The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,903
- 19,098
Hivi kula ugali na wali tu vinaweza kusababisha kuongezeka uzito?
Mimi sili chakula kingine chochote zaidi ya ugali na wali, nyama nimepunguza karibu 75℅, sili chips wala kuku wa kisasa.
Sinywi na sijawahi kunywa pombe wala kilevi chochote, sinywi soda wala hizi juice za kopo zaidi ya maji tu.
Nina urefu wa sentimita 190 au futi 6.1, lakini nashangaa naongezeka uzito kadri siku zinavyoenda, nilikua na kilo 88 sasa naelekea 94.kadhaa.
Mbaya zaidi naona kuna dalili ya kitambi inaninyemelea(navyochukia kitambi).. Bora ningekua naongezeka tu uzito bila dalili za kitambi ila hizi dalili za kitambi ndizo zinanikosesha amani.
Wataalam naomba mnisaidie shida ni nini katika mwili wangu. Kwa nini naongezeka uzito?