Hivi kwa nini...?

Hivi kwa nini...?

6-400.jpg


Mwanamke anaonekana kuwa mzuri anayetamanisha na anayefaa kuoa pale anapokuwa siyo mkeo, lakini akishakuwa mkeo kila kitu kinabadilika.

Sijasema anakuwa mbaya lakini.......
Haka ka-manzi kamenona kweli!.
 

Huyu ni MZURI wa nje tu kwa mtazamo wangu na uzoefu wangu....Amechukua muda wake mwingi kuujenga muonekano wake wa nje,ni jambo jema,ila hainihamasishi kuishi nae.....ila kwa starehe tu anavutia.....wa hivi hawachelewi kuumia,wako sensitive/Delicate sana sana,ukijisahau kidogo tu ameruka kwa mwingine....muda wote/huamini kwa kula ganda la mua bila kukuta fundo:yaani matatizo kwanini yakutokee wakati yeye sio sehemu ya maisha yake....
Anyway huyu ana Gharama zake....WE call "The cost of good Quality" hapa quality namaanisha muonekano wa nje,First impression....
 
kwanza nadhani ni tamaa za mtu ndo zinasababisha mpaka kufikia hatua ya kutoka na kwenda kutafuta wengine nje ya ndoa.
Pili ni kutofahamiana vizuri kati ya wenzi, kabla ya kuoana. Hii pia ni moja ya sababu
 
hata jogoo halitembei na tetea moja .....

nayahusudu sana mapenzi ya kuku.....
 
married love lazima u google ndiyo ladha ya mtandao , waswahili wanakwambia ndoa mbwembwe mapenzi nyumba ndogo.
 
6-400.jpg


Mwanamke anaonekana kuwa mzuri anayetamanisha na anayefaa kuoa pale anapokuwa siyo mkeo, lakini akishakuwa mkeo kila kitu kinabadilika.

Sijasema anakuwa mbaya lakini.......

kwanini mwanaume handsome anayetamanisha na anafaa kukuoa anapokuwa siyo mmeo lakini akishakuwa father house kila kitu kinabadilika.............
images
images
1172684317_extras_fotos_gente_0.jpg
 
namaanisha.....hata sisi wanawake......huwa tunawaona wanaume hivyo hivyo....kwanza usiku unasikia anakoroma.......

tena wanakoroma kama simba yuko maeneo ya uani kumbe hata kichaka hakuna wala hifadhi ya wanyama maeneo ya jirani loh shughuli ipo.
 
Kaka Mtambuzi hata sisi wanawake huwa tunawachoka nyinyi wanaume/waume zetu, kwa sababu kubwa ni kubadilika kwa tabia zenu, pindi mnapotuchumbia, mpk ndoa mnakuwa watu wazuri sana amao mnajua kujali, kutusikiliza kwa kila kitu hata ushauri wetu mnausikiliza na kuufanyia kazi. Lakini pindi nimeshakuwa mke ndani ya nyumba basiiiiiiiiii kila kitu kinabadilika , na yeye ndiye anayekuwa msemaji wa mwisho, hataki tena ushauri, hana kujali tena, wanawake wa nje ndiyo mali kwake kuliko familia yake, anaondoka asubuhi kurudi lala salama, hadi watoto wanakuuliza " BABA KASAFIRI?"
inabidi uitikie ili kuuwa so hapo nyumbani, Sasa hali hii humpelekea mwanaumke kuwa mpweke muda mwingi na kuumia moyoni na kujuta kwa nini alikubali kuolewa na huyo mwanaume.
NINI KINAPELEKEA MWANAMKE KUTOKA NJE: Kwa kipindi hicho anapokuwa mpweke na mwenye majonzi mengi anaweza akapata mtu wa kumweleza shida zake na hisia zake na anaumia vipi moyoni mwake , sasa huyo mwanaume akimbembeleza kidogo tu, akili ya huyo mwanamke ikatulia na kumahidi kumsaidia, hata kama huyo mwanamke alikuwa mzuri na mwenye adabu vipi ni lazima atakuwa na mahusiano ya kula sakalameti takatifu na huyo mwanaume. na kama unavyojua MTAMBUZI cha nje kilivyo kitamu, basi ndipo anaponchonga mzinga.Na familia ndipo inaposambaratika kabisa. MARA NYINGI WANAOANZA NI WANAUME KUTOKA NJE YA NDOA.
 
moja ya sababu ni mazoea..ulikua ukimpenda na kumtamani na kuhitaji sana awe na wewe mmuda wote,akishakua na wewe unaona kama umejihakikishia kua nae na hatokwenda popote,kila siku unamuona ni yule yule,hajabadilika.
ukishamzoea na kumuona wa kawaida basi mambo yatabadilika..
 
Mabadiliko yapo na yanatokea kadri unavyoendelea kuishi na mwenzako......cha msingi ni kuyaelewa hayo mabadiliko na kujua jinsi ya kuyakabili.......mabadiliko yoyote nayaona kama changamoto tu......na mtu ujitahidi kuyakabili in positive way.
 
Back
Top Bottom