Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,199
- 10,935
Sasa imejulikana rasmi kuwa nyambizi ya mchongo iliyokuwa ikifanyiwa biashara na kampuni ya Ocean Gate imepasuka na abiria wote watano kufariki dunia.
Waliofariki ni pamoja na mzamiaji maarufu wa kifaransa Paul-Henri Nargeolet. Wengine ni tajiri mkubwa wa kipakistani Shahzada Dawood na mwanawe Suleiman mwenye umri wa miaka 19.
Wengine ni tajiri mkubwa wa Uiengereza na msafiri aitwaye Hamish Harding. Na wa tano ni Stockton Rush ambaye alikuwa ndiye miongoni mwa waendeshaji wa kampuni hiyo na aliyekuwa baharia mkuu katika safari hiyo ya kitalii.
Matumizi ya chombo hicho inasemekana yalikwisha kutolewa onyo na wataalamu wengi kwamba si salama miaka kadhaa iliyopita hata hivyo safari za kitalii za aina hiyo zimekuwa zikiendelea kwa malipo ya fedha nyingi .
Kampuni ya Boeng imekataa kuhusishwa na kutengeneza kinyambizi hicho. Vivyo hivyo shirika la Nasa limejitenga na chombo hicho kama kilivyofanya chuo kikuu cha Washington kilipotajwa kushiriki kukitengeneza kinyambizi hicho
Safari kubwa za chombo hicho ilikuwa ni kuchukua watalii kuwapeleka chini ya bahari takriban futi 13000 katikati ya bahari ya Atlantic ilipozama meli ya Titanic mwaka 1913 na kuua idadi kubwa karibu ya abiria wate walioingia katika meli hiyo.
Kutokana na kupitiwa na muda mrefu meli hiyo ya Titanic kwa sasa imebaki vyuma vyenye matundu matundu ambayo ni makazi ya samaki wachache wanaohimili kuishi kina kirefu cha bahari kama hicho.
Mwaka 2000 mwandishi wa masuala ya sayansi wa kituo cha CBS aliwahi kuganda kwenye Titanic aliposhuka huko kwenye nyambizi ndogo ya kirusi pale waliponasa kwenye feni la meli hiyo na hatimaye kufanikiwa kutoka baada ya saa 72.
Suali la kujiuliza ni kipi wanachokwenda kuangalia wale watalii wanaolipa kiwango kikubwa cha pesa kwa ajili ya safari hiyo ya hatari.
Mwandishi wa CBC akiwa ndani ya nyambizi iiyonaswa na feni la Titanic
Suleiman imeelezwa alionekana akiwa na hofu sana kabla ya kuingia kwenye chombo hicho ambacho huendeswa na rimoti ya michezo ya watoto kwani hakina teknolojia ya kuwasiliana na vyombo vya juu ya bahari kwani chini ya bahari kina hicho hakuna GPS wala mawasilaino mengine ya kawaida.