Hivi mahari na michango ya harusi ni nini haswa?

eddy brown

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
393
500
Hivi niwaulize wadau wa JF,

Kwanini mtu unadaiwa ulipe mahari ndo uweze kuoa au kuolewa ni muhimu kwa pande zote.

Nilipata bahati ya kutembea na kuishi nchi nyingi na sijaona watu wakidaiwa mahari au michango ya harusi kwanini kwetu huku inakuwa ndio dili?

Hivi wanaume wakigoma kulipa mahari ndoa hazitokuwepo? Tunajifanya tunapenda kuiga mbona hatuigi hili.

Tunapendana tuoane na harusi tugharamie wenyewe. Kwani huko mbele kama ni raha au shida ni zenu wenyewe.

Tusipende ujinga.
 

Vitalis Msungwite

Verified Member
May 11, 2014
2,114
2,000
Hahahahahahahhahahaha ukikua na kufikia umri wa kuoa utaelewa kwasasa naona umepata kadem ambako unahis utapigwa sana kwahiyo unatafuta huruma huku .
Kuna baadhi ya wazazi hawadai hata sent na maisha yanaenda wengine hudai hela kidogo ya kutolea baraka haizidi laki 5, but wapo wafanyabiashara wao mahari ni 5mil +,kabla ya kuoa tafiti kwanza ili usikosane na wakwe zako.
 

Dionize N

Verified Member
Oct 22, 2012
1,598
2,000
huo ni utaratibu tu wa kiungwana ambao waungwana wamejiwekea, hata hivo mahali si lazima kwa kila familia na hata michango ya harusi si lazima saana kwa mfano ww mleta maada sitegemei kama utakuja kuwachangisha watu katika harusi yako kwa sababu ushaona kuwa hilo ni tatizo kwahiyo utasimamia show nzima mwenyewe
 

eddy brown

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
393
500
Mi nimeshao mzelu zelu wa huko majuu miaka 24 ilipita, ila ninarudi huku ndo nakuta haya mambo, utamaduni wa mahari kweli niliuacha na mke wangu wa kwanza wa hapa nilitozwa mahari, ila michango ilikua hakuna na sielewi michango ilianzaje.
 

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,773
2,000
namdharau mwanaume ambaye haoi bila mahari, binafsi lazima nikupe mahari ndo nioe mwanao, nitathibitishaje kuwa mimi ni dume la haja?
 

Roger Sterling

JF-Expert Member
May 10, 2015
12,311
2,000
Nadhani mahari ilileta maana zaidi zamani, cos mke alikuwa na majukumu ya kuitunza na kuiangalia familia wakati mume anatafuta mkate. Kwa hiyo kimsingi, ulikuwa unalipia zile huduma ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa covered na wasaidizi wa ndani siku hizi.

Michango ni utashi wenu tu wahusika. Binafsi naiona haina maana pia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom