Hivi kusema ukweli ndio faraja kwa Wahanga?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Kuna wakati mtu unaweza kuwaza mpaka hata akili ikasimama ikawa haifanyi kazi tena. Watanzania tuna matatizo gani jamani? Hivi haya ndio mimi nayatambua kwa akili yangu au kwa sababu tunafikiri tofauti? Sasa ndio napata jibu ni kwanini tunataka kupunguza idadi ya vyyo vikuu nchini.


Kuna mfuko wa serikali kwa ajili ya maafa ulio chini ya ofisi ya waziri mkuu, mfuko huu hutengewa bajeti yake Bungeni na hua ni kama mfuko wa dharura hivyo pesa yake sio sawa na bajeti ya kujenga barabara, hiyo pesa bajeti yake haina mjadala lazima iwepo tu kwa ajili ya kuwasaidia wananchi pale linapotokea janga.

Wanadamu wenzangu, Rais JPM kasema ukweli wa kwamba SERIKALI HAITOWAJENGEA WALA KUWASAIDIA CHAKULA waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera ispokua inaenda kujenga miundombinu yake. Kwa kauli hii sidhani kama kuna Mtanzania angefurahia hata kama ni UKWELI, endapo Kama tunatambua kuna mfumo wa maafa ndio utaelewa kwanini si bizuri kufurahia hayo.


Nimejaribu kufikiria sana nikajiuliza,hata kama mtu akikuambia neno flani hata kama sio zuri ili mradi kasema ukweli utafurahia na kumsifia tu. Yaani" hata kama una njaa lakini mimi sikupi Chakula" lakini wewe na njaa yako utafurahia tu kwa sababu amesema ukweli.


Asante sana My President JPM kusema ukweli, msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
 
Mimi sishangai, maana ni huyuhuyu aliyekataa kuwajengea wahanga wa mvua ya mawe na upepo mkali pale maeneo ya kogongwa kahama licha ya JK kuahidi kuwajengea.
 
Back
Top Bottom