Hivi kwa nini hili hutokea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kwa nini hili hutokea?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Nyalotsi, Nov 8, 2011.

 1. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Kijana wa kiume unapofikia age ya kuoa,mama na kina dada wanaanza kukupa wosia kuhusu mtu wa kuoa. Mbona madingi huwa wanauchuna? Nipo kwenye hiyo age,siku moja nilikuwa nastorika na mama anielekeza kuhusu mke ninayetakiwa kuoa na sifa zote alizotaja ni zile anazopenda yeye. Kuna vitu vngine mi naona kawaida lakini yeye hapendi. Walipokuja dada zangu nao wimbo ukawa ule ule! Mbona dada zetu cc hatuwapangii mume wa kuolewa? Au mbona akina baba huwa hawawapi wosia mabinti kuhusu wanaume watakaowaleta? Mama na dada zangu nipeni ufafanuzi kuna siri gani huwa inawaumiza? Sory kwa wale watakaofikiri ni teenage marriage niko above 26yrz.
   
 2. b

  bwaxxlo Senior Member

  #2
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kawaida nafikiri madingi huwa hawana muda wa kupoteza na wakwe zao. Mradi unamheshimu yeye hana soo na wewe. Nafikiri akina dada na mama huwa wanatumia muda mwingi na wakwe kwa hiyo wanahitaji mtu atayeelewana nao. Sina experience na kuoa ila nafikiri labda hili linachangia
   
 3. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  lakini somtime unapoletewa mgeni inabidi ajifunze kulingana na mazingira? Au huwa wanaogopa kivuli vile wao walivyokuwa? Kwa nn wanawake wanaogopana kiasi hiki?
   
 4. S

  Song'ito JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Trust me unayekwenda kumuoa ni msichana, hivo wao kama wanawake wapo katika position nzuri zaidi ya kukushauri maana kuna mambo ya kina dada ambao wanaume sio rahisi kujua...thats why wanakushauri wao na sio baba maana wanajijua vizuri jinsi wanawake wanavyokuwa...
  Mi nitofautiane na wewe kidogo kaka, ushauri wao ni muhimu sana, hasa mama mkuu!! siku hizi tunadharau sana busara za hawa watu tunapotafuta majiko lakini kiuhalisia wao wanajua mengi sana juu ya maisha...

  enzi hizo kabla ya mzazi kukushauri umchumbie binti flani, anakuwa amemfahamu muda mrefu sana may be tangu anazaliwa, anakuwa,anakuwa anafahamu historia ya familia yake kwa mapana na marefu na hivyo anajua in and out juu ya huyo anayekuarifu juu yake... thats why unakuta ndoa za miaka hiyo zinadumu sana na pengine kifo ndo huwatenganisha wanandoa..

  Hebu angalia haya mapenzi ya ki.com ya siku hizi... watu wanaoana asubuhi, jioni mwanandoa anafumaniwa au anaachika... tu ni kwa kuwa wakati wa kuoa/kuolewa walitazama sura, urembo, uhandsome bila kujua historia halisi ya mtu anayeolewa nae au anayemwoa.... na hii ndo siri kubwa ya ndoa nyingi za vijana wa siku hizi kuvunjika.... wanaoana wakiwa hawafahamiani hata, hawajuani hata...zamani hii kazi walikuwa wanafanya wazee.. wanachunguza weeeeeee, wewe unawowaaaaaa tuuuuuuuuuuu
   
 5. e

  evaluator Senior Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  umenena vyema,nothing more to add!
   
 6. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Madingi wanatoa ushauri lakini indirectly. Kwa mabinti zao huwa wanawatumia mama zao kufikisha ujumbe. Kwa vijana wa kiume kuna wanaozungumza moja kwa moja, kuna wanaotumia akina mama kwa sababu hata vijana wa kiume huwa wanajisikia comfortable mbele ya mama zao kuliko baba na wengine wanashauri katika mazungumzo ya kawaida bila kuonekana wanalazimisha na mwisho kuna wanaowachagulia wachumba watoto wao moja kwa moja. Siku hizi vijana wakikutana na kukubaliana wanaenda kutambulishana kwa wazazi. Sasa unapomtambulisha mchumba wako unategemea wakae kimya bila kuhoji na kutaka kumfahamu zaidi?
   
 7. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Jihesabie una bahati ya kuwa na washauri katika hili; wengi wetu tulienda kichwa kichwa pengine kwa kukosa watu kama ulionao wewe na ndio maana unatuona hapa tukilalalma!
   
 8. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  mi mwenyewe nimeshawishika,nimemgonga like!
   
 9. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  mkuu niliona maza anazungumzia vigezo vingine kumkuta navyo binti wa kileo ni ngumu. Yaani nilishindwa hata kumbishia,ila ccta zangu niliwapa shule wakanielewa japo kwa shingo upande.
   
Loading...