Hivi kuna utofauti kati ya congo, DRC na Congo Braziville au Congo Kinshasa?

Hivi kuna utofauti kati ya congo, DRC na Congo Braziville au Congo Kinshasa?

Mpendakukimbiakimbia

Senior Member
Joined
May 18, 2018
Posts
151
Reaction score
274
Nimekuwa nikiyasikia hayo majina yananichanganya sana kama ilivyo kwa UK, England na great britain
 
Kongo DRC ndiyo Kongo Kinshasa hapa Rais wao ni Joseph Kabila na Kongo republic hii ndiyo Kongo Brazzaville na Rais wake ni Denis Sassou Nguesso. Japo wanaongea lugha zinazofanana ni kama Burundi na Rwanda, hata jinsi walivyopakana inafanana kama Burundi na Rwanda.
 
Wametenganishwa na MTO Congo sawa na kivukoni na Kigamboni, ikulu zao zinatazamana zote zilikuwa koloni za Belgium
Kongo DRC ndiyo Kongo Kinshasa hapa Rais wao ni Joseph Kabila na Kongo republic hii ndiyo Kongo Brazzaville na Rais wake ni Denis Sassou Nguesso. Japo wanaongea lugha zinazofanana ni kama Burundi na Rwanda, hata jinsi walivyopakana inafanana kama Burundi na Rwanda.
 
Hizi nchi si ilikuwa moja kama ilivyo kwa Sudan?
 
Nimekuwa nikiyasikia hayo majina yananichanganya sana kama ilivyo kwa UK, England na great britain
Congo Brazzaville ni ya Rais Nguesso na Congo Kinshasa ndo DRC ambayo ni ya Rais Kabila. Ni nchi majirani na wote wanaongea French na Lingala. Congo Brazzaville ndo waliko wale Extra musica kwa upande wa muziki.
 
Congo DR ni ile iliyokua Zaire ya Mobutu seseseko, ndio hiyo Congo ya Kinshasha (Leopordville), halafu pana Congo ile nyingine jirani yake ambayo ni Congo Brazaville. Zimetenganishwa na mpaka wa mto Congo kama walivyosema watangulizi huko juu
 
Back
Top Bottom