nia ovu yoyote ile basi ni nafasi pia kumfikisha mtaani mlengwa na kugeuka omba omba huku akili yake ikiwa si akili yenye afya.Na kwa kuwa zamani mambo haya ya michezo ya kiafrika yalikuwa na mahakama zake za wazee [wakiongozwa na machifu] waliweza sana kumudu kufanya wale wote wanaowatenda wengine kwa kuwakomoa basi hukumu ya kijadi dhidi yao ilisimama kwao na hivyo kuepusha michezo ya kuoneana ovyo ovyo pasipo huruma ya waja wa Mungu.

Mikoa ya Shinyanga hapo zamani kuliibuka magonjwa ya ukoma ...lakin yaliusishwa na ushrikina kabla ya kutambua kuwa ni ugonjwa.Kutengwa kwao wagonjwa kuliperekea ujenzi wa nyumba za kuwahifadhi wagonjwa hao-Mfano Shinyanga kulikuwa na Nkorandoto, Buhangija na Mwanza pia. Kwa kuwaweka pamoja wagonjwa hao waliokuwa wametengwa na jamii kwa imani ya ushirikina. Pia kwa mazingira ya nyakati hizo za ugonjwa wenyewe uliitaji karantini, na omba omba hao waliishi kwenye vituo hivyo ambavyo ni kama Nkorandoto-AIC na Buhangija -Roman Cathoric...na kwa support ya Serikali watu hawa walipata hifadhi njema na maisha yao kuendelea kwa amani chini ya ulinzi sahihi.

Lakini ujio wa Utandawazi na kutufanya kusahau UAFRIKA -katika ushrikiano wa kindugu wagonjwa hawa wametoka kwenye baadhi ya taasisi hizo na kuamia mitaani kushiriki kuomba...wakisafiri toka Mkoa mmoja mpaka mwingine na kugeuza maisha yao ni ya kuomba omba.

2: Swala la Kifamilia -Migogolo Mingi ya Kifamilai [Famiry Conflicts]
Hapa napo kuna kizaa zaa sana, ujio wa style mpya ya maisha ya watu kutokuwa na ule utamaduni wa maisha ya ushrikiano katika ngazi za familia katika kusaidiana na kuwasaidia wana ndugu wenye matatizo katika familia. Mfano kijana anawea kukana kuwasaidia wazazi wake na jukumu hilo la kuwalea wazazi likakosa mwanafamilia wa kuwasupport wazazi hao na hatimae wazazi wale kuishia kuwa omba omba.

Pia migogolo ya magomvi ya Baba na Mama kama wazazi wakigombana na kutalikiana basi hati hati ya watoto kuibukia kwenye malezi hatarishi yatakayo wafikisha kuwa omba omba, yana asilimia kubwa sana.Kwa kuwa watoto wanakosa wasimame wapi kwenye malezi hivyo uishia kutanga tanga.Na kama mmoja wa Wazazi hayuko kwenye uchumi mwema kuweza kulea watoto ama wote wawili hawana uwezo wa kusimama kiuchumi kuwalea watoto na wao wako kwenye mtafaruku basi ni bomu kubwa la kuwafikisha watoto na mama yao au watoto pekee yao kuingia mitaani kuwa omba omba.

Pia swala Mimba za utotoni na ngono hatarishi zimepelekea mabinti kuzaa watoto nao wakiwa bado watoto ama hawana uwezo wowote wa kulea watoto. Style hiyo ya maisha elmaalufu kama life ya USWAZI hii imezalisha aina fulani ya kaya zenye ugumu wa maisha unao sababisha wanafamilia wengi kuingia mtaani kutakufuta riziki za watoto-Si ajabu kwa Mwanadarisalama kukatiza mitaa ya Kariakoo, Fire, Posta na ilala au Mtaa wa Makoroboi-Mwanza, Arusha -Road ukakumbana na kundi la kina mama wakiwa na watoto wadogo mikononi na mgongoni.

Kuna kasumba ya tatizo hili ambalo imeenea kuwa ''Maskini na Watoto wake, tajiri na Mali yake''...Ukweli Ugumu wa masisha na ukosefu wa Elimu na hasa elimu ya Uzazi wa Mpango umezalisha aina ya kizazi toka viunga vya Uswahili-Uswazi-Tanzania nzima kuwaza sana kwenye ngono na ulevi [sex & alcholism ] kama liwazo la kupumbuza kaili zao kutafuta majibu ya ugumu wa maisha japo yana challenge nyingi kutokana na kutotimiziwa baadhi ya mambo ya msingi kuwawezesha wavuke.Japo ni kweli lakini hailalishi jamii kuwa Walevi na Wapenda ngino holela amabzo zimezaa jamii ya omba omba.

3: Swala la Kiuchumi- Wengine Wamegeuza ni vitega Uchumi Vikubwa sana-Economical Factor
Hapa kuna baadhi ya familia za Kitanzania zimeligeuza swala la omba omba kama swala la kiuchumi-Kuna watanzania wenzetu wanaotoka mikoa ya kanda ya kati haswa Dodoma swala hili kwao walio wengi ni la kiuchumi.Si kuwa watu hawa hawajiwezi na hawana mali bali kupitia style hiyo wanapata sana Mitaji na kuwekeza sana kwenye miradi yao vijijini kama kununua Ngombe, Vinu vya kusaga mazao, Mashamba na Mifugo na hata ujenzi wa nyumba.
Kupitia kwa waasisi wao kama kina Mzee Matonya basi ujumbe dhidi ya jukumu la kuomba kwenye majiji umetapakaa kwa wananchi wa kabila husika na hivyo kugeuza tendo ilo kama jawabu la mafanikio kiuchumi.

Na si wao tu wanaofaidika kuna watu kwenye majiji yetu wanao hifadhi PESA zinazokusanywa na omba omba hawa na kuwapa siku wataka kuludi nyumba kwao.Kama kila siku anaweka kima cha chini elfu 10,000/=- cha juu 40,000/= na ana miaka miwili ajaludi nyumbani kwao analala barazani kwa yuke anaehifadhi pesa hizo unategemea mwenye kuhifadhi akimpa ataondoka na shillingi ngapi...Je na mwenye kuhifadhi muda wote huo analudisha kama alivyozipokea yeye kafanyia biashara na kuludisha pesa isiyo na Riba Je kafaidikaje na game hilo.

Kwa kumegea tu omba omba ni swala lilikuwapo toka enzi na enzi kama ulivyo ukahaba...hakuna Serikli ya leo inayoweza kulimaliza kwa haraka mara moja lakini ni swala ambalo linaweza kuwepo kwa kiasi kidogo sana na si kuwa ni swala ukiliona likakukera nafsi.Manake hata ukiomba takwimu tegemea ushangaeee!!!!

Subira yavuta heri siku moja atapatikana Rais aliyelelewa kitanzania [Yani ujamaa wa kindugu] atajisikia vibaya na kuona kuna umuhimu wa kueradicate omba omba kwa kuimalisha vituo vilivyopo na kuanzisha vipya ili kuwaondoa mitaani na kuwafundisha elimu ya ujasiliamali kwenye vituo hivyo kabla ya kuwaresha majumbani mwao kwa wale wenye familia zao.

4: Mwenye wajibu wa Kulinda/Kuzuia na Kuelimisha atimizi wajibu.
Vyomo vya umma vyenye wajibuwa kulinda na kuzuia yasitokea haviwajibiki kwa swala husika nao wamebaki kuangaliahoja tatu za juu zikichukua hatua kwa kuwa kimsingi zenyewe ni za umma na si vyombo.Wkati kiuhalisia vyombo vya umma ndivyo vyenye uwezo wa kuliondoa tatizo kwa kutoa hata elimu juu ya tatizo husika na kuwaondoa wahusika toka maeneo ya mitaani na mabarabarani na kuwapeleka maeneo maalumu kama ilivyokuwa enzi ya Mwalimu Jk.
 
Back
Top Bottom