Dr Boaz Mkumbo MD
New Member
- Jan 6, 2016
- 1
- 0
Nawashukuru wasomaji wa Makala zangu wote kwa shuhuda zenu nyingi sana Mungu awabariki kwani nafurahi sana ninapo ona kila kona watu wananipa pongezi kwa kazi ninayo ifanya. Ninacho waomba wapenzi wa ukurasa wangu ili tuweze kuwafikia watu wengi hakikisha unawatumia watu wengi hii Makala na uwakaribishe marafiki zako wote kujumuika nasi kwani iliandikwa katika maandishi matakatifu, ukipewa bure, toa bure Mungu atakuzidishia yaliyo mema.
Napenda pia kuwapa wosia mchache watu wote wenye ndoto ya kurejea katika afya zenu za mwanzo na uzito ambao ni salama kiafya kuwa.
1. Kitendo cha kuongezeka kilo hadi kufikia kupata kitambi ni mabadiriko ya polepole sana na hivyo hata kitendo cha kupunguza uzito kiafya ni POLEPOLE labda ukitaka kupunguza kwa haraka LISHE SIO CHAGUO LAKO na sikushauri uwe na kiu cha namna hio rafiki yangu.
2. Kitendo cha Kupunguza uzito kinahitaji uvumilivu wa kufanya jambo lile lile bila kukata tamaa mpaka pale utakapo anza kuona mabadiriko madogo na unapo ona hivyo JIPONGEZE KWA HATUA kwani Furaha nayo huongeza uwezekano wa kupunguza kilo Zaidi katika mpangilio wa lishe hii.
3. Epuka KUDANGANYA kuwa upo unatumia lishe halafu kesho yake unaonesha udanganyifu, kumbuka kuwa lishe hii ili uweze kupunguza uzito vitu vinavyo bomoa kabisa ni Udanganyifu na kujinyima kupata chakula wakati una njaa.
Kwa kufuata kanunuzi hizo chache nina Imani rafiki yangu, kiu chako kitakuwa kinalenga kupunguza uzito salama kabisa kwa kutumia lishe yako.
Moja ya swali ambalo wengi wameniuliza kupitia ukurasa wangu facebook kuwa Dr Boaz Mkumbo hivi kwa nini watu wengine ni wanene angali wanaishi maisha duni kabisa?
Najua hata wewe umeshaga wahi kujiuliza swali hili , Binafsi huwa nasisitiza tena tatizo sio UDUNI NA UFAHALI WA MAISHA NDIO UNASABABISHA WATU WENGI KUWA NA KITAMBI NA UZITO ULIOKITHIRI, Hapana! Bali ni mambo yafuatayo
1. Kukosa elimu SAHIHI neon hili nimeweka alama kabisa nikimaanisha kuwa sio kila elimu inakufaa kutimiza malengo yako katika sayansi ya kupunguza uzito. Na hapa ndipo ugonjwa unapoibuka watu wengi wanasumbuka hadi inafikia hatua anaogopa chakula chochote ili tu akate kiu yake, nab ado kila siku kilo zake akienda kwenye mizani zinasonga mbele. Elimu sahihi sasa umeipata utekelezaji ni juu yako kabisa.
2. Kushindwa kupangilio Chakula chako na wengi wenye maisha duni ndio wanakabiliwa na ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi na wanga nyingi kwa sababu ndivyo vyenye bei ya chini kabisa kwa mtanzania masikini. Unapokuwa na kifungua kinywa chako mkate ambao ni aina ya wanga yenye sukari nyingi sana imefikia hadi Gycemic index ya 100 bado mtanzania atapata chai yake kwa TSH 1000 pamoja na watoto wake. Usifurahie baadhi ya bidhaa kwa nini zina bei ndogo, Jiulize kwa nini zina bei ndogo? Ukipata jibu utajua kwa nini unaweka rehani afya yako kwa TSH 1000 na hapo utakuja usumbuke na kitambia maisha yako yote. Ni wakati wa kupata elimu sahihi namna gani unaweza kupangilia lishe yako vizuri kabisa na usibadili bajeti yako kabisa.
