Hivi kwa nn wanamuziki wa kipindi hiki hawavai uhusika wa mwanamke?

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
19,477
25,404
Wakuu hivi ni kwa nini wanamuziki wa kizazi hiki hawavai uhusika wa mwanamke kulinganisha na wanamuziki wa miaka ya 90?

Tuchukulie baadhi kama Sam mapangala, mbaraka mwishehe nk ni kawaida sana kukuta wamevaa uhusika wa kike na kujiita warembo , kubeba uhusika kama mama wa familia au mwanamke aliye kwenye ndoa na changamoto anazokutana nazo

sasa vuta picha mtu kama ney wa mitego atoe wimbo na awe amebeba uhusika wa kike huko IG kungekuwaje?
 
Sasa hivi wakijararibu kuuvaa u-ke na wanavyopenda kujilamba lamba lips wataweza kukonyezwa,dunia hii star wa kibongo anavaa hereni wengine wametoga hadi pua wakikutana na wenyeji wa Mambasa itakuwa balaa.
 
Vuta picha dimpozi kavaa uhusika wa ke itakuaje
 
Yap kweli..
Mfano kwenye 'Rangi Ya chungwa' jamaa anaimba alafu anajijibu mwenyewe kwa kuvaa uhusika wa mwanamke..

"Pole Kaka Mimi Ni bado msichana,Tena bado Sijamaliza masomo, nifanye nini kukuacha siwezi"..

Wanaosema ni nyimbo za kishoga nadhani wao ndio MASHOGA..
 
Ha ha ha ha
Mkuu usiwahukumu bado ni vijana hawakuwa kwenye zile enzi zetu, hawajui walisemalo
 
Sipati picha Muumini Mwinjuma angeimba mwenye ile "nalia mgumba sina mwana.... tangu nimeolewa na mume wangu ni mwaka wa tano sasa...."
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom