Hivi kwanini mpenzi wangu hanipendi?

Hivi kwanini mpenzi wangu hanipendi?

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
23,917
Reaction score
31,705
Wandugu nimekuja hapa mnipe ushauri kidogo

Nilikuwaga na demu wangu she is so cute kwa kweli ila tatizo lake alikuwa ananipiga mizinga sana

Huyu demu nilikutana nae kipindi fulani alikuwa boy wake sema huyo boy wake alikuwa bahili sana yani hata vocha alikuwa hamtumii ,demu alimpenda mshikaji sema mshikaji alikuwa hana time nae kabisa

Baadaye demu akaamua aachie ngazi, mwanzoni tulikuwa washkaji sana na huyo demu sema baada ya kuachana na mtu wake akaamua anitamkie ananipenda mimi na angependa niwe mpenzi wake ,mm nikaona poa tu pia sikushangaa kunitongoza kwa kuwa mimi nina mwili uliojengeka kimazoezi pia nina sura yenye kuzuzua mademu so suala la kunitongoza sikuona la ajabu sana


Sema tatizo lilikuja kuanza pale nillipogundua huyu demu ni mtu wa mizinga sana pia ni muongo muongo sana na mbaya zaidi uongo wake anawashirikisha rafiki zake ili iwe rahisi kunidanganya


Huyu demu ilikuwa nikitoka nae nijipange haswa ,chini ya laki 3 lazima niaibike kabisa kwa kuwa kila kizuri atachokiona lazima atake nimnunulie nisipo fanya hivyo anakasirika na haongei na mimi wiki nzima akipiga simu lazima atake pesa



Pia alikuwa na tabia ya kuwalingishia wenzake kuhusu mimi ,ilikuwa nikimnunulia kitu cha gharama lazima akawatambie wenzake


Sitasahau siku moja nimetoka nae kwenda MCity kwa gari la kwao mfukoni nilikuwa na laki 5 ,unaambiwa siku hiyo laki 5 yote iliishia hapo hapo mcity mbaya zaidi sikuwa na nauli ya kurudia home na akakataa kabisa kunipeleka home nilijuta sana kwa nini sikwenda na gari kwa kweli,sema kwa bahati nzuri bro wangu alikuwa kaenda tegeta nikampigia simu akirudi anipitie turudi wote nyumbani kwa kuwa sina nauli ,aisee alinicheka sana kwa kuwa kipindi natoka aliniona nazo pesa zote



Yote tisa kumi suala la yeye kuninyima penzi aisee linaniuma sana alikuwa ananionjesha mara chache chache sana tena sio bure bure mpaka nimpe hela


Baadaye nikawaza nikaona nimpigie simu nimwambie tuachane ila tubaki kuwa marafiki tu kama zamani cha ajabu alichonijibu kilinishangaza sana alinijibu ndio amekubali tuachane na akasema nifute namba yake kabisa na hataki kabisa hata urafiki na mimi

Mwanzoni nilijua anatania maana lugha aliyokuwa anatumia ilikuwa laini sana baadaye siku zilivyozidi kukatika ndo nikaamini alichokuwa anamaanisha


Yaani mpaka sasa sielewi kwa nini huyu msichana alikuwa hanipendi maana kwetu ni matajiri kama kwao na vitu vingi nilikuwa namnunulia kwa kifupi alinifanya kama baba yake ingawa mimi ni mwanafunzi wa chuo tena mwaka wa kwanza kama yeye


Sielewi kwa kweli yani ,naombeni ushauri wenu pia nataka madada wa humu waseme vitu gani wanampendea mwanaume maana sielewi kwa kweli yani
 
Cc HR 666 njoo ujipe ushauri uku
 
Nimesoma vizur ila nilipofikia hapa ckutaka kuendelea maana umenichefua
.

"""sikushangaa kunitongoza kwa kuwa mimi nina mwili uliojengeka kimazoezi pia nina sura yenye kuzuzua mademu"""
 
When you walk with the devil, price is always inevitable
 
Yan hapa tena umeongea pumba mkuu, nan kakwmbia mtu anakupendea utajiri....

"""Yaani mpaka sasa sielewi kwa nini huyu msichana alikuwa hanipendi maana kwetu ni matajiri"""
Haha! Akidhani ya kuwa watu hupendwa kwa kuwa ni matajiri!!!!
 
Mnatoa hela muda wa kupiga show mnalamba lips, silaha ya mwanamke ni kumkaza vizuri, atazurura kuchuna mafala jioni atakileta kwako.. Nadhani umenisoma
 
Back
Top Bottom