Hivi kwanini serikali haikithamini chuo cha Ardhi licha ya kutoa wahitimu muhimu?

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
19,454
25,371
Wakuu nimekuwa nikiuliza nakosa jibu.Haiwezekani kila kukicha serikali ing'ang'anie kukiboresha chuo cha UDSM kama vile kukijengea mabweni ya kisasa ma lectures wa kutosha lakini wakati huo huo majirani zao wa Ardhi wana mabweni yaliyochoka sana.

Kwa kifupi mabweni ya chuo kikuu cha Ardhi yanaweza kubeba wanafunzi wasiozidi mia 5 na wanaopewa nafasi ya kukaa chuoni ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza pekee na sio wote wanaopata nafasi bali ni baadhi yao.

Sasa najiuliza kwa nini hizo pesa bilioni 10 wasingewapa hata bilion 2 chuo cha Ardhi nacho kiboreshe mabweni yao kwa sababu mabweni ya chuo cha Ardhi ni hayana hadhi ya kukaliwa na mwanachuo kikuu ,maji ni shida, vyoo vibovu, vyumba vibaya nk

Ifike mahala serikali wawe wana fanya equally distribution of resources sio kama wanavyofanya hivi sasa, na hiyo ndio itakuwa demokrasia ya kweli kuliko wanavyofanya hivi sasa.

Wataalamu wengi wa masuala ya Ardhi, na mazingira kwa ujumla wanategemewa kutoka pale sasa kama hamuwawezeshi au kuwapa motisha mmategemea watafanya vizuri kweli kwenye masomo yao???

Serikali badilikeni acheni kufanya kazi kwa upendeleo.
 
Ni aibu kwa Chuo kikuu kulalamika eti hawana pesa na wakati wana Maprofesa nguli (PhDs) wanaoehishimika duniani. Ardhi university kajifunzeni Pale UDBS (university of dar es Salaam) kuna Prof. RUTASHOBYA ndie aliyeandika mradi wa majengo "pacha" ambapo ndipo zilipo benki za CRDB na NMB na baadhi ya ofisi kuu za chuo/UDBS. Zipo tetesi hao UDBS wanataka kujitenga kutoka UDSM. Sasa nyie wapima ardhi mnalia lia tu hapo acheni upuuuzzi.
*mnapata pesa toka serikalini mnaenda kununua V8 za mabosi, timamu kweli?
** iweje chuo kama SAUT, Tumaini waweze kujiendesha na hawapewi pesa toka serikalini?
*** Acheni mawazo mgando na wivu usio na tija.
 
Ni aibu kwa Chuo kikuu kulalamika eti hawana pesa na wakati wana Maprofesa nguli wanaoehishimika duniani. Ardhi university kajifunzeni Pale UDBS (university of dar es Salaam) kuna Prof. RUTASHOBYA ndie aliyeandika mradi wa majengo "pacha" ambapo ndipo zilipo benki za CRDB na NMB na ofisi kadhaa za chuo/UDBS. Zipo tetesi hao UDBS wanataka kujitenga kutoka UDSM. Sasa nyie wapima ardhi mnalia lia tu hapo acheni upuuuzzi.
Una akili timamu?

Mbona UDSM kinapewa pesa na serikali?

Basi kama ndio hivyo wasingegawa kote ili ijulikane moja kuliko kila kukicha kukipendelea chuo kimoja

Basi wafute vyuo vyote tujue moja.
 
kwanza ardhi kutenganishwa na udsm ni kupeana ulaji tu... ardhi ilipaswa iwe department tu ya udsm...

mkuu wa chuo ardhi anakula mshahara wa bure tu.

fika makerere au university za usa uone campus inavyokuwa kijijiii...

hizo uni za mbele mbele kama university of california ukisikia ni kama kijijiiiiiii ...

ingia hata youtube one mavyuo yalivyo makubwaaaa usa.... huku eti ardhi nacho chuo jiran na udsm ila kimegawanywaaa
 
Sio Ardhi tu hata muhimbili nacho kilikuwa chuo cha UDSM
 
Una akili timamu?

