Shamba zuri la waridi lisipopaliliwa, magugu huvamia shamba na kuharibu mwonekano mzuri wa shamba hilo! Aidha, kipindi cha uchumba, mapenzi huwa motomoto! Siku haipiti bila kuongea na kumjulia hali mchumba wako. Hauruhusu siku ipite bila kumwona kuongea naye! Unakuwa makini katika kuteua maneno ya kuzumgumza naye, asije akasepa, na zawadi kemu kemu nzuri. Lakini baada ya kuoana unasitisha kufanya hayo ambayo ndiyo yaliamsha hisia nzuri za mapenzi ndani yako.
Aidha, moyo wa binadamu ni kama akaunti ya benki, kuna kutoa na kuweka fedha. Mambo mazuri unapomfanyie mwandani wako, hisia nzuri huongezeka ndani yenu. Ajabu, unataka kwenda kuchukua pesa benki na pesa hujaweka katika akaunti yako? Unatengemea nini? Ukimfanyia mabaya mwandani wako unaondoa akiba yote ya upendo ktk moyo wake na kinyume chake chuki, hasira, dharau, n.k. zinazidi kushamiri! Love your mate as you would have him/her love you!!