Hivi Kweli Muhimbili ni Hospitali ya Taifa????

Amanikwenu

Senior Member
Dec 1, 2009
187
0
Hali ya Vifaa katika Hospitali yetu ya Muhimbili inasikitisha sana na ninachelea kukubali kuwa inastahili kuitwa Hospitali ya Taifa. Hivi inaingia akilini kweli kwa Hospitali ya Muhimbili kuwa na Mashine moja tu ya kupima moyo (ECHO Mashine)? Kwa mgonjwa anayelipia shilingi elfu 50 chini ya utaratibu wa Fast Track inabidi asubiri si chini ya siku tano ili kupata huduma hiyo. Kwa wale ambao hawawezi kulipia Fast Track muda wa chini wanaotakiwa kusubiri ni miezi mitatu. Aibu nyingine kubwa ni kuwa Muhimbili haina huduma ya DIALYSIS. Na huduma ya UTRASOUND nayo ni balaa tupu. Hii ni sehemu ndogo tu ya Matatizo ya Hospitali ya Muhimbili. Mashine ya ECHO gharama yake haizidi shilingi milioni 50 wakati zile za DIALYSIS gharama yake ni kama shilingi milioni 14 kwa mashine moja. Mbaya zaidi kuliko yote ni uhaba mkubwa wa Madaktari Bingwa hapa nchini. Ni ngumu sana kusikia kuwa katika eneo moja la ujuzi kwa upande wa udaktari kuwa kuna madaktari bingwa wanaofikia watano (ukiachilia wale wa akina mama).

Ni muhimu sana kama taifa tukatengeneza mpango wa kudumu wa kuwa tunazalisha madaktari wa kawaida wasiopungua 2000 kila mwaka na Madaktari Bingwa wasiopungua 200 kila mwaka kuanzia mwaka 2014. Vijana wanaotaka kuwa Madaktari Bingwa wapo wengi tatizo ni ufadhili. Tukiwekeza angalau shilingi bilioni 25 kila mwaka kwa ajili ya kusomesha Madaktari Bingwa natumaini ndani ya miaka 15 ijayo tutakuwa mbali. Tukumbuke kuwa Daktari mmoja hapa nchini kwa sasa anawajibika kuwahudumia Watanzania wasiopungua 33,333.

NAWASILISHA.
 
Mabel

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
1,134
1,500

Nchi hii ina mengi makubwa na mapana zaidi ya matatizo ya muhimbili, Kihandisi Mitambo tunasema inahitaji OVERHAUL, je nani wa kufanya?
 
A Lady

Senior Member
Apr 28, 2009
103
0
Sidhani kama huu ni muda wa kulalamika! Haya mambo yanajulikana na WATZ wamekubali hali hii. Huu muda ni wa kuvumilia maumivu had hapo mtakapopata nafasi nyingine ya kufanya mabadiliko. Na msipofanya mabadiliko tena basi ni lifetime ya maumivu. Watu hawaelewi somo! Si mnapenda amani! Basi mkale na kutibiwa na amani yenu!
 
Edson

JF-Expert Member
Mar 7, 2009
9,455
2,000

imebidi niheke kidogo..... mleta mada kasema kweli.... ile hosp haina kitu bali wizi tu.....mkuu wa kaya nae sasa hivi hovyo kabisa yupo yupo tu anazid kukondeana... tusubiri miaka mitano mingine na kama hali itabaki kuwa hivi basi ni maumivu mpaka mwisho......

we fikiria mtu aliulizwa hiv: mna matatizo gani nchini kwako...akajibu tunasumbuliwa na malaria... akaulizwa tena kwa hiyo tuwape msaad gani akajibu ..... tunaomba vyandarua!!!! nani alikwambia chandarua kinamaliza tatizo la mbu?!!!
 
Kizibao

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
951
500

Mimi naona hata kuiita Hospital pia naona kinyaa.Haiwezekani ni mtu anamaliza master tu ndiyo tunamuuita dakrtari bingwa wakati yanayofanyika madudu matupu....wageni wanaofika Tz ukawaambia ndiyo Muhimbili ndiyo hospital ya taifa sasa wakiiona ile hali iliyokuwepo pale basi ndiyo anakuuliza hizo hospital za wilaya ziko hali gani kama hii ya Taifa ni uozo mtupu. na kitu chengine napenda kutoa ushauri usifanye Ultra sound muhimbili kwa hiyo report utakayopewa ni sawa na kutokufanya na kuhusu kipimo cha Moyo(ECHO) hakuna mtaalamu aliye specialize na anaekubalika kwa kufanya kipimo hicho muhimbili wote wanabahatisha tu. wamemaliza internal medicine leo mtu anakuwa mtaalamu wa echo.hiyo iko tanzania tu.na mtu anadengua kwa kujifanya mungu mtu.
 
Lasikoki

JF-Expert Member
Jan 10, 2010
640
195
@ kizibao kufanya ECHO inahitajika training ya muda gani? Je daktari bingwa anatakiwa kula ya qualification zipi zaidi ya kuwa na
 
