Hivi kwa UKAWA, Plan B ni ipi?

wabuyaga

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,681
588
Wana JF wengi wetu tunapenda mabadiriko ya kweli yatokee hasa mwaka huu. Na haya mabadiriko yanaweza kutokea baada ya matokeo ya uchuguzi mkuu ujao kuwa kama ifutavyo:

1. Rais ajaye atoke katika vyama vya UPINZANI au atokee ktk chama tawala lakini awe ni mtu ambaye akiangaliwa na wale wote walio kandamizwa na kunyimwa haki zao wajibu kwa kujiamini kuwa ‘’ NI HUYU TULIKUWA TUNAMSUBIRI’’

2. Bunge lijalo liwe na wabunge zaidi ya asilimia 55 kutoka katika vyama vya UPINZANI.

3. Rais wa Zanzibar atokee CUF na wakati huo yatokee kati ya haya: Rais wa Tanzania atokee UPINZANI au asilimia zaidi ya 55 ya Wabunge ktk Bunge la JMT watokee UPINZANI.


SASA BASI:
Wengi wetu tunajua kuwa kutokana na hali ya wananchi ilivyo hasa kiuchumi na kijamii, mabadiriko kutokea ilikuwa ni kusubiri hiyo siku ifike na kuweka tiki tu. Lakini wenzangu tunafahamu kuwa mtaji mkubwa wa chama tawala ni huko vijijini ambako watu hawaelewi kinachoendelea nchini kwetu. Pia ikumbukwe kuna tatizo la kutumia mabavu ili lengo la watawala waliopo likamilike.
Kwa maana hiyo mimi NINASEMA hivi, ni lazima UKAWA iwe na PLAN B ya kuweza kufikia hayo mabadiriko kwa kutumia kati ya njia hizo tatu hapo juu.

Wana JF nani anajua PLAN B ya UPINZANI?


Wenu wa Buyaga akiwa MIKOANI
 
Wenda nisiguse moja kwa moja unachohitaji lakini......moto ule wa uchaguzi serikali za mitaa ukiongezwa....tutapata mabadiliko.Japo tuna mabadiliko ya kifikra, bado taifa letu linategemea mlipuko wa matukio ili kutugutua.Si mnakumbuka escro na uchaguzi serikali za mitaa.!
 
Watu hawana plan A wewe unawauliza plan B si unawaonea tu . UKAWA ni bora liende.
 
Back
Top Bottom