Amanikwenu
Senior Member
- Dec 1, 2009
- 187
- 0
Hali ya Vifaa katika Hospitali yetu ya Muhimbili inasikitisha sana na ninachelea kukubali kuwa inastahili kuitwa Hospitali ya Taifa. Hivi inaingia akilini kweli kwa Hospitali ya Muhimbili kuwa na Mashine moja tu ya kupima moyo (ECHO Mashine)? Kwa mgonjwa anayelipia shilingi elfu 50 chini ya utaratibu wa Fast Track inabidi asubiri si chini ya siku tano ili kupata huduma hiyo. Kwa wale ambao hawawezi kulipia Fast Track muda wa chini wanaotakiwa kusubiri ni miezi mitatu. Aibu nyingine kubwa ni kuwa Muhimbili haina huduma ya DIALYSIS. Na huduma ya UTRASOUND nayo ni balaa tupu. Hii ni sehemu ndogo tu ya Matatizo ya Hospitali ya Muhimbili. Mashine ya ECHO gharama yake haizidi shilingi milioni 50 wakati zile za DIALYSIS gharama yake ni kama shilingi milioni 14 kwa mashine moja. Mbaya zaidi kuliko yote ni uhaba mkubwa wa Madaktari Bingwa hapa nchini. Ni ngumu sana kusikia kuwa katika eneo moja la ujuzi kwa upande wa udaktari kuwa kuna madaktari bingwa wanaofikia watano (ukiachilia wale wa akina mama).
Ni muhimu sana kama taifa tukatengeneza mpango wa kudumu wa kuwa tunazalisha madaktari wa kawaida wasiopungua 2000 kila mwaka na Madaktari Bingwa wasiopungua 200 kila mwaka kuanzia mwaka 2014. Vijana wanaotaka kuwa Madaktari Bingwa wapo wengi tatizo ni ufadhili. Tukiwekeza angalau shilingi bilioni 25 kila mwaka kwa ajili ya kusomesha Madaktari Bingwa natumaini ndani ya miaka 15 ijayo tutakuwa mbali. Tukumbuke kuwa Daktari mmoja hapa nchini kwa sasa anawajibika kuwahudumia Watanzania wasiopungua 33,333.
NAWASILISHA.