Kizibao

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
951
500
@ kizibao kufanya ECHO inahitajika training ya muda gani? Je daktari bingwa anatakiwa kula ya qualification zipi zaidi ya kuwa na
Simchezo.. mtu wenye master huwezi kumuita daktari bingwa kwa mfano umemaliza master master yako internal medicine(kwa bongo) baadae baadae ukasomea cardiology( kama ni fellow au master of science) baada ya kumaliza hapo ukafanya postdoctorate research yako kwenye heartfailure au hypertension.. mimi hapo naweza kukuita daktari bingwa kwa sababu najua nikiwa na tatizo la blood pressure wewe ndiyo mtaalam au nikiwa na tatizo la heart failure wewe ni bingwa lakini leo unamaliza general internalmedicine ndiyo daktari bingwa hiyo haikubali duniani ispokuwa tz. au mtu anamaliza general OB&GY anakuwa dakrati bingwa wa maradhi ya kina mama haiwezekani.... sasa nenda bongo waulize hao wanaotwa mabigwa muulize yeye ni obstetric endocrinologist,fetal metanal au gynecology malignancy atakuambia yeye yuko general wakati haiwezzekani kwani ukiangalia najua superficial tu na hayuko deep ku solve complex problem..kwa hivyo mimi daktari bigwa atleast ile sehemu ameifanyia post doctorate pamoja na experience ya miaka mingi huyo tunamuuita daktari bingwa. na kuhusu Echo ni kuwa mtu baada ya kumaliza kusoma cardiology basi huwa anafanya fellowship ya ECHO kwa miaka 3 na baada ya hapo hiyo hiyo ECHO kuna subspeciality zake. ukichanganya na experience.sasa huyo mtu nitaziamini report zake na siyo leo mtu amemaliza general internal medicine anakuwa mtu wa kutegemewa kwa ECHO....no way matokeo yake ndiyo unaona report za muhimbili madudu matupu
 
Skype

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
7,275
1,195
Hospitali ya taifa???
Watu wanapasuliwa vichwa badala ya miguu na miguu badala ya vichwa!!!
Nanyamaza:teeth:
 
Tekelinalokujia

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
353
225
imebidi niheke kidogo..... mleta mada kasema kweli.... ile hosp haina kitu bali wizi tu.....mkuu wa kaya nae sasa hivi hovyo kabisa yupo yupo tu anazid kukondeana... tusubiri miaka mitano mingine na kama hali itabaki kuwa hivi basi ni maumivu mpaka mwisho......

we fikiria mtu aliulizwa hiv: mna matatizo gani nchini kwako...akajibu tunasumbuliwa na malaria... akaulizwa tena kwa hiyo tuwape msaad gani akajibu ..... tunaomba vyandarua!!!! nani alikwambia chandarua kinamaliza tatizo la mbu?!!!

Hahahahaaa unajua wakati wa mchakato wa uchaguzi mpaka sisiem wanajishindisha nilikua sitegemei watanzania wataruhusu hilo litokee ila ndio ikawa hivyo, sasa nikisikia mtu analalamikia matatizo kama haya saizi najaribu kufikiria wakati wa kupiga kura alikua anafikiria nini? maana aliepigia kura chama mbadala hawezi kuwa anazungumza hivyo leo bali atakua anazundumzia katiba mpya. alafu hawahawa wanaojifanya kupinpoint matatizo tanzania ukiwauliza vipi kuhusu sirikali na uongozi wa sisiem watakuambia sisiem juu.:crazy:
 
Mchapakazi

Member
Feb 24, 2008
67
0
Msiwe mnaongea ongea tu kama vile mnatumia lower GI kufikiria. Aliyeleta mada ni daktari so what? Kuna shida au hakuna shida.
Wewe mtu unayejaribu kutoa tafsiri ya daktari bingwa unajua serikali yako inatoa kiasi gani cha hela kwa ajili ya kufanya utafiti kama Grants..Zero, sifuri ngocho. Hao mafellow watafanya utafiti na nini? Nchi nyingi za Africa watu wanaishia MMED na wanafanya kazi nzuri tu kwa mazingira yaliyopo.
Unajua unapochukua uchafu wa system au baada ya kukubaliana na upuuzi na kukataa mageuzi usije ukarudi nyuma na kuanza kutafuta victims wa kulaani.
Kuna mtu kasema madaktari wasomeshwe, kama unasomesha halafu unamlipa dollar 300 kwa mwezi akienda tu hapo Malawi anapata zaidi ya mara kumi au hapo Rwanda ambapo ukiangalia kwa makini kama una hela Malawi ni karibu kuliko Rukwa na Rwanda na Bukoba hamna tofauti kwa nini akae. Unless ni kilaza na hajiamini anachotaka maishani. Kwa taarifa yako wataalamu wapo ila wansonga mbele kuacha mliokunywa maji ya sox muendelee kupigika.
Kichwa na mguu: Medical errors zipo kila mahali duniani and you should not insinuate this. Kilichotokea Muhimbili sio mara ya kwanza duniani usitumie hilo kosa la mtu mmoja kama kipimo cha wafanyakazi karibu 7000 wa Muhimbili.
Mbuzi anakula urefu wa kamba yake kwa kukumbatia mafisadi baada ya wao kula resources makapi ndo hayo ECHO moja hospitali nzima na kulala chini kama kawa!
 
Lasikoki

JF-Expert Member
Jan 10, 2010
640
195
@kizibao wewe ni daktari? Umesoma wapi? Cuba au? Ndugu yangu ECHO haisomwi kwa miaka mitatu!! Duhh! Kwa hiyo tuwe na ECHOlogists siyo? Vascular and Cardiac ultrasound or ECHO can be learnt fully in 3 months and 4 sure it's not a big deal or big school learning how 2 do an ECHO....kuwa specialist medical doctor you need a training at masters level 4 the respective field of medicine. One may then do super specialized training for example dealing with gynaecological oncology for the case of obs and gyn people or nephrology for internal medicine etc etc etc. The whole issue of research work or post doctoral work is meant for researchers and academicians and it's not really a necessity of practitioners or clinicians. Don't forget medicine is an art when it come 2 practise. You might have 10 pHD and then you fail 2 diagnose malaria or fail 2 build rapport with a patient.....
 
Amanikwenu

Senior Member
Dec 1, 2009
187
0
Asante kwa michango yenu. Natumaini wahusika wamesikia. Kitaaluma mi si Daktari. Siku njema kwenu wote.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom