Hivi kwanini police wanapokukamata ukiwa hauna sticker ya nenda kwa usalama wanakimbilia faini?

Kimweli

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
899
231
Nilitegemea kupewa elimu kwanza kabla ya kuniandikia faini, sasa haya maisha sasa ni ugomvi sticker inauzwa sh. 3000, nishindwe kulipa hafi nije kulipa elfu 30,000 fain.

Ni nini umhimu wa hiyo sticker? Hii ni sawa na ile elfu 30,000 tunalipa kwa ajiri ya fire extinguisher ambayo ilivyokusudiwa si vile inavyofanyika. Police kwa hiki kiwango tulichofikia sasa siyo hii nchi ni yetu sote toeni elimu si kuonea kwa kiasi hicho sijawahi kuona nchi yeyote niliyowahi kufika inayotenda kama mnavyotenda kwa sasa toeni elimu na si kuforce fine. Likewise unamkamata mtu anaspeed ya 55/50km/h unamkomalia kama vile haujui mechanism ya gari kweli is this the meaning of the reality?

Uvumilivu una mwisho
 
mie mwenyewe nilishangaa na ile si kwa wiki 1 lakini naona wao mwezi wa 2 wanayo ile sticker, juzi ilibidi nikubali tu kwani nilikuwa nawahi ndege kwenda mwanza wakanidaka maeneo ya mnazi 1, nikashangaa siku zishaisha lakini nilipojaribu kuwauliza wakadai usitufundishe kazi, yani majibu yao ya kibashite bashite tu, nikakubali fine ya elf 30 manake ningeendelea ningeachwa, nikampa dogo akawalipe oysterbay
 
Kwani kabla ya kupewa huyo stika si chombo huwa kinakaguliwa kwanza kama kipo Ok! sasa kama wewe huna stika maana ake gari lako halijakaguliwa.

Ni bora tu mkalipa huyo faini maana hii ngoma ni endelevu na askari wetu hawa wa kibashite basi kazi ipo.
 
wamenilamba elfu 30,000 mara mbili mwezi huu, Jana nimeenda traffic central pale hakuna sticker ,ila askari mmoja kaniuzia 10,000 mtaani nitaibandika leo.
yaani hawa wameshatufanya sisi Mang'ombe wanatukamuaa tu .ila ipo siku
 
Dah...Acheni udaku bana...Pelekeni magari yenu yakakaguliwe kwa buku 3 ...Hatutaki ajali
 
Kwani kabla ya kupewa huyo stika si chombo huwa kinakaguliwa kwanza kama kipo Ok! sasa kama wewe huna stika maana ake gari lako halijakaguliwa.

Ni bora tu mkalipa huyo faini maana hii ngoma ni endelevu na askari wetu hawa wa kibashite basi kazi ipo.
Gari kukaguliwa? Wanakusimamisha,unaambiwa hili ni wiki la nenda kwa usalama,lipia stika,ole wako utoe 5,000 chenji haupati.
 
Naona wanafidia gap LA makusanyo haba ya kodi,ishakuwa ni mradi hakuna maelezo wala kuelemishwa ni mwendo wa 30, sidhani km kuna gari iliyobarabarani kila siku ipite mwezi lzm iandikiwe,sisi magari ya biashara ndo tushageuzwa ngombe hata ujitahidi vipi uwezi maliza wiki.Ila km zinaenda kwenye miradi ya maendeleo inayoonekana itatupoza machungu.
 
Kwani kabla ya kupewa huyo stika si chombo huwa kinakaguliwa kwanza kama kipo Ok! sasa kama wewe huna stika maana ake gari lako halijakaguliwa.

Ni bora tu mkalipa huyo faini maana hii ngoma ni endelevu na askari wetu hawa wa kibashite basi kazi ipo.
Heri yenu mnaokaguliwa, sisi malipo hufanyika pasi na kukaguliwa na ni sh 5,000
 
Back
Top Bottom