Mbona UDSM kinapewa pesa na serikali?

Basi kama ndio hivyo wasingegawa kote ili ijulikane moja kuliko kila kukicha kukipendelea chuo kimoja

Basi wafute vyuo vyote tujue moja.
wachaa akili mgando we jamaa ...wafute ili iweje sasa...??
 
kwanza ardhi kutenganishwa na udsm ni kupeana ulaji tu... ardhi ilipaswa iwe department tu ya udsm...

mkuu wa chuo ardhi anakula mshahara wa bure tu.

fika makerere au university za usa uone campus inavyokuwa kijijiii...

hizo uni za mbele mbele kama university of california ukisikia ni kama kijijiiiiiii ...

ingia hata youtube one mavyuo yalivyo makubwaaaa usa.... huku eti ardhi nacho chuo jiran na udsm ila kimegawanywaaa
Mimi mpaka leo sielewi reasoning ya kuvitenganisha...
Cheki kama University of London, chuo kina colleges 18, na most of those colleges zina wanafunzi 10,000+ each, lakini mpaka leo hawana mpango wakuvitenganisha
 
wachaa akili mgando we jamaa ...wafute ili iweje sasa...??
Wafute ndio ,kwa sababu wanakithamini chuo kimoja tu

Embu jaribu kufikiria chuo cha Ardhi mabweni yao hayana uwezo wa kubeba wanafunzi wanaozidi mia tano lakini serikali wamekaa kimya tu lakini UDSM tatizo la mabweni sio kubwa lakini wameongezewa mengine wewe unaona hii ni haki kweli?

Chuo cha ardhi hata maji tu nayo ni shida ,majengo yamechakaa ile mbaya,Computer lab ,Computer zipo chache

Yani kwa kifupi Aru kuna matatizo mengi saana .
 
Wakuu nimekuwa nikiuliza nakosa jibu.Haiwezekani kila kukicha serikali ing'ang'anie kukiboresha chuo cha UDSM kama vile kukijengea mabweni ya kisasa ma lectures wa kutosha lakini wakati huo huo majirani zao wa Ardhi wana mabweni yaliyochoka sana.

Kwa kifupi mabweni ya chuo kikuu cha Ardhi yanaweza kubeba wanafunzi wasiozidi mia 5 na wanaopewa nafasi ya kukaa chuoni ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza pekee na sio wote wanaopata nafasi bali ni baadhi yao.

Sasa najiuliza kwa nini hizo pesa bilioni 10 wasingewapa hata bilion 2 chuo cha Ardhi nacho kiboreshe mabweni yao kwa sababu mabweni ya chuo cha Ardhi ni hayana hadhi ya kukaliwa na mwanachuo kikuu ,maji ni shida, vyoo vibovu, vyumba vibaya nk

Ifike mahala serikali wawe wana fanya equally distribution of resources sio kama wanavyofanya hivi sasa, na hiyo ndio itakuwa demokrasia ya kweli kuliko wanavyofanya hivi sasa.

Wataalamu wengi wa masuala ya Ardhi, na mazingira kwa ujumla wanategemewa kutoka pale sasa kama hamuwawezeshi au kuwapa motisha mmategemea watafanya vizuri kweli kwenye masomo yao???

Serikali badilikeni acheni kufanya kazi kwa upendeleo.
Allocation ya rasilimali bado ni tatizo hapa Bongo. Sasa sijui kulikuwa na ulazima gani kujenga mabweni kibao UDOM yenye kila kitu ila wanaishi ndege na jongoo tu na sasa mabweni mengine ni "wizara", halafu hali ya miundombinu ni tete kwenye vyuo vikongwe vinavyodahili wanafunzi wengi na ambavyo ni vituo muhimu kabisa vya utafiti mf. SUA, UDSM,Ardhi...
 
Allocation ya rasilimali bado ni tatizo hapa Bongo. Sasa sijui kulikuwa na ulazima gani kujenga mabweni kibao UDOM yenye kila kitu ila wanaishi ndege na jongoo tu na sasa mabweni mengine ni "wizara", halafu hali ya miundombinu ni tete kwenye vyuo vikongwe vinavyodahili wanafunzi wengi na ambavyo ni vituo muhimu kabisa vya utafiti mf. SUA, UDSM.
Wanafanya kazi kwa kujiskia sio kwa kuangalia mahitaji sehemu husika.

Chuo kikuu cha Ardhi hata viwanja vya michezo tu ni shida

Shule niliyosoma O lev na A lev ina hadhi mara 10 ya chuo cha Ardhi
 
Una akili timamu?

Mbona UDSM kinapewa pesa na serikali?

Basi kama ndio hivyo wasingegawa kote ili ijulikane moja kuliko kila kukicha kukipendelea chuo kimoja

Basi wafute vyuo vyote tujue moja.
Ardhi university tengenezeni Brand yenu kupitia graduates "alumni" & tafiti zenu. Acheni wivu vyuo vingine vikifanikiwa kwa taarifa tu UDSM wakijipanga vizuri zaidi watapabadilisha hapo mlimani. Ni suala la muda tu ninyi ardhi Endeleeni kulumbana tu.
 
mlitetenga wenyewe toka udsm kelele za nini,yaani ni aibu chuo cha ardhi kulilia majengo wakati hapo mna wataalam wa civil engineering,quantity surveyors,architec, watumieni hao
 
Sorry chuo gani ?? Kipo wapi hiki na wahitimu wake kama akina nani ??
 
mlitetenga wenyewe toka udsm kelele za nini,yaani ni aibu chuo cha ardhi kulilia majengo wakati hapo mna wataalam wa civil engineering,quantity surveyors,architec, watumieni hao
Ninacholalamika ni kitendo cha serikali kuwapendelea wao kila kukicha kinawapa pesa.

Ingekuwa vizuri zaidi kila chuo kiachwe kijiendeshe chenyewe lakini sio kuacha vyuo vingine kutowapa msaada wowote halafu kila kukicha wanapeleka mabilioni ya pesa Udsm wewe una ona ni haki hapo?kuna demokrasia ya kweli hapo?
 
Ulilosema mtoa hoja ni la msingi sana ARU pana tatizo kubwa la miundombinu pamoja na kuwa moja ya vyuo vikongwe nchini na ndipo wataalamu wakubwa wa Ardhi na usanifu majengo wanapotokea. Na mimi nimekuwa nikijiuliza swali hilihili kwani Chuo hakikui? mbaya zaidi VC wote wantokea pale UDSM unashindwa kuelewa kama ni sabotage au ninini? Inaumiza sana kuona hakuna miundombinu ya maana katika Chuo kile yaaani pana vijumba vya Miaka ya 50 huko kilipokuwa kinatoa Diploma hadi leo ni aibu kubwa sn. Nadhani hata uongozi wa chuo inabidi ujiulize kama wanastahili kuendelea kubaki katika nafasi wanazoshikilia
 
Wakuu nimekuwa nikiuliza nakosa jibu.Haiwezekani kila kukicha serikali ing'ang'anie kukiboresha chuo cha UDSM kama vile kukijengea mabweni ya kisasa ma lectures wa kutosha lakini wakati huo huo majirani zao wa Ardhi wana mabweni yaliyochoka sana.

Chuo chenyewe hakina madem hostel za nini?
 
Mimi mpaka leo sielewi reasoning ya kuvitenganisha...
Cheki kama University of London, chuo kina colleges 18, na most of those colleges zina wanafunzi 10,000+ each, lakini mpaka leo hawana mpango wakuvitenganisha
Kwa kweli kutenganisha UDSM na ARDHI walikurupuka haikuwa na mantik yoyote!
 
Back
Top Bottom