Hivi kwanini wabongo choo tunakichukulia poa?

Hivi kwanini wabongo choo tunakichukulia poa?

mbwewe

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2014
Posts
3,267
Reaction score
3,415
Hii ni kwa mujibu wa utafiti wangu binafsi . Utakuta mtu nyumbani kwake kuna sofa za maana, chini kuna zulia la hadhi ya ikulu. Tv nchi 42 ikipewa sapoti na vinga'amuzi kama vitatu tofauti!!! lakini achana na hivyo vyote omba uonyeshwe choo kilipo , unakuta choo ni kichafu mpaka kimeota ukungu mweusi, kinatoa harufu kali yaani hata kama umebanwa haja utajihisi haja kupotea.

Sasa mi huwa najiuliza! Kwanini wabongo huwa hatujali kbsa linapokuja suala la choo lakini tupo tayari kutumia hta millioni 2 kwa ajili ya vitu luxury km tv???
 
Utamaduni wetu sio choo km kipaumbele,nafkiri ndio mda muafaka wa kubadirisha fikra.
 
Utamaduni wetu sio choo km kipaumbele,nafkiri ndio mda muafaka wa kubadirisha fikra.
Kumbe ishu ni utamaduni...km ni hivyo inabidi tubadikishe mtazamo, maana magonjwa mengi yanaanzia chooni
 
utafiti wako haukuzingatia vitu muhimu.
Jua kabisa kwa nyumba nyingi za zamani, sebule na sehemu nyingine ni rahisi kufanyiwa marekebisho au upambaji ili kubadili mandhari mfano kutoa makochi ya kizamani na kuweka sofa, kutoa tv ya kichogo na kuweka flat, na vitu vingine, ila choo mkuu ni kazi, kama ni cha shimo ili kiwe cha kuflash labda ujenge kipya na sewage system mpya, kama ni cha sink ha sakafu ya kawaida, siku ukisema uweke malumalu ile sink inabaki chini sakafu inakuwa juu juu na muonekano unakuwa mbaya zaidi
 
Mtazamo wetu waafrica inabidi ubadilike kuhusu choo...tunakichukulia poa sana bila kujua kuwa magonjwa mengi chanzo chake ni chooni
 
utafiti wako haukuzingatia vitu muhimu.
Jua kabisa kwa nyumba nyingi za zamani, sebule na sehemu nyingine ni rahisi kufanyiwa marekebisho au upambaji ili kubadili mandhari mfano kutoa makochi ya kizamani na kuweka sofa, kutoa tv ya kichogo na kuweka flat, na vitu vingine, ila choo mkuu ni kazi, kama ni cha shimo ili kiwe cha kuflash labda ujenge kipya na sewage system mpya, kama ni cha sink ha sakafu ya kawaida, siku ukisema uweke malumalu ile sink inabaki chini sakafu inakuwa juu juu na muonekano unakuwa mbaya zaidi
Hii excuse bado haijaniingia akilini ...unakuta the same family wanatumia hadi millioni mbili kununua tv, huku choo kikiwa kina hali mbaya kbsa
 
Hii ni kwa mujibu wa utafiti wangu binafsi . Utakuta mtu nyumbani kwake kuna sofa za maana, chini kuna zulia la hadhi ya ikulu. Tv nchi 42 ikipewa sapoti na vinga'amuzi km vitatu tofauti!!! lakini achana na ivo vyote omba uonyeshwe choo kilipo , unakuta choo ni kichafu mpaka kimeota ukungu mweusi.kinatoa harufu kali yaani hta km umebanwa haja utajihisi haja kupotea
Sasa mi huwa najiuliza! Kwanini wabongo huwa hatujali kbsa linapokuja suala la choo lakini tupo tayari kutumia hta millioni 2 kwa ajili ya vitu luxury km tv???
Choo kipi mkuu ni kile cha nyumbani au kile kinachobebwa na kina dada?
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Hii ni kwa mujibu wa utafiti wangu binafsi . Utakuta mtu nyumbani kwake kuna sofa za maana, chini kuna zulia la hadhi ya ikulu. Tv nchi 42 ikipewa sapoti na vinga'amuzi km vitatu tofauti!!! lakini achana na ivo vyote omba uonyeshwe choo kilipo , unakuta choo ni kichafu mpaka kimeota ukungu mweusi.kinatoa harufu kali yaani hta km umebanwa haja utajihisi haja kupotea
Sasa mi huwa najiuliza! Kwanini wabongo huwa hatujali kbsa linapokuja suala la choo lakini tupo tayari kutumia hta millioni 2 kwa ajili ya vitu luxury km tv???
Ila Kweli. Uchafu pia unachangia kizidi kunuka.watu wengine Licha ya ubaya wa Choo lkn pia hawafanyi usafi
 
Kaka principle yangu hakuna atakeyukafanyia usafi vile wewe unataka. Mimi husafisha toilet mwenyewe, house yangu mwenyewe nafanya vile navypona inafaa. Hatuna dada sababu walishindwa fanya kazi ikaonekana. Mama anapika, Mimi napika, usafi wa nyumba tunafanya wote tuna Watoto watatu, huyu wa kwanza ndo anaweza fanya kazi lkn weekends only Sababu alikuwa std 7. Tunashirikiana mpaka hatuoni Sababu ya dada. Mie mfanyakazi mwenzangu mfanyabiashara. Mimi nawahi kuondoka, yeye anafanya chaos za jikoni, jioni nikirudi na mop langu nikisaidia na mwanangu wa std 7 tunasafisha house mama akarudi anakuja. Choo kwangu hawezi kuta kichafu ni mipango tuu
 
Choo ni maji mkuu. Tatizo uswahilini maji nayo ya shida.

Mtu anaenda chooni amebeba maji lita moja kwenye kikopo. Hapo hata kutawaza tu hayatoshi sembuse aoshe na choo baada ya kumaliza haja?

Ndio maana mimi sitakagi choo cha ku share. Nikikosa chumba self basi hata kama choo kipo nje kiwe changu mwenyewe.
 
Watu wanategeana. Kuna sehemu nlienda nyumba Hizi za kupanga.. Unaweza Rudi na mzigo wako nyumban, watz Mungu anatuona
Kuna kipindi nilienda uganda nikakutana na tatizo hili hili ...inaonekana ni tatizo letu waafrica kwa ujumla km uliskia juzi kati harare kulilipuka kipindupindu na watu kadhaa walifariki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom