Hivi Dawasa wataendelea kutegemea mvua zinyeshe ndio maji yatoke hadi lini?

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,628
Hivi jamani hawa Dawasa wataendelea kuishi kwa kutegemea maji ya mvua hadi lini?Nasema hivi kwasababu ni nusura ya mungu tu mvua imenyesha mikoani haswa morogoro na Iringa ndo maji yakafurika kwenye mito ndo na huku tukaanza kuyaona mabombani.

Haya mambo ni hadi lini?Jee kila mwaka November na kiangazi tutakua tunapata shida za maji tu?

Mwaka jana November sinema ilikua ni hii hii tu walidai kuwa maji yanachepushwa, mwaka huu wamesingizia ukame na mwaka ujao sijui watasingizia nini.

Kwanini serikali isije na mkakati wa kuchimba kisima kikubwa kabisa chenye uwezo wa kuhudumia mkoa nzima wa Dar es Sallam badala ya kulia lia na mto Ruvu tu?

Sio hayo tu sote tunafahamu kuna mito kibao kama Rufiji ambayo huishia kumwaga maji baharini kwanini tusielekeze nguvu humo?

Hivi serikali ikiamua kuchimba kisima kikubwa cha maji safi yasiyokua ya Chumvi mbona inawezeka mbona?

Maana Mkuranga na Sehemu nyingi tu za Dar ya kusini hakuna shida za maji maana watu wamechimba visima na wanayasambaza kama Dawasa.

Mbona ishu ya maji ni very Easy tu wakisema hawana fedha kwanini wasiyape makampuni binafsi kandarasi za kuhangaikia ishu za maji serikali ijitoe huko?

Yaani kusingizia ukame ni ulimbukeni wa karne ya 21 mnasingizia ukame?Hapa ni Africa tu mnasingizia ukame na huko Israel na uarabuni pakame na jangwa wasemeje wao?

Hii nchi sijui kailoga nani yaani sijui tunakosa viongozi wenye maono?Haya mambo ni very easy ni suala la kuwaza na kuamua tu.
 
Kwa mujibu wa tafiti Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye adhina kubwa ya maji yaliyo kwenye ardhi. Licha ya ayo tuna ziwa tanganyika ziwa nyasa ziwa Victoria ziwa manyara.

Kinachosikitisha bado tuna tegemea maji ya mito tangu mwaka 1960 kweli. kama tutaendana na kasi ya technology maji sio shida kwa nchi yetu ni swala la mahamuzi tu kwa wizara husika..
 
viongozi wa dini si wapo.mvua zikigoma wanapiga maombi inanyesha miaka yote hizo ndo akili za watu wanaoongoza nchi.
 
Wana single yao ya bwawa la kidunda, naona ndo itakuwa ina hit nyakati hizi....
 
Kwa mujibu wa tafiti Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye adhina kubwa ya maji yaliyo kwenye ardhi. Licha ya ayo tuna ziwa tanganyika ziwa nyasa ziwa Victoria ziwa manyara. Kinachosikitisha bado tuna tegemea maji ya mito tangu mwaka 1960 kweli. kama tutaendana na kasi ya technology maji sio shida kwa nchi yetu ni swala la mahamuzi tu kwa wizara husika..
Nchi ya ajabu sana
 
Hivi ni kweli wameshindwa ku come up na mpango wa kuchakata maji ya Bahari kuwa safi na salama kwa matumizi ya Binadamu?

Na wapo wanazunguka kwenye viti, wanalipwa mishahara, wanakula incentives kibao kama watumishi wenye msaada kwa serikali? Bahari ipo mita 800 kutoka ofisi ya Dawasa! Kuna la kujitafakari kwa kweli!
 
Hivi ni kweli wameshindwa ku come up na mpango wa kuchakata maji ya Bahari kuwa safi na salama kwa matumizi ya Binadamu? na wapo wanazunguka kwenye viti, wanalipwa mishahara, wanakula incentives kibao kama watumishi wenye msaada kwa serikali? Bahari ipo mita 800 kutoka ofisi ya Dawasa! Kuna la kujitafakari kwa kweli!
Nchi hii kbs?
 
Huo mchakato unagharama kubwa sana. Ukiona wamisri wanang'ang'ana na limkataba la miaka ya ujima la mto nile wakati pembeni wana shamu na meditrania bahari. Fikiria mara mbili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nadhani long term plan ni kuchimba visima upstream (Bagamoyo/ Pwani/) and not downstream (Mwananyamala/ Buguruni)

si ajabu kwa baadae ruvu ikaja nyauka kauu kauuuu endapo hatutopanda miti kwa wingi na kutunza vyanzo vya maji Morogoro na Iringa.
 
Kule maeneo ya goba na mbezi waliishia kulaza mabomba na kusepa, mwaka wa pili huu...
 
Kikubwa ni kuangalia label yao ili kuona kilichomo ndani na faida kwa public health perspective.

Ukiangalia level ya Na(sodium) kwenye kilimanjaro ni kubwa sana ambayo kwa mwenye pressure na hypertension au dalili, siyo mazuri na haitakiwi kuyatumia.

Tulisoma kwenye food microbiology, public health na animal microbiology na kuona kuna maji ambayo ni sahihi kwa matumozi husika kama kunywa, kutumia nyumbani, kwa ajili ya mifugo na mengine hayapaswi hata kutumiwa

Tulifanya coliform test na MPN test na confirmatory test kwa baadhi ya bidhaa za hapa ndani kama jiuce na maji na kugundua mambo kadha wa kadha.

Kikubwa kama utaweza kuchemsha maji ni vyema kufanya hivyo, kama una matatizo ya moyo achana na Kilimanjaro.

Tuwe na utamaduni wa kuangalia kwenye label(lebo) ya bidhaa husika ili kuepukana na dhahama za kujitakia.
View attachment 2458448
Una uhakika na unachokisema au umeamua kuvuruga biashara za watu, kusoma food microbiology tayari umeshakuwa daktari.....wabongo bhana kishule kidogo ujuaji mwingiii, ndo maana mtu kama msukuma naye anatamba kuwa msomi wa kiwango cha PhD, kumbe chenga tu.​
 
Tunaenda na fact, siyo kama mpiga maneno wewe hapo, nakuona kama msukuma tu, afu nimekosea hii comment siyo ya hapa.
 
Tunaenda na fact, siyo kama mpiga maneno wewe hapo, nakuona kama msukuma tu, afu nimekosea hii comment siyo ya hapa.
Hakuna fact hapo wewe kilaza, weka utafiti wako ulioonyesha kwamba maji ya kilimamnjaro yaliwaathiri watu wenye hypertension, au peleka hizo facts TBS ili hayo maji yaondolewe kwenye soko ukiambatanisha na utafiti uliofanya.

Au kingine unachoweza kufanya wewe kilaza katoe presentation kwenye chama cha madaktari Tanzania uwape hizo facts ili kwenye mapendekezo yao waishauri serikali kupitia TBS kuondoa hayo maji sokoni kwani yana madhara kwa watumiaji, au yawekwe pharmacy yauzwe kama drip kwa wagonjwa wenye hypotension.

Mbali na hapo utaonekana kilaza pro-max na unaweza hata kushtakiwa kwa kuharibu brand za watu.​
 
Bogus.
 
Back
Top Bottom