Hivi kuna urafiki wa kweli kwa office mates?

msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,627
1,880
kichwa cha habari chahusika,katika maisha yangu ya kazi nimejifunza kitu kimoja muhimu sana,kwamba katika ofisi moja hakuna urafiki wa kweli kabisa. Nimejaribu kuwasikia mara kadhaa watu wakienda nyumbani kwa office mates mwenzao basi utawasikia wanamsema vibaya mara oooh ujanja wote lakini anakaa pale,mara oooooh yule hela ametolea wapi maana lile jumba sio kwa hela hizi.

Sasa mimi staili yangu ya kuishi ni tofauti kabisa na mates wenzangu, kwanza hutanisikia nikiropoka ofisini kwamba oooh nina hichi, nina hichi, niko silence sana,na wenzangu wanahisi mimi ni mtu wa kujirusha kweli kumbe mwenzao kila cent ninayopata nipo ninaitumia kwa makini kweli,wengi nimewakuta hapa ofisini mpaka muda huu wanaendekeza starehe hawana mbele wala nyuma, mpaka sasa nina assets kuwazidi hata wao walionza kazi miaka kumi iliyopita,hakuna hata mtu mmoja wa ofisini anayepajua nyumbani kwangu kwakuwa naamini hata wakipajua nikipatwa na shida wa kunisaidia ni ndugu na marafiki zangu ambao sijanyi nao kazi,siku zote najua ukimkaribisha office mate nyumbani lazma ipo siku atakugeuka tu atakusengenya kwa mtu.

Na hata nikisafiri kikazi mikoani wakishapanga ooooh leo twende club gani sijui gani tutakubaliana pale ila muda ukifika lazma nitapiga chenga tu hawataniona,siku nikiwa fresh mfukoni mimi namchukua mke wangu na watoto wangu wawili tunaenda zetu kula misele,ile city centre tunazunakula bata hata mpaka saa saba then tunarudi home.Nikiwa nyumbani nafanya shughuli zangu kama natokea veitnam vile sina muda wa kupoteza wala kukaa baa kupiga blah blah kwakua najua hiyo ndio nguzo ya maisha yangu mazuri,vitu wanavyoongea office mate wenzangu nyumbani kwamba wanavyo unakuta mimi tayari siku nyingi ninavyo.

SIO KWAMBA MIMI NI MLUGA LUGA ILA HIYO NDIYO STAILI YANGU YA KUISHI, mtaani pale najichanganya ile mbaya pamoja na kazi yangu nzuri ila mtaani wananiona ni mskaji tu kwakuwa naamini majirani ni nguzo muhimu sana kwenye kufikia malengo yangu.

NAWASILISHA.
 
Binadamu hatuna Jema, anyway,ni maisha yako na umeamua kuishi hivyo.

Ila amini kua hata hao majirani na hao unaowaita marafiki wa nje ya office yako bado wanakusema vile vile. Ndio tumeumbwa hivyo na hatuezi badilisha hilo mkuu. Cha msingi wewe Fanya yako maisha yasonge
 
Nimejaribu kuwasikia mara kadhaa watu wakienda nyumbani kwa office mates mwenzao basi utawasikia wanamsema vibaya mara oooh ujanja wote lakini anakaa pale,mara oooooh yule hela ametolea wapi maana lile jumba sio kwa hela hizi.

Haka katabia siyo kazuri

wengi nimewakuta hapa ofisini mpaka muda huu wanaendekeza starehe hawana mbele wala nyuma, mpaka sasa nina assets kuwazidi hata wao walionza kazi miaka kumi iliyopita,

Kumbe na wewe unawafatilia wenzako ... aiseee
 
Dont try! Jamaa yangu aliwapeleka wafanyakazi wenzie kwake, wakamchoma kwa bosi (main share holder). Jamaa na Ghorofa, mara ana swimming pool, mara ana daladala 4, mara na hiki..

Bosi akaanza kumwambia, vp umepata wapi hela ndani ya mwaka mmoja unamiliki hiki na kile... Ofisi ikawa chungu.. jamaa akaacha kazi

Ila anajuta kuwapeleka ofismates zake kwake
 
Binafsi naunga mkono hoja yako saana tu na ujue urafiki wa workmate ni wa mashaka ukibadilisha shirika la kazi wale mabest ni wachache unaweza kuendelea kuwasiliana nao au mawasiliano yanaweza kwisha kabisa. Binafsi marafiki wa kusoma pamoja ndio nimeona ni trustworth.
 
Haka katabia siyo kazuri



Kumbe na wewe unawafatilia wenzako ... aiseee

Kweli mkuu anawafatilia wenzake halafu anajifanya anajua na umachinooo kibao, aache ushamba kumbe bora ya hao wanaoongea, sasa yeye hii ndio tabia gani ya kuwasema wenzie kwenye social network, yale yale na yeye ni walewale anawafuatilia wenzie kinafiki ili upate cha kuandikika humu
 
acha iupoyoyo wewe unafikiri huku duniani kila mtu anatabia za ubahili kama zako nawote wakiwa na tabia kama zako unafikiri biashara zitafanyika
 
Mie sina rafiki jamani mpaka huwa najishangaa, sio ofisini sio mtaani ni ile tu ya habari gani au kuna matatizo tunasaidiana baada ya hapo full stop

Nilijaribu kuwa nao hapo nyuma lakini sasa ....ilikuwa mkitoka out utayakuta ofisi ya pembeni , ukifanya hivi lazima news ziko sehemu na hapo unajua hii habari nimeongea na mmoja tu au nilikuwa na fulani..

Baadae nikaona headache ya nini bora niwe karibu sana na family yangu na ndugu ,watoto na mme tu

Ila huwa najiuliza niko sawa kweli maana huu ni mwaka wa nane sasa kukaa bila rafiki:):):):)
 
Nafikiri uko sahihi, ila kuna vitu ni kasoro zako pia, mfano kushadadia tabia mbaya za wenzako ukijifanya na wewe unazo kumbe unawalizisha tu, kwa hili naweza sema hata wewe ni wa uongo, si rafiki mzuri
Nafikiri ni vizuri kuwaambia wenzako hupendi nini , ila si poa kuwaambia unafanya nini , hili uko sahihi.ukiwaambia hupendi nini itakusave kupata marafiki wa ukweli hata kazini coz itawapa picha wewe ni wa aina gani, wa aina yako wataambana na wewe, wasio wa aina yako wataendelea na Yao,ie kwenda club nk
 
Back
Top Bottom