Basi naomba niseme kuwa wengi wetu mmekuwa mkiniuliza maswali kwa nini watu sasa wanasumbuliwa sana na kitambi na uzito mkubwa hadi watumishi wa afya wanajua nini maana ya lishe nao wapo matatani, hii ni kwa sababu ELIMU KATIKA JAMII INAYO TOLEWA inakuwa haina MTIRIRIKO MAALUMU na hakuna hospitali yoyote unayoweza kwenda kulazwa kuwa unaumwa KITAMBI AU UZITO MKUBWA. Wanaolazwa ni wale waliopatwa na madhara ya uzito mkubwa kama presha,kisukari,uvimbe kwenye kizazi,ukosefu wa nguvu za kiume,ugumba nk. Sasa napenda kukuambia kuwa kama una kitambi na uzito mkubwa, ni wajibu wako kuhakikisha pesa yako inatumika kulinda afya yako maana bila afya kuwa njema pesa ni kitu bure, Hakika! Ndio maana nikaanzisha ukurasa wangu, wa facebook wa Dr Boaz Mkumbo MD sio kwa kuwa mbinafsi bali nimetaka kuwapa uwezo wa kupata elimu sahihi yenye mtiririko mzuri ili muwe suluhisho kwa wengine na hatimaye Mungu atanizidishia na wewe pia utazidishiwa popote unapotaka mazuri watakie na wengine mazuri hio ndio ya utu katika ulimwengu wa Mungu.
Nalejea katika mada yangu ya leso! Kma umekuwa ukipunguza kilo moja au mbili kwa wiki na wengine wamekuwa wakitoa ushuhuda wa kilo Zaidi ya 8 kwa wiki tatu hii ni ishara kuwa tunatofautiana na huu utofauti nataka leo niupambanue kwa kina kidogo napenda utilize ubongo wako uwe msaada kwa wengine kwa elimu hii. Kama unapungua kidogo sana basi hili hapa suluhisho mpendwa:
Kuna visababishi vifuatavyo vinaweza kukuzuia usipungue uzito kwa haraka angalau kilo 3 hadi 4 kwa wiki kwa sababu hizi hapa nimeanisha
1. HOMONI ZA TEZI YA THYROID
Napenda nikurudishe kidogo darasani, kwa wale mliofanikiwa kufika hadi kidato cha pili najua tutakuwa pamoja, lakini hata kama hukufika lazima utanielewa.
Tezi ya thyroid ipo mbele ya koo la hewa ambayo kazi yake huchovya homoni iitwayo THYROXIN ambayo kazi yake kuu ni kuhakikisha shughuli za mwili zinaenenda katika kasi inayotakiwa mwili uishi salama.
Endapo basi kiwango chake kinapokuwa kidogo sana kinaweza kusababisha shughuli za mwili kufanyika chini ya kiwango kabisa. Na hii inaambatana na maradhi mbalimbali ambayo nitayajadili si muda mrefu. Na endapo ikizidi kupita kiasi pia inaweza kukuletea matatizo kiafya sana unakuwa unapungua uzito bila sababu na unakuwa huna uwezo wa kuhimili joto na mengineyo.
Basi endapo kiwango hiki cha homoni za tezi ya Thyroid kikiwa chini ya kiwango hata utendaji kazi wa shughuli zote zinakuwa chini ya kiwango na hali hii inakupelekea kuanza kupata dalili hizi
-Uchuvu wa muda mrefu ( Bila sababu ya msingi inakufanya uchoke)
-kuongezeka uzito sana
-Choo Kuwa kigumu sana
-Ngozi kavu sana
Hayo ndio matatizo yanayosababishwa na tezi yako ya Thyroid kutotengeneza homoni za kutosha nah ii hali kitaalamu huitwa HYPOTHYROIDISM.
SASA KWA NINI UNAPATA TATIZO HILO MPENDWA AU NINI KISABABISHI CHAKE?
Nitaongelea mambo makuu mawili ambayo ni moja wapo wengi huwakumba na kuwasababishia tatizo hili la tezi hii kutofanya kazi yake ipasavyo kuchovya homoni ya Thyroxine.
-A. Kiwango Kidogo cha madini ya Iodine ambayo husaidia tezi hii kutenegeneza homoni zake ipasavyo. Madini haya ya Iodine nayafananisha na matofali yanayojenga homoni hii ya Thyroxine.
