Hivi Kuna sheria yoyote ya kugawana mali za mwanamke?

mafoleni

JF-Expert Member
Nov 18, 2016
220
371
Wanasheria Msaada tutani, hivi kwa mfano nikawa naishi na mwanamke mwenye kipato kunizidi, yani mimi mwalimu wa shule ya msingi na yeye akabahatika kuwa mbunge. Kabla ya kua mbunge tulikua tumepanga nyumba, muda kidogo akanunua nyumba tukahama. Akanunua magar na nyumba zingine
Miaka ya mbele tukaja tofautiana na kuachana.
Je ninahaki ya kufungua mashtaka mahakamani ili tugawane mali kwa kua tumezipata tukiwa pamoja?
 
mali hizo mmechuma wote kwa hiyo ni za kwenu wote. ila tu muwe mmeoana kwa mujibu wa sheria
 
Si utafute tu Mali zako Mkuu. Kwani nyumba na magari kitu gani Mkuu?

Ukikomaa kwa nguvu zote na kwa nia hakika utanunua gari nyingi tu na kujenga nyumba za kutosha Mkuu!
 
Pole. Hata wanapoongelea mirathi ukweli ni kuwa anafikiriwa kuwa mwanaume ndie atakufa kwanza. Na sheria yote inalenga huko.

Hata uhamasishaji wa kuandika wosia anayeambiwa ni mwanaume !!

Hata unyanyasaji wa kijinsia anayenyanyaswa ni mwanamke tu. Akinyanyaswa mwanaume anachekwa. Akijibu mapigo anashtakiwa.

Ile sheria ya makosa ya kujamiana makosa yote yanamlenga mwanaume. Mpaka kukonyeza. Mwanamke akifanya....

Angalia mwanamke akiua au kujeruhi mwanaume. Ni wivu wa kimapenzi. Mwanaume akifanya ni ukatili mkubwa.

Usawa wa kijinsia. Huko ndo usiseme.

Mimba. Mwanamke amedanganywa. Ukimwita mpumbavu unamdhalilisha!! Sasa anayendanganywa ni mtu wa aina gani?

.....
 
Nadhani mleta uzi ametumia mbunge na mwalimu kama mfano ili apate ufafanuzi kisheria. Naona wengine mnampa hadi pole. Sidhani kama hii ni case yake, lengo lake kuu ni kujua sheria inasemaje kuhusu hili??

Wajuzi wa sheria watoe mwongozo na sisi wengine tujue na sio kumkandia mtoa uzi.
 
Acha ujinga. Mali kachuma yy. Utapewa kifuta machozi. Ktk wealthier yake hukujiongeza ?. Au ulikua papaa ? We ni mzaire nn? Ulifurahia kulelewa .? Vumilia kaka hivyo ndio vya kunyonga kaka.
 
mali hizo mmechuma wote kwa hiyo ni za kwenu wote. ila tu muwe mmeoana kwa mujibu wa sheria
Ayu serious kuoana kwa mjibu wa sheria ndo kukoje hapa Tz?? Km una mashaka na hoja uccte kuacha kuchangia co lzm kila thread uchangie. Soma sheria ya ndoa Na 5/1971 (cap 29 R.E 2002) kuna aina 2 tu za ndoa (monogamy & Polygamy) na pia kuna njia 3 tu za kufunga ndoa (traditional, civil & religion)

Tunapokuja kwenye suala la kugawana mali kinachoangaliwa ni MUDA mlioishi na co aina ya ndoa. Muda uanzie miaka 2 na kuendelea.
 
Mkuu anachokisema ni sahihi. Ndoa isipotambulika kisheria (kwa mujib wa sheria) hamna division of matrimonial propert. Hususan chini ya islamic law hata watoto hawana chake. Pia mali zote zinazopatikana wakati wa uhai wa ndoa is what we call matrimonial propert, na ni halali ya wanandoa na family kwa ujumla. Ingawa hamuwezi gawana equally. Automatically mama ambaye n mchumaji atazidi kiasi. Soma maamuzi mahakama ktk kesi ya #@bi hawa mohamedi# ukigoogle inapatikana.
 
Back
Top Bottom