Wapendwa,
Naomba leo kujadili swala la chuki za kisaikolojia zilizopo baina watembea kwa mguu/Bodaboda na wenye magari binafsi, swala hili linaonekana sasa kuwa changamoto kwakweli kama vipi mamlaka na police wafanye kampeni kuelimisha watu waache kujichukulia sheria mkononi,
HISTORIA YA MATUKIO
Kwa mda sasa imekuwa kama kasumba, nimeshuhudia ajali kadhaa kwa magari ya watu binafsi inapotokea labda kwa bahati mbaya wanagongana na Bodaboda ama mtembea kwa miguu-Mara nyingi mwenye gari huonekana ana makosa au hata kupigwa na raia ama gari yake kuumizwa kwa fujo na kuharibiwa ama kuibiwa mali zake.mfano;
1. Historia inaonesha chanzo cha wa-machinga kuondolewa Kariakoo, ilikuwa ni tukio moja la mwenye gari ndogo binafsi alimgusa mtembea kwa miguu yaani kama kumpush,sasa kutokana na ule msongamano watu walimshambulia mwenye ile gari hadi wakamuua kabisa.
2. Kuna jamaa mmoja alikuwa mgeni njia moja halafu mvua ilikuwa imenyesha kukawa na madimbwi, sasa kwakuwa hakuijuwa njia ile vizuri ikabidi awaulize watembea kwa miguu wanaishi maeneo hayo, wakamwambia pita tu pafupi- mwenye gari alipopita akazama kulikuwa na bonge la shimo.
3. Kawaida gari na mtembea kwa miguu mnatakiwa kila mmoja ampishe mwenzake, tena ni vizuri mtembea kwa miguu ndiye haswa ampishe mwenye gari, lakini utashangaa inapotokea mtembea kwa miguu /boda kupushiwa…huwa wanakuja juu sana ama kununa na kumchungulia dreva wa gari sielewi lawama ni za nini.
4. Kuna ajali iliwahi kutokea maeneo ya Mbagala jamaa mwenye gari ndogo alichomekewa na Bodaboda jamaa akawa kamgonga, ila kwa usitaarabu alisimama ili kutaka muafaka, baada ya mda mfupi bodaboda kibao zilimshambulia jamaa kwa mawe kiasi kwamba hadi jamaa akachomoa bastola akamchapa mmoja, walipoona mmoja kafa –wengine wakatawanyika jamaa akachomoa mchuma mpaka kituoni kwenda kuripoti ( trafiki kesi na shambulizi)
5. Mwendesha bodaboda alijigonga/aliligonga kwa nyuma gari la taka akafa palepale, wenzake wakashambulia liel gari.
6. Magari madogo huvunjiwa sidemirror na waendesha bodaboda kwa chuki binafsi ambayo haijulikani.
7. Kuna jamaa yangu alipata ajali maeneo ya Ubungo, watu badala ya kumsaidia badala, wakamwambia ebu fungua boneti harakaharaka gari inaungua, jamaa kubinua tu, wakachomoa betri fasta, na kumwambiwa fungua buti la nyuma tuweke, ile kufungua wakachukua vitu kule kwenye buti na kuanza mbio, alipowafukuzia wengine wakachomoa radio n.k
Sasa naomba tuambizane hapa, hii tabia ya watu kujichukilia sheria mkononi kumshambulia mwenye gari ndogo pindi ajari inapotokea itokomezwe vipi? Maana sasa hivi imekuwa ni bora ukimbie na gari hadi police kujisalimisha kuepuka hawa raia wanapotokea mara nyingi wamekuwa wakishambulia mwenye gari kwasababu ambazo mi naona ni kama chuki binafsi iliyojengeka akilini mwa watu. (mimi natembea na bastora lakini bado naona si busara kuitumia cha msingingi ni maelewano na sheria ifatwe)
MIFANO HIYO INAONYESHA VILE MWENYE GARI ANACHUKIWA NA WATEMBEA KWA MIGUU
Je wadau jambo hili mnalitazamaje? Watu kushambulia magari yanapopata ajari na bodaboda ama kumgonga mtu? NINI KIFANYIKE? maana kama halitafanyiwa kazi ipo siku mwenye gari ataangamiza raia kwa bastola ili kujihami.