Hivi kwanini binadamu tuko hivi.?

uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,700
1,415
Katika pitapita zangu club kuna usiku moja nikipata moja moto moja baridi kaunta akaja binti mmoja 'kaka naomba na mimi uninunulie moja' nikamnunulia na tukawa tunaongea,ana miaka 19 na ni yatima.Kamaliza form 4 mwaka jana hana wa kumuendeleza na rafiki yake akamshauri wajiuze.Nikasema hivi Uporoto si utakuwa umefanya jambo jema ukimsaidia huyu mtoto mmoja na kumbadili maisha kwa kumuendeleza na kumuepusha na uchangu ? Nikampa elfu 30 na kumwambia aende nyumbani kesho aje mjini,kesho yake tukakutana nikampeleka sehemu na kumwandikisha asome secretarial course na kumlipia na kumwambia kila wiki nitamtumia hela ya nauli na matumizi madogo kwa Mpesa.Ijumaa nimepita chuo na kuambiwa hajaonekana siku 10 na kwenye simu hapatikani.
 
pole sana uporoto......hukujua kama kunguru hafugikagi eeh
 
duuuhh Uporoto kumbe unarohoo nzuri hivyo..
Mungu atakuongezea kwa wema ulioonyesha...

mmmhhh unajua kama alisha anza ile kazi ni ngumu sana kuacha..
kwa hiyo weye ulifanya jema
lakini halikupokelewa..
nadhani yeye kashajichagulia maisha yake yawe hivyo..

lakini ni vizuri sana ulitenda wema...
 
si wote wanaojiuza hawana wa kuwaendeleza kielimu, wengine ni biashara zao
huyo hawezi kusoma tena, tatizo alilolifanya ni kutokukweleza ukweli wake.
 
pole sana uporoto......hukujua kama kunguru hafugikagi eeh
Niliona kwakuwa ni wiki yake ya kwanza pale labda ningeweza kumuokoa mapema.

duuuhh Uporoto kumbe unarohoo nzuri hivyo..
Mungu atakuongezea kwa wema ulioonyesha...

mmmhhh unajua kama alisha anza ile kazi ni ngumu sana kuacha..
kwa hiyo weye ulifanya jema
lakini halikupokelewa..
nadhani yeye kashajichagulia maisha yake yawe hivyo..

lakini ni vizuri sana ulitenda wema...
Inauma kwasababu kwa wiki mbili nilikuwa namtumia hela ya nauli/matumizi na ananiambia anaendelea na masomo.
 
si wote wanaojiuza hawana wa kuwaendeleza kielimu, wengine ni biashara zao
huyo hawezi kusoma tena, tatizo alilolifanya ni kutokukweleza ukweli wake.
Siku ile ya pili niliona cheti chake ni kweli alimaliza form 4 mwaka jana na aliniahidi kunipeleka kwa shangazi yake anaeishinaye nikipata nafasi nikaona inawezekana kumuwahi.
 
Inauma kwasababu kwa wiki mbili nilikuwa namtumia hela ya nauli/matumizi na ananiambia anaendelea na masomo.[/QUOTE]

Duuhhh pole sana mtu wangu..
Hizo pesa sahau tu dear...
lakini labda umemsaida kwa njia nyingine..
(kapata hela ya chakula , au kaenda kununua protection {condoms})
ulitenda wema ukaenda zako..
hayo mengine mwachie Mungu..

ka bado inauma sana njoo kipandee hii
nikutulize kidogo
hahahahah lol
 
Inauma kwasababu kwa wiki mbili nilikuwa namtumia hela ya nauli/matumizi na ananiambia anaendelea na masomo.

Duuhhh pole sana mtu wangu..
Hizo pesa sahau tu dear...
lakini labda umemsaida kwa njia nyingine..
(kapata hela ya chakula , au kaenda kununua protection {condoms})
ulitenda wema ukaenda zako..
hayo mengine mwachie Mungu..

ka bado inauma sana njoo kipandee hii
nikutulize kidogo
hahahahah lol[/QUOTE]
Nakuja sasa hivi,asante lol! Pale chuoni wameniambia wasipomwona mpaka wiki ijayo niende watanirudishia hela yangu alionekana siku moja tu.
 
Duuhhh pole sana mtu wangu..
Hizo pesa sahau tu dear...
lakini labda umemsaida kwa njia nyingine..
(kapata hela ya chakula , au kaenda kununua protection {condoms})
ulitenda wema ukaenda zako..
hayo mengine mwachie Mungu..

ka bado inauma sana njoo kipandee hii
nikutulize kidogo
hahahahah lol
Nakuja sasa hivi,asante lol! Pale chuoni wameniambia wasipomwona mpaka wiki ijayo niende watanirudishia hela yangu alionekana siku moja tu.[/QUOTE]

haya safi sana ,
vizuri kusikia utarudishiwa fweza zako dear..
haya weekend ijayo kaitundike yote
usahau machungu hahaha lol
 
Usianze kumlaumu mapema huwezi jua kakutwa na masahibu gani

Usifikiri Uporoto amemlaumu,hapana ameeleza ukweli ulivyo,mimi hapa nilipo hata nusu saa haijapita bado nilikuwa nimesimamishwa na wasichana wawili wakati natoka supermarket,wakaniomba niwanunulie sigara nikawaambia nitawapa pesa wakanunue wakaongeza,kama unataka group sex tuko tayari,nikashtuka maana nikiwatazama ni kama vile wako under 18,sasa kwa hali hiyo inamaanisha ni tabia za ajabu tu za binadamu zinazowafanya wafanye mambo hayo.Na wala hawana shida ya kusema inaweza kumsukuma kufanya mambo hayo.
 
umzima lakini?
 
Lol! Ndio techniques zao hizo.
Wengine wapo stand ya mkoa ubungo wanajifanya wametoka sitimbi hawawaoni wenyeji wao.
Hongera uporoto kwa moyo maridadi.
 
Tenda wema uende zako!Hongera Uporoto kwa kua na moyo wa ukarimu na huruma hivyo!!OFF TOPIC:Itabidi nikupaishe aisee..kwa hili unastahili!So we niambie lini tu ntatimiza!
 
Usianze kumlaumu mapema huwezi jua kakutwa na masahibu gani

Masahibu yapi mtu anakuambia anaendelea na masomo af unaenda unakuta hayupo. Sema tu kashazoea shipa ndo maana shule(secretarial) ilimshinda.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom