mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,701
Salamu hii imekuwa ikilalamikiwa kutokana na asili na maana yake kutokuwepo kwa lugha nyingine. Lakini pia simulizi zinaonyesha ziliibuka enzi za utumwa akitoa heshima kwa Bwana wake.
Kwa lugha za asili nyingi ni halali kumwambia mtu mzima "Habari za asubuhi" kwa kilugha mfano "mwangaluka" lkn salamu hiyohiyo kwa maana hiyo hiyo ukimwambia kwa kiswahili mtu Mzima au mzee itaonekana huna adabu.
Nauliza wanagenzi na wananzuoni wa lugha adhimu ya kiswahili.
HII imekaaje?
Mfano
Hbr za asubuhi/mchana/jioni/usiku.
Kwa kiswahili kama zinavyotumika ktk lugha za asili na lugha nyingine za ulimwenguni. Je kuna sehem yenye salamu yenye sura na maana ya shikamoo marahaba! ?
Mfano chokonozi
Kwa nini wazoea na watu wenye umri mkubwa wengi wa Jiji Kong we la dar es salaam huwa hawapendi kusalimiswa shikamoo.
Je huko nchi nyingine kuna salamu za kitaifa zenye sura ya kitaifa kama hizi.?
Je tuendelee kuzienzi kama urithi wa waliotuachia waarabu japo wao hawazitumii?
Nawaza Kilughalugha
UPDATES...
Kwa Mujibu wa Mtaalam wa kiswahili na Muadhili wa Chuo kikuu cha DSM Dr Rajabu Chipila ktk kipindi cha Meza Huru ITV. Pamoja na mwananchi mdau wa Kiswahili.
1:Shikamoo ni Ishara ya Heshima. Kiini ni heshima licha ya asili yake kuhusishwa na utumwa.
2: Ingekuwa haifai, au hata wazee wetu wasingeiendeleza.
3: Ni kichocheo cha amani pia ikiwa taifa likiwa halina mfumo wa watu kuheshimiana kwa lika, umri, hata mfumo wa amani unakuwa hatarini.
4:Tuzienzi salamu hizi kwa misingi ya Kuheshimiana kizio kinachotuunganisha na sio asili ya neno lenyewe. Maneno haya yanaifanya jamii ya waswahili kuwa jamii ya watu wenye kuheshimiana.
5:Kuna sababu nyingi kwa nini watu hawapendi kutumia salamu hizi ikiwemo za kikabila, utandawazi na haijaanza leo ni tangu enzi inaanza salamu hii, lkn ni vizuri ienziwe kama miongoni mwa kiungo cha umoja na mshikamano kama taifa la watu wanaoheshimiana.