runyaga
JF-Expert Member
- Dec 23, 2013
- 523
- 241
Manji amewekeza hela zake nyingi Yanga, kama tunavyojua hakuna mfanyabiashara (Manji akiwa mmoja wapo) wanatengeneza hasara; hawezi kufanya kitu kisicho na faida.
Tumeshuhudia Manji akitoa hela yake nyingi kuigharamikia Yanga ikiwepo kulipa mishahara ya wachezaji na kulipa gharama zote za mechi ya TP Mazembe (japo anadaiwa) bila kuonesha faida anayoipata yanga.
Jana kamfukuza Mfaransa akiyeajiriwa kama mtendaji mkuu, japo yeye anasema hakuwahi kuona kazi yoyote ya kufanya chini ya Yanga yetu.
Ile mi nahisi ulikuwa mchezo wa kisiasa ili kuwadanganya wanachama kwamba sasa Yanga inaenda kuendeshwa kimataifa. Mkataba wake umevunjwa jana na lazima kuna malipo ya kuvunja mkataba.
Hizi gharama zote anazolipa Manji kwa manufaa ya Yanga yeye anafaidika nini?