Nawaza kwa sauti tu!!haya mambo yanayoendelea nchini,kwa nini watz wengi tunakaa kimya?tunaridhika na maisha tuliyonayo,au tuna busara na hekima kuzidi mataifa mengine?
Tatizo la Watanzania sio Woga ila ni Ujinga. Ujinga wao sio wa tafsiri ya kutokujua kusoma na kuandika Bali ni ule wa kukosa fikra ya kutatua matatizo yaliopo. Wananchi hawana elimu stahiki na wamejengwa katika Imani ya "one day yes" bila ya kuwa na mikakati ya kutekeleza Imani hiyo huku wakiwa na mifano ya watu. Watu wanaishi Kama vile wamepigwa "ganzi" ya kutoweza kufanya maamuzi stahili mmoja mmoja na hawana maamuzi ya pamoja. Hali hii imetufikisha mahali ambapo viongozi wamekosa uoga. Nachujua Hali hii ni ya Muda. Ole wao wanaojitokeza waziwazi kupinga ya wengi.Watanzania siyo waoga isipokuwa walio wengi ni mataahira, na hasa hawa wanaoishabikia CCM kwa rushwa ya chumvi, kanga na vitisheti vya kijani!!!