Hivi Laana ni nini?

Hawa wao walilaaniwa na mungu ?! Mbona watu humsingizia shetani ndiye mwenye kulaani watu na sio mungu?!
OK, laana zote zinatoka kwa Mungu na sio watu tunakua tunajidanganya tu.
Na mara nyingi anaelaaniwa ni yule ambae atakua anatenda Dhabi ambazo zimezidi kiwango...
Kwa mfano kusema "hakuna Mungu" hii ni laana kwa huyo mtu ambayo atalaaniwa na huyo ambae anasema hayupo angali yupo.
Vipo vitu vitu duniani ambavyo vimelaaniwa na hata mtumiaji akiwemo.
 
Hivyo Hekima, Heshima na Busara ndiyo chanjo au ya laana?! Unapataje hekuma na busara kama hunazo?! Je laana hutolewa na Wazazi au ni mungu hutoa hii laana?! Wazazi wana umri stahiki wa kutoa laana au mzazi umri wowote anaweza kulaani?! Vipi mtu asiye mzazi wako anaweza kukulaani pia?! Sifa za mlaani au mtoa laana ni zipi?!
 
Hapa nahitaji elimu, huwa nasikia dhambi zina uzito sawa kwenye mzani wa mungu, kwamba hakuna dhambi kubwa wala ndogo. Unaposema unapata laana kwa dhambi zilizozidi kiwango, kiwango cha kawaida cha dhambi ni kipi na nikiasi gani unakua umezidi/umezidisha?!
Kwa maelezo yako ni mungu tu ndiye anatoa laana, kumbe hii nadharia ya wazazi au babu/bibi kulaani ni uongo tu?! Na nikimkosea mungu tu ndiye atanilaani na ndiye mwenye mamlaka, vipi nikikukosea wewe na nisikuombe msamaha, hii ikoje?!
 
mkuu umeelewa tofauti, laana sio kukosekana kwa pesa hapana, haiko hivyo duuh!!* kiufupi mimi siwezi nikakusababishia wewe ulaanike kw matamko tuu!!, nilitoa mfano kama ulinisoma, kwmba laana nikitu kikubwa sana, ukitaka kujuwa laana ni nini mpige mama yako au mtukane, au fanya kitu kibaya chochote kw mzazi wako kwa makusudi, yaani kusudia kufanya kitu kw wazee wako, huu ni mfano wa haraka haraka tu,, lingine em telekeza family yako kwa makusudi tu, Jamba ambalo mungu mwenyewe anahudhunika, **** jamaa alitelekeza familia yake yaani mke tena anamtoto mchanga kabisa, siku moja akarudi nyumbani Saa 9 mchana akamkuta mama anabembeleza mtoto wake akamsalimiavkabla mama hajaitikia salam mtoto akamsemesha baba yake, kwa mara yakwanza mtoto mchanga akaongea kwa kumwambia Baba kwanini Unatutesaa???# mtoto hakurudiavkusema chochote,, Na baba aliondoka kama kaenda kukojoa ndo mazima hadi leo zaidi ya miaka 20* hajulikani alipo wala fununu.
 
Hahaha huwa wanasema eti huu uongozi umelaanika, kumbe siasa tu. Wanapotoa/kutumia hili neno (laani) huwa ni katazo au tangazo?!
 
Ukiangalia mambo yanayofanywa na serikali ya Tanzania utaelewa nin maana ya laana. Mfano mwanasiasa eg. Mbunge ambaye hajasoma na kaipata kazi yake kwa rushwa na wizi wa kura tena kwa kupga kelele majukwaan kwa muda wa mwezi mmoja tu analipwa vizur na anaenjoy maisha zaid kuliko daktari aliesomea kazi yake miaka 5 tena kwa mkopo ambao ni lazima alipe huk akilipishwa kodi kubwa akinyimwa haki zake za msingi kama nyumba(malazi) na usafiri pale anapoajiriwa hata vya mkopo. Mfano mwingne pale kiongozi anapohimiza wananchi wachague kiongozi wa chama tawala ili wasipatwe na madhira ya kubomolewa nyumba zao pale watakapochagua kiongozi toka upinzan. Hii ndo maana halisi ya laana. In shot ukipata laana unafanya mambo bila commom sense. Binafsi nimeshindwa kabisa kua mzalendo kwenye hili taifa lililojaa laana.
 
