Hivi kwanini watanzania wanapenda kushangaa shangaa?

Hivi kwanini watanzania wanapenda kushangaa shangaa?

aisee hiyo tabia huwa inanikera na huwa najiuliza hv watu wengine wakoje, unakuta mtu kashuka kwenye dalala ana safari zake lakini kakuta tukio halina mbele wala nyuma watu wanashangaa na yeye safari inaishia hapo hapo anashangaa, na mengine ni ya kijinga ambayo huniacha hoi mfano mimi asubhi nnapotoka kwangu sina wa kunifungulia geti basi nnapotoka inanibidi nifungue geti nitoe gari then nishuke kwenye gari nirudi kufunga geti na nnaporud nyumbani ni hivyo hivyo ila cha kushangaza unakuta mtu anasimama kabisa anashangaa nnavyofungua lile geti natoa gari au naingiza gari na atashangaa mpaka gari inapopotelea, sasa najiulizaga cha ajabu ni nini au ni habit tu baadhi ya watu wamejijengea, mbona mimi siwezi kuwa hivyo

Huoni na ww umeshangaa anavyo kushangaa,
 
wanashangaa kama wewe unavyowashangaa wao....yan hapo mnashangaa wote tofauti ni mnachoshangaa....wao wanashangaa greda wewe unawashangaa wao
 
kuna suala huwa najiuliza,hivi tabia ya watanzania kushangaa shangaa hovyo tumeitoa wapi?
unakuta maybe greda linachimba tu mtaro huko mtaani but wazee,vijana na watoto wanakua wamelizingira Hilo greda.na hii tabia iko mijini na vijijini.
hivi tatizo huwa ni ukosefu wa kazi za kufanya au ni nin tatizo?
Duh juzi kati nilipita barabara moja mwz nikapishana na greda linatengeneza barabara ya mtaa kwa mbele nikakuta umati mkubwa wa watu nikasimama kuuliza kulikoni naambiwa greda limetoboa bomba la maji sasa nikauliza nyie ni mafundi bomba hapana tunaangalia tu maji yanavyomwagika,
 
Ututake radhi watz.....hatujawahi yaona kwann tusiyatolee macho!
 
kushangaa ni jambo la kawaida mbona tukiona misambwanda huwa tunashangaa
 
Wengi tunazurura bila kwenda mda au timetable tuna mda wakutosha wakushangaa sana
 
kuna suala huwa najiuliza,hivi tabia ya watanzania kushangaa shangaa hovyo tumeitoa wapi?
unakuta maybe greda linachimba tu mtaro huko mtaani but wazee,vijana na watoto wanakua wamelizingira Hilo greda.na hii tabia iko mijini na vijijini.
hivi tatizo huwa ni ukosefu wa kazi za kufanya au ni nin tatizo?
Hawana la kufanya zaidi ya kushangaa!!
 
kuna suala huwa najiuliza,hivi tabia ya watanzania kushangaa shangaa hovyo tumeitoa wapi?
unakuta maybe greda linachimba tu mtaro huko mtaani but wazee,vijana na watoto wanakua wamelizingira Hilo greda.na hii tabia iko mijini na vijijini.
hivi tatizo huwa ni ukosefu wa kazi za kufanya au ni nin tatizo?
Hiyo inaitwa Polisi jamii. Umbea unaweka Tanzania salama.
 
kuna suala huwa najiuliza,hivi tabia ya watanzania kushangaa shangaa hovyo tumeitoa wapi?
unakuta maybe greda linachimba tu mtaro huko mtaani but wazee,vijana na watoto wanakua wamelizingira Hilo greda.na hii tabia iko mijini na vijijini.
hivi tatizo huwa ni ukosefu wa kazi za kufanya au ni nin tatizo?
Kwanza wanaoshangaa wana muda wa ziada kukosa cha kufanya. Pamoja na hayo pia wanapenda kujua hicho wanachokishangaa kinafanyaje hicho kinachofanya. Hivyo, kati ya washangaaji wapo wanaoambulia uelewa zaidi.
 
Hahahah inafurahisha sana hii, tena kama unapita eneo flani ukaona umati wa watu wanashangaa kitu wala usijisumbue kwenda kumuuliza mtu yeyote hapo, wengi wao watakwambia "hata mimi mwenyewe sijui nini kinaendelea hapa"

Hua najiuliza kama hajui kitu nini kimempeleka pale?
 
Back
Top Bottom