Hivi kuvaa kanga ni ustaarabu?

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,681
1,698
Wakuu, nimetoka kuangalia kipindi cha 'chetu ni chetu' kilichorushwa na ITV mchana huu.

Japo sikukiangalia tokea mwanzo, maana nilikuwa sehemu, kipindi hicho kilikuwa kikitukumbusha historia ya chifu Mkwawa.

Kilichonifadhaisha ni pale mtangazaji alipoelezea mavazi ya asili ya kabila la Wahehe. Alieleza kwa uzuri kabisa kuwa wanaume walivaa vazi la mgolole na akina mama nguo nyeusi.

Baadae mtangazaji akaeleza kuwa kwa sasa akina mama wanavaa vazi la kistaarabu la kanga, hapo ndo alinichefua na kuanza kujiuliza maswali mengi kuhusu dhumuni la hicho kipindi ni nini!

Ni vema tukavithamini vile wazee wetu walikuwa wakivitumia kwani vilikuwa na maana kiasili yetu.
 
Amekuchefua?

Mwanaume um3chefukwa kwa Sababu ya kina mama kushauriana kuvaa kanga?
We we unataka kuvaa mini?
 
Wakuu, nimetoka kuangalia kipindi cha 'chetu ni chetu' kilichorushwa na ITV mchana huu.

Japo sikukiangalia tokea mwanzo, maana nilikuwa sehemu, kipindi hicho kilikuwa kikitukumbusha historia ya chifu Mkwawa.

Kilichonifadhaisha ni pale mtangazaji alipoelezea mavazi ya asili ya kabila la Wahehe. Alieleza kwa uzuri kabisa kuwa wanaume walivaa vazi la mgolole na akina mama nguo nyeusi.

Baadae mtangazaji akaeleza kuwa kwa sasa akina mama wanavaa vazi la kistaarabu la kanga, hapo ndo alinichefua na kuanza kujiuliza maswali mengi kuhusu dhumuni la hicho kipindi ni nini!

Ni vema tukavithamini vile wazee wetu walikuwa wakivitumia kwani vilikuwa na maana kiasili yetu.
Khanga inategemea ni ya aina gani(nyepesi au nzito)
Imevaliwaje
Imevaliwa na nini (vazi lingine)
Imevaliwa kwa kusudi lipi
Ina maandishi gani nknk
Kukimbilia kusema tu ni vazi la ustaarabu sio sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom