Hivi Kunguru weusi wamepotelea wapi hapa Dar?

Hivi Kunguru weusi wamepotelea wapi hapa Dar?

Crimea

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
26,815
Reaction score
38,887
Kuna kipindi walikuwa wengi sana..kiasi kwamba huku uswahilini ilikuwa unaweza kupika nyama yako jikon akaja kufunua ili achukue!

Akina mama ilikuwa unakuta anaosha vyombo nje huku anafukuzana na kunguru..

Nguo za watoto zikianikwa unakuta zimebebwa na kunguru..

Pale Ikulu kunguru walikuwa wanahanikiza kwa kelele mpaka mtu una jiuliza wamefugwa ama?

Kiufupi kunguru weusi walikuwa wengi na walikuwa kero sana kwa wakazi wa dar. Siku hizi wapo ila mmoja-mmoja sana. Hivi kulikuwa na mpango wa kuwaangamiza ama?
 
Kweli wamepungua kiasi, nakumbuka kunamwaka nilienda kwa jamaa yangu Magomeni Usalama basi wakati namsubiri atoke ndani kunguru akawa anaimendea simu yangu niliyokuwa anandiki text sio siri nilibanwa na kicheko
 
Unajua hawa kunguru si wenyeji wa dar,ni wahamiaji tu na inawezekana kabisa tabia zetu huku bara zimewachosha wakaamua kurudi nchini kwao zenj.
 
Unajua hawa kunguru si wenyeji wa dar,ni wahamiaji tu na inawezekana kabisa tabia zetu huku bara zimewachosha wakaamua kurudi nchini kwao zenj.

teh teh....wameenda kupiga kampeni ya kukataa katiba pendekezwa!
 
wamerudi kwao india baada ya kampeni ya tokomeza kunguru weusi kurushwa dar.....kila ukiuwa mmoja ulukuwa unapewa kati ya mia moja na mia mbili............!!
 
Ni Kampeni na sikumbuki ulifadhiliwa na Norway au nchi gani si kumbuki.Lakini ipo mitego mingi tu na kila baada ya muda jamaa huja na gari kuwakusanya na kwenda kuwateketeza. Pia niliwahi kusikia kuwa ilikuaepo campaign ya kukamata kunguru unalipwa pesa na Hao jamaa
 
Mbona wapo wengi tu hapa dar,mimi naona umechanganya waliopotea ni wale walio na baka jeupe kifuani lakini hao wala mizoga wapo tele ,kwani wewe mkuu unawala hao
 
Bado wapo ingawa si kwa wingi

Hawa wanaiba hadi chujio la chai

Vifaranga wanabeba

Ole wako uweke nyama ovyo wanaichukua kama wamenunua wao
 
Naona wengi wenu mnachanganya mambo humu. Kunguru anaowauliza mleta uzi ni wale weusi wenye doa jeupe kifuani na ni wakubwa kuliko hawa kunguru wezi wanaonyea watu hovyo. Ila baadhi ya mikoa wapo wale hapa Dar ni nadra sana kuwaona.
 
Ile mishikaki ya chelewa mnayobugia huko ndio imesaidia kuwapunguza punguza..
 
Hahahaha majibu yaliyotolewa humu! Hata kama jamaa alikua serious nafikiri imebidi acheke tu!
 
kampeni ya kuwapunza kunguru 2010 au mmesahau.
 
Unajua hawa kunguru si wenyeji wa dar,ni wahamiaji tu na inawezekana kabisa tabia zetu huku bara zimewachosha wakaamua kurudi nchini kwao zenj.

alafu pale zenji kuna kunguru wenye mabaka meupe shingoni hawapatani kabisa na hawa kunguru wa bara
 
Ha ha ha ha, smart def`n.
Ok,kuhusu suala la kuiga democrasia na mengine siwezi sana kulikataa.Duniani kote watu wanachukua skeletoni ya idea yoyote ila smart nations huwa wanailocalize na kuifanya iwafae na kuwa kwa manufaa yao.Sasa sisi huwa tunatumia settings zilezile tulizozikuta.Hapa namaanisha kuwa kila kitu kikiundwa kinakuwa na marekebisho ya mwanzo kulingana na mteja.Mfano software programs nyingi zinakuwa na default settings ambazo huwa unaanza nazo ila baadaye inatakaiwa tuzibadili kwa manufaa yetu,kuanzia number ya siri na mengineyo.

China hawakugundua chochote,ila siku hizi wana ndege za kisasa, Nyuklia, magari na vitu vingine vingi ambavyo wanatamba navyo.Saddam mwenyewe scud alinunua silaha na missiles ila akafanyia utundu na kumfanya awe katishio fulani ktk waarabu wenziwe.

Hata magharibi nao wamechukua mengi kwa tamaduni nyingine na kuyafanya yawafae.

Pia hatuhitaji kupoteza muda na gharama kutaka tuanzie sifuri ktk kila nyanja ya maisha.Tayari wenzetu wamegharamia researches na mengineyo na km ni iformation zipo wazi ni sisi kuzitumia tuu kwa ufanisi ili kufukia huu umbali tulioachwa. China na sasa India wameweza, sasa kama sisi tunasubiri tupewe haki miliki bure km ilivyokuwa kwa hati miliki ya kuzalisha dawa za kurefusha maisha kwa waathirika wa ugonjwa wa ukimwi tumeisha. Wachina wamecheza rafu mpaka wazungu wanalia.

Sisi kinatushinda nini wakati hakuna hata mwenye haja ya kuliangalia soko letu? Hapa kazi ni moja tuchukue utaalamu tuufany kuwa wa gharama nafuu then tupige kazi. Nashangaa hao SIDO na Veta wanataka Gundua Computer, gari au mashine yoyote ya kipindi hiki. Wenzio wana makampuni yenye nguvu kuliko serikali zetu, yanaendesha tafiti na yanatengeneza vifaa tofauti ktk hiyo computer au gari, sasa kutaka fanya kazi ya zaidi ya kampuni moja ni kupoteza muda.Wwao wapige akili cha kufanya basi waunganishe vipande kazi iende mbele.

Ok, nadhani ni muda wa kutumia akili na kucheza na vilivyopo duniani kwa manufaa yetu tutafika. Sasa tukitaka kugundua kila kitu. Tutarudi miaka mingi, kwani tutakuta hata nyundo msumari hatuna haki ya kutumia na hata tukiweza buni hatutaweza pata muda wa majaribio ambao vitu vya leo vimepitia. Pistoni ya gari imegundulika miaka mingi na kufanyiwa mabadiliko kwa vizazi, na ktk mazingira ya aina nyingi na gharama kubwa.

Kuna njia kibao za kuwahadaa mataifa ili kupata haki miliki kwa manufaa ya taifa. Njia rahisi ni kudai kupewa msaada na ruhusa ya research na bidhaa za bei nafuu kwa ajili ya vijana na wanafunzi, na baadaye kujikuta kila raia anapata vitu muhimu.Hivi ndivyo wenzetu India na China wamejikuta wanaweza tengeneza computer km laptop ambazo zinauzwa bei ya simu ya mlalahoi wa bongo.

India wamevuta watu kufanya tafiti vijijini na maporini ili kuwezesha huduma muhimu kupelekwa huko kwa gharama ya wengine, leo hii kuna vituo ktk vitongoji vya porini, amabvyo vina internet kwa umma kupitia satelite na kutumia solar, kitu ambacho kimesaidia makampuni machanga ya IT india kuweza kufanya kazi kwa urahisi bila kugharamia mitandao. Pia kazi nyingine za kufunga hivi vifaa zilipewa wahindi.Sisi tunabaki na kimoja tuu ubinafsishaji.

Tunashindwa anzisha wazo na kubandika taasisi za kimataifa wajibebeshe, hatujui hii ndio njia ya kuwadai gharama za ukoloni na utumwa bila nguvu.

Ok, nisiandike mengi ila hizi ndizo njia za kuwatumia wengine watujengee nchi.

Huu hapa ndio mtego wao, upo hapa NIT (Chuo Cha Usafirishaji)
 

Attachments

  • 1413202906639.jpg
    1413202906639.jpg
    113.6 KB · Views: 86
  • 1413202933719.jpg
    1413202933719.jpg
    100.2 KB · Views: 76
Kuna kipindi walikuwa wengi sana..kiasi kwamba huku uswahilini ilikuwa unaweza kupika nyama yako jikon akaja kufunua ili achukue!

Akina mama ilikuwa unakuta anaosha vyombo nje huku anafukuzana na kunguru..

Nguo za watoto zikianikwa unakuta zimebebwa na kunguru..

Pale Ikulu kunguru walikuwa wanahanikiza kwa kelele mpaka mtu una jiuliza wamefugwa ama?

Kiufupi kunguru weusi walikuwa wengi na walikuwa kero sana kwa wakazi wa dar. Siku hizi wapo ila mmoja-mmoja sana. Hivi kulikuwa na mpango wa kuwaangamiza ama?

Hii mitego iko mahali pengi sana. Unaweza usijue kama ni mitego
 

Attachments

  • 1413203475143.jpg
    1413203475143.jpg
    78.4 KB · Views: 74
Back
Top Bottom