Laana ni deni ya kisasi cha mtu kwa mtu aliemkosea against pure coincidences ya matatizo yanayompata yule mtu mkosaji..Hakuna scientific correlation kabisa!
Naamini wote tunakoseana at one point in life, ndii kusema woote tumelaanika/tumelaaniwa.
Matatizo watu husema ni sehemu ya maisha, ni matatizo kiasi gani ukipata utasema hii ni laana na ni kiasi gani utasema hii ni kawaida/sawa na sio laana.
Kwa maana yako Laana is direct proportional to dhambi/makosa/matatizo. Laana nyingi matatizo mengi, laana kidogo matatizo kidogo?!
 

Swali lako ni zuri lakini linahitaji mjadala mpana Kama topic inayojitegemea!
 
Hivyo serikali imelaanika?! Nani kailaani?! Hawa watawala wamelaanika?! Operational standard ya serikali ni ipi ili tuifuate, yani tuipe scale kwamba hapa normal, hapa below na hapa ni high au beyond normal ili ikifanya tunajua hii ni abnormal, and it is out normalcy.
Duh Laana siyo mchezo.
 
Swali lako ni zuri lakini linahitaji mjadala mpana Kama topic inayojitegemea!
Hahaha anzisha uni tag tueleweshane. Au tiririka hapa kwa faida ya JF members, it is gratifying to dare to empty with no fear or malice or prejudice.
Leta vitu mkuu hii JF hakuna limit panuka tu.
 
Dhambi zinazidiana kuna kubwa na ndogo, kuzini kunatofautiana na kutukana wazazi wako.
Hahaha huu mzani wako wa dhambi au wa mungu /high power?! Unatumia kigezo/standard gani kuipa zinaa uzito mkubwa au Tusi kwa mzazi linakuwaje na uzito mkubwa kuliko tusi kwangu au kwako?! Nimewahi kuambiwa dhambi ni dhambi tu hakuna iliyo kuu. Nitaanza kuzipima inawezekana una point nisiyoiona.
 
Mfano wa mafanikio ni Kama vile;
Umeshawahi kuona Mtu ana Mali Kama vile majumba lakini wanaofaidika ni watu baki!
Wapangaji wanaishi hawalipi kodi wala nini !
Yani sijui ni semeji
 
Mfano wa mafanikio ni Kama vile;
Umeshawahi kuona Mtu ana Mali Kama vile majumba lakini wanaofaidika ni watu baki!
Wapangaji wanaishi hawalipi kodi wala nini !
Yani sijui ni semeji
Kwa mfano wako nilidhani huyo mtu sasa ana neemeka kwa baraka kusaidia wenzake?! Mpangaji halipi kwamba hataki au mwenye nyumba hapokei pesa kwa sababu kalaanika?!
Hivi ile kusaidia bila kujali au kiebrania mnaita good samaritan au kujitolea ina maana gani ikiwa kila kitu kinapimwa kwa faida.
Ni lini mtu atapata baraka/rehema au positive karma kwa kusaidia wengine/watu baki.
 


Mshua

Yaani sentensi yangu ya pili nimeikataa kabisa ile definition ya kutoka sentensi yangu ya kwanza.Definition yangu ni very abstract,ni hypothetical ambapo kiuhalisia si kweli...

Unachokisema ni sawa kabisa.Ni ishu very subjective,na kitu kishakua subjective kinakua si halisi kabisa.

Laana ni kitu kisichokuwepo kiukweli...Ni hypothetical belief tu mkuu.

Yaani nakuelewa sana jembe!
 
umemaliza mkuu, kiziwi hawezi kisikia hata ukipiga kipenga ktk masikio yake
 

kwa aliyekusudia kufanya hivyo kwa ajili ya kusaidia watu yaweza kuwa baraka.
Lakini kwa Mtu mwenye laana yeye Hata hajielewi yupo yupo tu!
Nimependa michango yako iko na changamoto ndani Yake !
 
Hahaha karibu tuendelee kuchangia, tueleweshane zaidi.
kwa aliyekusudia kufanya hivyo kwa ajili ya kusaidia watu yaweza kuwa baraka.
Lakini kwa Mtu mwenye laana yeye Hata hajielewi yupo yupo tu!
Nimependa michango yako iko na changamoto ndani Yake !
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…