B. Magonjwa yanayoshambulia seli zinazotenegeneza homoni hii na kuizuia tezi yako isifanikiwe kutenegeneza homoni hii pasavyo, hasa magonjwa yajulikanayo kama AUTOIMMUNE (Ni pale kinga ya mwili inapokosea kimtazamo wa kupambana na kuanza kushambulia seli za mwili wa binadamu badala ya adui) Mfano, Gluten inayopatikana katika vyakula vingi vya ngano ni protininngumu ambayo mara nyingi husababisha mfumo wa chakula kutoitambua katika kuimengenya vizur na hatimaye hupelekea kuingia katika mzunguko wa damu bila makusudio hayo. Baada ya kuingia mwili una baini kuna adui unajipanga kwa kutengeneza kemikali za ulizo wa mwili ziitwazo ANDIBODIES na hizo badala ya kushambulia Gluten kemikali hio inaanza kushambulia tezi ya Thyroid. Kwa nini hiki kinatokea? Hii ni kwa sababu kuna baadhi ya seli ambazo zina ufanano wa kibaolojia na gluten (SAME GENOMIC STRUCTURE) na hivyo badala ya kinga kwenda kumwondoa adui GLUTEN inaanza kushambulia Seli za tezi na hatimaye kupata upungufu wa utenegenezwaji wa homoni hii ya Thyroxine. Hivyo hivyo magonjwa kama kisukari aina ya kwanza (TYPE 1) Kisukari cha utotoni kinavyotokea badala ya kinga ya mwili kupambana na adui huanza kupambana au kuzimaliza seli za kutenegeneza insulin zilizopo kwenye Kongosho ( Elimu yake itafuata hapo mbele)
Dalili za tatizo hili ni kama nilivyo eleza hapo juu, Uchovu,uzito mkubwa,.choo kuwa ngumu, na Ngozi kuwa kavu kupita kiasi.
NAMNA YA KUBAINI TATIZO HILI
Unaweza kwenda hospitali kubwa ambazo zinaweza kupima kipimo cha kutizama utendaji kazi wa Thyroid kipimo hiki huitwa THYROID HORMON TEST. Ambapo utachukuliwa sampuli ya maabala na kisha yatapelekwa katika maabala ya kikemia kwenda kuangalia viwango vya homoni zifuatazo
- THYROID STIMULATING HORMONE (TSH)
Kiwango hiki huwa kipo juu kuonesha kwamba una tatizo hilo. Hii ni kwa sababu TSH hutolewa na tezi ya pituitary upande wa mbele kutokana na mwitikio kutoka kwenye HYPOTHALAMUS kwa ili kwenda kui amuru tezi ya thyroid itengeneze homoni zake.
Hivyo kiwango chake kitakuwa juu kwa kuitikia kiwango kidogo cha homoni ya thyroxine katika damu.
- T3 AND T4
T3 huitwa Tri iodothyronine na T4 huitwa Thyroxine Hizi ndizo homoni halisi zinazo onesha moja kwa moja utendaji kazi wa tezi ya Thyroid. Kama tezi ina tatizo kiwango cha T3 na T4 kitakuwa kidogo sana kwenye damu na hapo itajidhhirisha una tatizo la hypotharoidism
JINSI YA KUONDOA TATIZO LAKO KWA LISHE YAKO
- Tumia vyakula vyenye madini mengi ya Iodini kama SAMAKI kwani wameonesha kukuongezea Madini haya kiurahisi sana na upatikanaji wake ni mrahisi
- Tumia chumvi katika chakula chako bila woga na yakutosha, Endapo tu ( Hauna ugonjwa wa figo na ugonjwa moyo kupanuko na huna tatizo la miguu kujaa maji)
- Tumia mboga za majani kwa wingi sana kama kachumbari n ahata katika mfumo wa juisi ( Kinywaji)
Kama UMMEPIMA UMEKUTA TEZI YAKO INAFANYA KAZI VIZURI KABISA NA KIWANGO CHA TSH,T4 NA T3 VIKO SAWA KATIKA MZUNGUKO WA DAMU BASI ANGALIA TENA UNAWEZA UKAWA NA MATATIZO HAYA YAFUATAYO.
