Hivi, kwa namna hii tutafika.....

shreak

Senior Member
Aug 8, 2011
101
103
Habari zenu wana JF,
Hivi naomba tusaidiane hili jambo, limenikera sana mpk sasa nimejiuliza kisa cha kufanya hivyo sijajua .
Wakati wengine wanalia ajira maisha ,magumu mbona wengine kama vile hawazihitaji vile sasa sijuikwanini wako bado kazini wasiwaachie nafasi wanazohitaji.
Kisa chenyewe ni hivi, nimeenda kwenye duka fulani wanauza mikate stendi ndogo(sunkist)Arusha ,nilihitaji kununua biscut za watoto mkononi nilichukua pesa yakununulia tu nilichokihitaji kuna elfu moja ilikuwa imechanika nusu na imeunganishwa na gundi sikuona kama ilikuwa na shida, cha ajabu nampa muuzaji akaniambia hapokei hiyo pesa kisa watu haitapokelewa nikajaribu kumtoa wasiwasi kwani ile ni pesa halali ya tanzania inafaakupokelewa ndo mana na mimi nimeipokea imechoka tu kwa sababu imezunguka sana kama watu wataikataa wakienda benk waipeleke akanijibu hatuendi benk nikaona huyu labda si mzoefu hazijui hizi pesa za Tz vizuri nikajaribu kumuita mwenzie jirani ambaye alikuwa bize na simu wakati wote aitizame ile pesa aniambie kama ilikuwa na shida cha ajabu hakuonyesha hata interest ya kunisikiliza nikawauliza mnatoa huduma kweli? mana kwa namna walivyokuwa wanatoa majibu.... mh! nimebaki najiuliza kama kweli hawa waliomba kazi na kama ni hivyo mshahara watapataje mana si mara moja nilisha shuhudia tena wakigombana na wateja wengine siku za nyuma, hivi mwenye duka anayajua haya ? nimetamani ningekuwa na namba yake ningempigia mana unajipinda sa nyingine na mikopo ya benki halafu wafanyakazi ndo hivyo inauma sana tutafika kweli? nihayo tu wakuu nawasilisha.
 

NIMIMI

Senior Member
Apr 2, 2011
170
16
Mbona amejitahidi kukujibu vizuri wenzio huku kigoma ni zaidi ya hayo. Pole sana.
 

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
3,799
10,709
Hili ni tatizo kubwa kila mahali. Ubaya ni kuwa hawa wafanyakazi wao hawana uchungu na biashara. Mradi wanajua mwisho wa mwezi mshahara wao upo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom