Hivi kwanini Maprofesa wengi ni wazee?

Hivi kwanini Maprofesa wengi ni wazee?

Bwana uber

Member
Joined
Jul 30, 2018
Posts
22
Reaction score
33
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada
Kwa utafiti mdogo ambao nimeufanya nimegundua maprofesa wengi ni wazee,vijana ni wachache mno.

Je, ni kwamba elimu ya wazee hawa ambao ndo wengi ni maprofesa ilikuwa rahisi kipindi hicho kuliko elimu ya sasa hivo ilikuwa rahisi kuupata uprofesa?

Au wazee hawa wana akili nyingi kuliko vijana ambao kwa sasa ni nadra sana kusikia kijana msomi ni profesa ,wengi wanaishia kuwa madaktari(PhD)tu?

Tatizo ni nini?
 
wakati us proffesor ni mwalimu tu, mfano Prof Ras Simba, kwetu ni msomi aliyepitia tabu saana hadi vipara kisa kubukua.
 
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada,,.
Kwautafiti mdogo ambao nimeufanya nimegundua maprofessor wengi ni wazee,vijana ni wachache mnoo.je

-nikwamba elimu ya wazee hawa ambao ndo wengi ni maprofessor ilikua rahisi kipindi hicho kuliko elimu ya sasa hivo ilikua rahisi kuupata uprofessor?
-au wazee hawa wana akili nyingi kuliko vijana ambao kwa sasa ni nadra sana kusikia kijana msomi ni professor ,wengi wanaishia kuwa madoctor tuu?

Tatizo ni nini?
elimu ya prof ni steji kubwa sana ambayo umemaliza steji zote za elimu au kuwa na jambo jipya ambalo watu wakakupa cheo kwenye kiwango cha elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikujua hili, nimejifunza kabla sijalala. Kwahiyo ukoshakua Tutorial Assistant huko US unaongeza neno Prof kabla ya jina lako. Au hata mwalimu wa mwandiko darasa la tatu?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada,,.
Kwautafiti mdogo ambao nimeufanya nimegundua maprofessor wengi ni wazee,vijana ni wachache mnoo.je

-nikwamba elimu ya wazee hawa ambao ndo wengi ni maprofessor ilikua rahisi kipindi hicho kuliko elimu ya sasa hivo ilikua rahisi kuupata uprofessor?
-au wazee hawa wana akili nyingi kuliko vijana ambao kwa sasa ni nadra sana kusikia kijana msomi ni professor ,wengi wanaishia kuwa madoctor tuu?

Tatizo ni nini?
It seems wewe huna ABC of academician life! Uprofessoe siyo kura za ndio au hapana! Wakishapiga kura ndiyo umekuwa Prof, NO!
 
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada,,.
Kwautafiti mdogo ambao nimeufanya nimegundua maprofessor wengi ni wazee,vijana ni wachache mnoo.je

-nikwamba elimu ya wazee hawa ambao ndo wengi ni maprofessor ilikua rahisi kipindi hicho kuliko elimu ya sasa hivo ilikua rahisi kuupata uprofessor?
-au wazee hawa wana akili nyingi kuliko vijana ambao kwa sasa ni nadra sana kusikia kijana msomi ni professor ,wengi wanaishia kuwa madoctor tuu?

Tatizo ni nini?
Mfano wewe ni kijana wa leo,una chochote cha kukuhamasisha toka kwa mapropesa km lipumba,kitila mkumbo,kabudi nk?
 
Uzee ni sifa mojawapo ya kuwa prof mkuu
 
Mwenye uelewa wa kutosha wa mtu ku-qualify kuwa prof atuwekee humu. Mchakato wa mtu awe prof ukoje kwetu hapa Bongoland

Sent using Jamii Forums mobile app
Uprofesa kwa Tanzania...

