Hivi kwanini wabongo choo tunakichukulia poa?

Hivi kwanini wabongo choo tunakichukulia poa?

Choo ni maji mkuu. Tatizo uswahilini maji nayo ya shida.

Mtu anaenda chooni amebeba maji lita moja kwenye kikopo. Hapo hata kutawaza tu hayatoshi sembuse aoshe na choo baada ya kumaliza haja?

Ndio maana mimi sitakagi choo cha ku share. Nikikosa chumba self basi hata kama choo kipo nje kiwe changu mwenyewe.
Solution ni nn mkuu? Inaweza kuwa fursa km tutaangalia hili tatizo kwa jicho la fursa
 
Mojawapo ya vitu ambavyo waweza jua personality ya mtu ni kuangalia vitu ambavyo vimejificha kama choo
Kwa kifupi Choo kina umuhimu sawa na Jiko
Huwezi ona umuhimu wa Choo ukiwa na njaa, Lakini huwezi ona umuhimu wa jiko ukiwa na kipindupindu
 
Nilienda nyumba moja ambayo huwezi dhania, nilibanwa nikaingia chooni nikakuta choo ni kichafu mpaka wale funza wamepanda juu aisee mavi yalirud ndani muda huo huo.

Ndio maana huwa sinyi nje ya nyumbani kwangu labda niwe nimesafiri.
 
then sijui kwa nn vyoo vingi hujengwa vidunchuuu halafu havina bati
 
Yote tisa, kumi ni kwamba hapahapa Tz kuna jamii hata hicho choo kichafu hawana, na hawana hata mpango, maadam wapo karibu na vichaka ama sehemu za wazi, si baba,mama wala mtoto anaejali, kweli Tz nikubwa sana.
 
Choo ni maji mkuu. Tatizo uswahilini maji nayo ya shida.

Mtu anaenda chooni amebeba maji lita moja kwenye kikopo. Hapo hata kutawaza tu hayatoshi sembuse aoshe na choo baada ya kumaliza haja?

Ndio maana mimi sitakagi choo cha ku share. Nikikosa chumba self basi hata kama choo kipo nje kiwe changu mwenyewe.
hii karibu kila nyumba ya kupanga uwazi inawahusu
 
kwani mababu zetu walivyokuwa wakijenga mabanda yao zamani walikuwa wana jumuishaga na vyoo??
 
Yani inahitajika awereness kubwa hususu wananchi kijijengea vyoo vyenye kifaa Kwa matumizi ya kibinadamu,
Mabwana/mabibi afya watumike kusimamia hili swala jamani!
Yani vyoo ni mtihani si mjini si vijijini!
 
Unakuta chooni hakuna Maji wala toilet papers sasa Mtu akisha jisaidie afanyeje?
 
Am done vice versa. Naweza piga msosi msalan kabisaaaa. Chooo kina starehe yake jaman tukipe kipaumbele katika maboresho ya makazi yetu.
 
Kuna kipindi nilienda uganda nikakutana na tatizo hili hili ...inaonekana ni tatizo letu waafrica kwa ujumla km uliskia juzi kati harare kulilipuka kipindupindu na watu kadhaa walifariki
Ni shida tupu
 
Yote tisa, kumi ni kwamba hapahapa Tz kuna jamii hata hicho choo kichafu hawana, na hawana hata mpango, maadam wapo karibu na vichaka ama sehemu za wazi, si baba,mama wala mtoto anaejali, kweli Tz nikubwa sana.
Aisee
 
kwani mababu zetu walivyokuwa wakijenga mabanda yao zamani walikuwa wana jumuishaga na vyoo??
Hatuongelei mambo ya zamani tunaongelea mambo ya karne ya 21
 
Yani inahitajika awereness kubwa hususu wananchi kijijengea vyoo vyenye kifaa Kwa matumizi ya kibinadamu,
Mabwana/mabibi afya watumike kusimamia hili swala jamani!
Yani vyoo ni mtihani si mjini si vijijini!
Mabwana afya na mabibi afya wanakula mshahara wa bure ...hakuna wanachofanya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom