Hivi kuna mwanamke maskini kweli?

Mkuu hapa umenifurahisha...Kuna demu Kasoma computer kozi mwezi mmoja pale ucc nimeona kwenye Facebook profile ame update...studied at the University of Dar es Salaam...
teh teh teh ukiingia facebook kila mtu kamaliza chuo kikuu tena UDSM aise hatari tupu duuuu
 
Mimi ni mwanamke nina elimu, sina kazi , sina mshahara , sijiuzi, nina mikono miwili na miguu miwili.
Lakini sio "masikini "
 
Wanawake wote mjini ni matajiri, hakuna maskini;

Wote wanakula zile sehemu za hali ya juu hakuna anayekula kwenye mabanda ya mama ntilie.

Akiagiza kitu lazima atatoa oda kwa vile vitu ambavyo ni vya bei ya ghali kabisa kwenye menu.

Dp zao zote ni either wanaendesha magari, wapo kwenye ndege, mwendokasi au wakifanya shoping.

Hakuna mwanamke mwenye simu ya kitochi.

Hakuna mwanamke wa mjini asiyejua kingereza.

WAKATI HUO HUO:

Hakuna mwenye nywele halisi; wote wana mawigi 99%.

Hakuna mwenye kucha halisi.

Hakuna mwenye kope halisi.

Hakuna mwenye ngozi halisi.

Hakuna mwenye mapenzi ya kweli.
Hii ni kutokana na uzoefu au!?
 
Back
Top Bottom