Hivi kwanini Wakenya hawatupendi Watanzania?

Hivi kwanini Wakenya hawatupendi Watanzania?

kende

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2013
Posts
3,527
Reaction score
1,671
Nimeshuhudia mara nyingi battle ya maneno kati ya watanzania na wakenya kwenye mitandao ya kijamii, na battle hizo mara nyingi wakenya ndo wanaanzisha kutokana na majisifu yao yasiyovumilika na kujiona superior sana kuliko watanzania.

Ni ngumu kuona battle ya mtanzania na Mganda / Rwanda / Burundi kwenye social networks but ni kawaida kuona battle ya mtanzania vs mkenya.

Mfano jana kwenye page ya facebook ya msanii wetu Diamond Platnumz aliandika post aliyoiandika kwa lugha mbili; kiingereza na kiswahili. Kama unavyojua kiingereza si lugha yetu, kiingereza chake kikawa na errors kidogo, wakenya wakaanza vimaneno vyao vya kejeli basi kukawa na vita kubwa ya matusi kati ya wakenya na wabongo.

Nini hasa kinasababisha chuki hizi?
 
tukipunguza rushwa kdg,tukiongeza bidhaa tunazo"export" nje ,tukibalance idadi ya wasomi na wataalam wetu ,tukipunguza idadi ya misaada kutoka nje,na pia tukiongeza idadi ya sehem za kutoza kodi km kodi za apartments,uraia,viwanja,na baadhi ya luxury goods kutoka nje........na uongozi ukabadilika........SOON WAKENYA WATAISOMA NAMBA.....VERY SOON
 
Kwani ni Lini Walitulazimisha Tuwapende? Swali Lako Ni Sawa Na Kuuliza Kwanini Watanzania Hawawapendi Wanyarwanda? Akhsante.
 
Wanatuchukia sababu wanajua tuna uwezo mkubwa kuliko wao sema tumelala, na wanajua kabisa siku Tanzania ikiamka hawataweza kutuchukia kwani misaada na mikopo ya fedha watakuwa wakituomba sisi
 
tukipunguza rushwa kdg,tukiongeza bidhaa tunazo"export" nje ,tukibalance idadi ya wasomi na wataalam wetu ,tukipunguza idadi ya misaada kutoka nje,na pia tukiongeza idadi ya sehem za kutoza kodi km kodi za apartments,uraia,viwanja,na baadhi ya luxury goods kutoka nje........na uongozi ukabadilika........SOON WAKENYA WATAISOMA NAMBA.....VERY SOON

Natamani sana ungepewa hata kawizara
 
You only something that threatens you. Watanzania hatubuluzwi kama ambavyo Nchi zingine Za Afrika Mashariki zinavyo buruzwa na Kenya na wakenya Wanajua hilo
Cc: MK254
 
Last edited by a moderator:
Sijapoteza muda kusoma ulichoandika.

We TANZANIANS are the most CHERISHED in ths regio. They always seek for us when in need.
 
Hawa jamaa wameishi ki sifasifa na kujiona wao ndokilakitu, hawashindwi kujipa vitu ambavyo sivyao ilimladi wapate sifa na kujipa umwamba, Wakenya wanakwambia Mt.Kilimanjaro upo kenya, Kiswahili chapatikana kenya, East africa ni kenya, usishangae ikatokea hata gesi ya mtwara huko nje wanatangaza ipo Kenya, kwahio jamaa hawa pia wanatambua Tanzania ndio nchi ambayo inauwezo wa kuisumbua kenya kwa lolote paletu tutajitambua hivyo wanafitina sana nasie.
 
Wakenya wengi ni selfish wakabila hatari sio kwamba tu hawatukubali Watanzania hata wao wenyewe kwa wenyewe.

Mtanzania yeyote asikubali kunyanyaswa na mkenya. Hawana kitu chochote na ni waoga mno, lakini kama utaonesha kuwaogopa watakunyanyasa sana. Kujiona kwao wameendelea ni ujinga wao wa zamani hayo maendeleo hayapo tena na sasa Tanzania tumewazidi katika mambo mengi sana na tena wana hotu kubwa kuhusu hilo.

Mtanzania jiamini kila mahali kwani hakuna taifa zuri na lenye neema na watu wema kama Tanzania.

Tuulize sisi tunaoifahamu dunia yote, huo ndio ukweli!
 
Nimeshuhudia maranyingi battle ya maneno kati ya watanzania na wakenya kwenye mitandao ya kijamii, na battle hizo maranyingi wakenya ndo wanaanzisha kutokana na majisifu yao yasiyovumilika na kujiona superior sana kuliko watanzania, ni ngumu kuona battle ya mtanzania na mganda/rwanda/burundi kwenye social networks but ni kawaida kuona battle ya mtanzania vs mkenya, mfano jana kwenye page ya facebook ya msanii wetu Diamond Platnumz aliandika post aliyoiandika kwa lugha mbili kiingereza na kiswahili, kama unavyojua kiingereza si lugha yetu kiingereza chake kikawa na errors kidogo, wakenya wakaanza vimaneno vyao vya kejeli basi kukawa na vita kubwa ya matusi kati ya wakenya na wabongo. Nini hasa kinasababisha chuki hizi?

11072537_1036594563035763_5241949039730488886_n.jpg


Ag. CS for Transport James Macharia, Uganda Minister for Works & Roads, and Chair of the Joint Committee Mr. John Byabagambi and KR MD Mr. A. K. Maina and other committee members during a familiarization tour of the SGR project at Mtito Andei. on Friday, May 1, 2015.
11008573_975829622449754_4849382645690333510_n.jpg


10922767_977705588928824_6489992242201783296_n.jpg
 
Wakenya wengi maisha yao ni magumu, wanajifariji na kiingereza uchwara ambacho kimejaa errors nyingi kwasababu ya lafudhi ya makabila yao. Wanaona wanauchumi mzuri wakati ukweli ni kwamba uchumi wao umemilikiwa na wageni wengi, wazungu na wahindi, waafrika ni wa chache na tena ni wanasiasa. Majority wapo hovyo hawana hata ardhi ya kuishi. Kwahiyo mi nawadharau Wakenya na ni sawa na mtu anajivunia utajiri wa mjomba wakati yeye hana kitu. Nimeshangaa juzi imetolewa list ya vyuo vikuu bora 50,nikakuta hakuna hata chuo chao kimoja kimo humo. Wakati UDSM ipo kumi bora. Ni wa kuwapuuza tu
 
I think cha kwanza ni kwasababu tunasikilizana kwa lugha moja kiswahili kulko uganda rwanda au burundi sio wengi wanaojua kiswahili vzr Ndo mana battle hua kubwa, cha pili Kenya wana ogopa Tz jinsi ilivyokuja kwa kasi mno kama kwenye music tumetake over na inatutambulisha vzr kote africa wao wanabaki kuhate tu na industry yao ya music inafall down.
Mtu uliyemkuta alaf unamtake over y asikuhate.
 
Back
Top Bottom