Trial balance
JF-Expert Member
- Jun 16, 2020
- 202
- 159
Jamani hii tabia inakera hasa kwenye daladala yani utakuta mtu anaongea kwenye simu kwa sifa, utasikia eh nyama vipi ipo? Vipi ile ela yule mtu alileta? eh mara nikaangie chipsi na nyama nizikute mezani, yaani ataongea kwa kujisifu sifu atakata atampigia mtu mwingine tena hallow natoka bank hapa ule mzigo nimeambiwa upo bado kuchukua tu, yaani utakuta mmepanda daladala ni makelele hadi mwisho wa safari, mimi hii tabia siipendi.
Utashangaa akiwa na watu ni tofauti na maongezi ya peke yake. Kuna siku nilikuwa natoka mkoani naenda Dar kuna kaka alibeba radio yake akawasha tangu mwanzo wa safari wakati huo gari limewasha screen miziki inapigwa kama kawaida na movie zinaendelea na yeye kaweka sauti ya kutosha tu unasikiliza radio yake unasikiliza radio ya gari.
Tulifika kituo flani ivi watu wakamchoka wakamwambia kaka weka earphone unakera wengine. Dah! kaka alikuwa mkali hakuzima radio akagoma kwasababu zilikuwa siti za nyuma tukamwita konda aje aongee naye, akamwambia kaka zima radio akagoma akidai nyimbo anazozipenda yeye zipo kwenye radio yake hafurahishwi na nyimbo za kwenye gari.
Akaendelea kudundisha nyimbo zake hadi mwisho wa safari, kwa kweli watu tulikuwa bored sana hasa Mimi huwa sipendi makelele hata TV kwenye gari siangaliagi nakaaga tu bora ingekuwa simu inakuwa na sauti nyembamba. Hebu imagine radio zile zenye spika alafu kaweka sauti kama yote sauti ilisambaa gari zima ila tuliekaanae karibu ndo tulikelekwa zaidi sauti mbili mbili masikioni bado sauti za story za watu dah makelele na Mimi hapana aisee!