Mtu mwenye masters na akawa anafundisha chuo kikuu huitwa assistant lecturer. Akisoma degree ya uzamivu (PhD) na kuhitimu ataitwa Dr.x na hapo anakuwa lecturer. Kutokea hapo kadiri anavyochapisha (publish) research papers ambazo pia nyingine hutokana na Thesis zake za Masters na PhD hupata point kila anavyopublish. hizo points kadiri zinavyoongezeka humpandisha daraja kutoka lecturer...senior lecturer...associate professor hadi kufikia professor.

Kwa maisha ya sasa wapo maprofesa vijana pia hapa Tanzania kwa maana kati ya umri wa miaka 38-45.
 
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada,,.
Kwautafiti mdogo ambao nimeufanya nimegundua maprofessor wengi ni wazee,vijana ni wachache mnoo.je

-nikwamba elimu ya wazee hawa ambao ndo wengi ni maprofessor ilikua rahisi kipindi hicho kuliko elimu ya sasa hivo ilikua rahisi kuupata uprofessor?
-au wazee hawa wana akili nyingi kuliko vijana ambao kwa sasa ni nadra sana kusikia kijana msomi ni professor ,wengi wanaishia kuwa madoctor tuu?

Tatizo ni nini?
Kwa mfumo wa vyuo vyetu kwa sasa, ili uwe professor, lazima kwanza uwe na PhD. Kwa uchache na mtu aliyeunganisha, PhD inachukua miaka 8 ( mitatu digrii ya Kwanza, miwili digrii ya pili na mitatu tena PhD yenyewe.
Mtu mwenye PhD au mhadhiri akienda bila kikwazo huchukua miaka mitatu kuwa mhadhiri maandalizi. Mitatu mengine kuwa profesa mshiriki na mitatu mengine kuwa profesa kamili. Maana yake ni tisa. Kwenye uhalisia, wengi huchukua miaka minne au zaidi toka ngazi moja hadi nyingine.
Kwa hesabu hizo, unaweza kukadiria inachukua muda kuwa profesa na kwamba inatoa jibu kwa nini wengi umri umesogea.
 
elimu ya prof ni steji kubwa sana ambayo umemaliza steji zote za elimu au kuwa na jambo jipya ambalo watu wakakupa cheo kwenye kiwango cha elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuh, basi tunatofautiana uelewa, mimi nilidhani mtu yeyote mwenye PHD anaweza kuwa Prof, kwa kukamilisha idadi flani ya machapisho yake.
 
Basic ni hiyo PhD then mtu anapanda kwa machapisho kwa hatua.
Hata za chupi zipo kama kawaida.
 
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada
Kwa utafiti mdogo ambao nimeufanya nimegundua maprofesa wengi ni wazee,vijana ni wachache mno.

Je, ni kwamba elimu ya wazee hawa ambao ndo wengi ni maprofesa ilikuwa rahisi kipindi hicho kuliko elimu ya sasa hivo ilikuwa rahisi kuupata uprofesa?

Au wazee hawa wana akili nyingi kuliko vijana ambao kwa sasa ni nadra sana kusikia kijana msomi ni profesa ,wengi wanaishia kuwa madaktari(PhD)tu?

Tatizo ni nini?
ahahaaaa siku hizi kuna elimu au kuna shule?
 
Unaenda kuchukua form veta mkuu,unajaza unachagua unataka uwe profesa wa nini,basi baada ya wiki mbili unapihiwa simu umekua profesa au haujabahatika, hapo ni hela yako tu kuwahonga wale wanaotoa uprofesa
Mwenye uelewa wa kutosha wa mtu ku-qualify kuwa prof atuwekee humu. Mchakato wa mtu awe prof ukoje kwetu hapa Bongoland

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sababu hawapendi kustaafuu pindi muda wao unapofika na badala yake wanaomba kuongezewa muda kwa kisingizio kwamba wapo wachache. Hilo la uchache wanalitengeneza wenyewe kwa kuhakikisha kwamba vijana hawapandi vyeo na kuwakaribia. Sasa hivi nasikia wanajenga hoja mpya ya kuongezewa muda wa kustaafu!
 
Back
Top Bottom