Hivi malezi ya aina hii ni sahihi?

Hivi malezi ya aina hii ni sahihi?

KIRIKIOU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2014
Posts
241
Reaction score
57
Mara nyingi nimeona familia ambazo zina jiweza kiuchumi zinawalea watoto kama mayai vile kitu ambacho kwa mtazamo wangu nanona kama ni sio vizuri kwa sababu mtoto anakosa uelewa wa vitu vidogo vidogo vya "kidomestic"

Kwa mfano unakuta nyumbani kuna msaidizi wa kazi hgirl ambae anafanya kila kitu, kuosha vyombo, kufua kudeki, kupika na kadhalika.

Watoto hawagusi chochote hata kama ni mtoto mwenyewe anataka labda kufua au kupika anakatazwa na kuambiwa nenda kasome.

Kwa hiyo watoto kama hawa wanakuwa katika hali hoyo ya kujifunza domestic activities na pindi wanapokuja kujitegeme inakuwa issue.

Kwa mtazamo wangu malezi kama haya sio sahihi, Mtoto ajifunze kupika, kufua, usafi wa ndani n.k kwa faida yake baadae.

Regards
 
Hapo umeongea mkuu.
Mie ndio maana kwangu habari ya Housegirl sitaki hata kuisikia.
Wanangu wote wanajua kupika kwa kiwango chao,wakike 6 yrs na kiume 9 yrs.
Mie nilijua kupika mdogo sana,na ndio maana hata shule niliosoma ya boarding sikupata tabu.
Ila nilitengeneza pesa kweli wakati nip Shule,mana tulikuwa tunaruhusiwa kupika.Sasa wale Kukuboy hata chai walikuwa hawajui kuchemsha,basi wananipa changu wanaleta Menu mzee naingia mzigoni.Nili Make kweli.
Hili tatizo lipo sehem nyingi sana,ila kwa ufupi sio malezi kabisa,yaani siku hizi unaweza kukuta msichana mkubwa lakini hajui kupika na akipika basi anazabika.Wakiolewa tu wanajidai kutafuta Housgirl ili awapikie na wengine kibao wamejifundisha kupika kupitia wafanyakazi wao wa ndani.
Sie wengine wake hao ndio wangetushinda,maana sio wake ndoa,ila hao ni wake Papuchi tu.
 
hasa kwa watoto wakiume jamii zetu bado zinamchukulia mtoto wa kiume hawezi pika,osha vyombo.Mtoto ni mvulana hagusi kitu. Mara zote anaambiwa "Usihangaike babangu, kama ni nguo zako ntakufulia" Huyu mvulana yuko darasa la tatu kwa mfano na hafui wala kufanya kazi yoyote hapo nyumbani, anabembelezwa tu. Hata nguo zake za ndani anafuliwa. Chumba chake hagusi;kinafagiliwa na kudekiwa. Hii nimeiona kwa macho wangu na akina mama ndio wadekezaji wakubwa wa watoto wa kiume hasa pale mtoto huyo ndiye pekee wa kiume katika nyumba hiyo, au kama huyo mama alimzaa baada ya kuhangaika kwa kipindi kirefu kushika mimba. Mtoto anageuka kitu cha ajabu hajui kufanya chochote. MBAYA SANA WAZAZI TUBADILIKE.
 
Mara nyingi nimeona familia ambazo zina jiweza kiuchumi zinawalea watoto kama mayai vile kitu ambacho kwa mtazamo wangu nanona kama ni sio vizuri kwa sababu mtoto anakosa uelewa wa vitu vidogo vidogo vya "kidomestic"

Kwa mfano unakuta nyumbani kuna msaidizi wa kazi hgirl ambae anafanya kila kitu, kuosha vyombo, kufua kudeki, kupika na kadhalika.

Watoto hawagusi chochote hata kama ni mtoto mwenyewe anataka labda kufua au kupika anakatazwa na kuambiwa nenda kasome.

Kwa hiyo watoto kama hawa wanakuwa katika hali hoyo ya kujifunza domestic activities na pindi wanapokuja kujitegeme inakuwa issue.

Kwa mtazamo wangu malezi kama haya sio sahihi, Mtoto ajifunze kupika, kufua, usafi wa ndani n.k kwa faida yake baadae.

Regards

Watoto kama hao ndo watajapata shida sana baadae pindi wazazi wao hawatakuwepo ama watakapotakiwa kujitegemea wanashindwa na kung'ang'ania nyumba tu
 
watoto kama hao ndo watajapata shida sana baadae pindi wazazi wao hawatakuwepo ama watakapotakiwa kujitegemea wanashindwa na kung'ang'ania nyumba tu

ni kweli,,lakini wazazi wanachangia tatizo hili.
 
dawa ya malezi hayo ni wazazi kudanji tuu....... watafanya kila kazi......
 
Mtoto kakosa mzazi hamfokei wala kumuadhibu pale inapobidi mtoto hashiki chombo kala chakula kainuka kaacha na sahani hapo hapo mzazi anachekela tuu yaani huwasielewi wanategemea watoto waishije baadae mtoto hata kukaa kwa watu hawezi maana atahisi ananyanyasika .
 
Mara nyingi nimeona familia ambazo zina jiweza kiuchumi zinawalea watoto kama mayai vile kitu ambacho kwa mtazamo wangu nanona kama ni sio vizuri kwa sababu mtoto anakosa uelewa wa vitu vidogo vidogo vya "kidomestic"

Kwa mfano unakuta nyumbani kuna msaidizi wa kazi hgirl ambae anafanya kila kitu, kuosha vyombo, kufua kudeki, kupika na kadhalika.

Watoto hawagusi chochote hata kama ni mtoto mwenyewe anataka labda kufua au kupika anakatazwa na kuambiwa nenda kasome.

Kwa hiyo watoto kama hawa wanakuwa katika hali hoyo ya kujifunza domestic activities na pindi wanapokuja kujitegeme inakuwa issue.

Kwa mtazamo wangu malezi kama haya sio sahihi, Mtoto ajifunze kupika, kufua, usafi wa ndani n.k kwa faida yake baadae.

Regards

Uko sahihi kabisa lakini pesa ni kitu cha ajabu mno kinabadilisha watu mpaka unashindwa kuamini kuwa hivi huyu ndo yule fulani tunayemfahamu?
 
Mtoto kakosa mzazi hamfokei wala kumuadhibu pale inapobidi mtoto hashiki chombo kala chakula kainuka kaacha na sahani hapo hapo mzazi anachekela tuu yaani huwasielewi wanategemea watoto waishije baadae mtoto hata kukaa kwa watu hawezi maana atahisi ananyanyasika .

Ni malezi mabaya lakini ukiwa nazo ni vigumu kucontrol unakuta mwanafunzi ana simu kali na ya gharama kuliko walimu wake
 
malezi malezi malezi malezi malezi malezi........................................................
 
kwa jambo hili namshukuru sana marehemu mama yangu (Mungu amrehemu) maana utaratibu wake ulikuwa tukirudi nyumbani likizo na dada wa ndani anapewa likizo akapumzike kwao...anamwambia nenda tu ukasalimie nyumbani mwezi huu ma'housegirl wangu washarudi
 
hasa kwa watoto wakiume jamii zetu bado zinamchukulia mtoto wa kiume hawezi pika,osha vyombo.Mtoto ni mvulana hagusi kitu. Mara zote anaambiwa "Usihangaike babangu, kama ni nguo zako ntakufulia" Huyu mvulana yuko darasa la tatu kwa mfano na hafui wala kufanya kazi yoyote hapo nyumbani, anabembelezwa tu. Hata nguo zake za ndani anafuliwa. Chumba chake hagusi;kinafagiliwa na kudekiwa. Hii nimeiona kwa macho wangu na akina mama ndio wadekezaji wakubwa wa watoto wa kiume hasa pale mtoto huyo ndiye pekee wa kiume katika nyumba hiyo, au kama huyo mama alimzaa baada ya kuhangaika kwa kipindi kirefu kushika mimba. Mtoto anageuka kitu cha ajabu hajui kufanya chochote. MBAYA SANA WAZAZI TUBADILIKE.
Kweli kabisa KIRIKIOU.Unanikumbusha mvulana wa jirani yangu aliyekwenda formI boarding akashindwa kufua nguo zake. Wenzake walimfulia kwa kuwalipa. Aliporudi likizo nyumbani loo alishageuzwa mwanamke.Mamaake aliyekuwa anamdekeza akaugua presha kali akafa!

Wazazi, kumpenda mtoto si kumdekeza hasa akiwa mvulana. Madhara ni makubwa sana.
 
Last edited by a moderator:
Siwezi wapa tabu vijana wangu ikiwa mzazi wao bado nipo hai na uwezo ninao. Watasubiri mpaka nife lakini kwasasa hapana kwakweli.
 
Ni sahihi lakini ni lazima na muhimu uwafundishe self reliance na upande wa pili wa maisha, waliofanya hivyo wamefaidika kwakuwa watoto wameweza kusimama na kusonga mbele pale ulipokomea, walioshindwa wanewaachia watoto majanga
 
hii kitu itaendelea hivi hivi miaka mia kwan ndio ukapitalist survival of the fitest
 
upo sawa kabisa kuwalea watoto katika maadili hayo mbaya sana ndio yale yale kama ni wakike wakiolewa wanaachika sababu hajui kufanya lolote
 
Back
Top Bottom