2. HOMONI ZA UZAZI
Nitapenda nizungumze kidogo hapa kwani nimekuwa nikisitishwa na wimbi la dada zetu wengu wanasumbuka na kurekebisha mzunguko wa kike lakini imekuwa ni ndoto na kama ni mtihani basi huu ni mtihani ambao wanawake wengi kuufuzu hadi watilie mkazo elimu hii katika kutekeleza.
A. WANAWAKE
Wanawake wengi wana mvurugiko wa homoni za kike na zinginezo ambazo zinawapelekea kupata maradhi mbalimbali, mfano siku hizi kuna wimbi la ugonjwa wa mvurugiko wa homoni za mwanamke uuitwao POLYCYSTIC OVARIAN SYNDROME ambapo mwanamke anakuwa na kiwango cha homoni za kiume yaani Testosterone kwa kiwango kingi kupita kiasi. Na hili linaendana sambamba na kiwango kingi cha INSULIN na hatimaye unapata dalili kama UZITO MKUBWA,UGUMBA,CHUNUSU NDOGO NDOGU SUGU USONI, NA NDEVU. Hili ni janga sana wala hata sio vipodozi ambavyo siku zote imekuwa ni shutuma nyingi zikielekezwa kwenye vipodozi vya kemikali. Hapana siri kubwa na ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi na wanga nyingi.
Njia pekee yaw ewe kutibu tatizo hili, ni kuacha kabisa au kupunguza ulaji wa vyakula vyenye wanga nyingi ( Fuata mpangilio wa lishe yangu ya kupunguza uzito) Ongeza vyakula vya mafuta mazuri katika lishe yako yanayofaa kuunguza mafuta, kula vykula vya protini kwa wastani na mboga za majani kwa wingi kama kachumbali au kinywaji.
B. WANAUME
Hii pia inasababishwa na kuwa na kiwango kidogo cha homoni za kiume na zinazo endana na kiwango kikubwa cha insulin na hatimaye kusababisha uzito kuongezeka kwa kasi,nywele kupungua, na kupungukiwa nguvu za kiume.
Mwanaume ukitaka kuepukana na tatizo hili na ukarudisha heshima yako hakikisha unarejea katika lishe yangu ya kupunguza uzito ambayo inalenga kupiga vita sukari na vyakula vya wanga kama ugali,wali,chapatti,tambi,viazi,mihogo,matunda nk na kuongeza ulaji wa vyakula vya mafuta kam Nyama,mayai,karanga,alizeti,olive,korosho,nazi nk na kula mboga za majani aina zote. Nikiona umetenga sahani yako nisikute chakula chochote ambapo ni wanga asilimia kubwa ninachotaka ni mwili wako ujipatie wanga kutoka katika vyakula vingine kama Mboga za majani na Protini wakati inapokuwa nyingi kupitia Gluconeogensisis kwenye ini.
Pili mazoezi ya viungo hata ya dk 30 kwa siku yatakusaidia wewe kukupa nguvu Zaidi hasa unapokuwa ndani yah ii lishe
Hilo ndilo suluhisho hata kama unataka kushangaza watu jinsi gani lishe hio imebadili maisha ya watu kwa kusoma program yangu na kuifanyia kazi
3. HOMONI ZA MSONGO WA MAWAZO
Unapokuwa katika program yangu ya kupunguza uzito napiga vita sana neon msongo wa mawazo kwani ni adui mkubwa sana katika hatua ya kupunguza kilo nyingi kiafya. Pili napenda mtu aandae chakula chake chenye madoido na manjonjo yote ya jikoni, hii ni kuufanya mwili wako ufurahie chakula ipasavyo na uweze kupunguza uzito.
Mwili wako unapokuwa katika msongo hushtuka na ile hali hupelekea mwili wako kuchovya homoni iitwayo CORTISOL huyu ndiye anayekufanya ule sana baada ya kujinyima kuanzia asubuhi hadi saa kumi ukija kula hutakaa hata muda mrefu utapatwa na njaa utatakiwa tena upate chakula kwani unapokuwa una njaa ya muda mrefu unashtua mwili wako na kusababisha kuzalisha cortisol nyingi ambazo zinakusababishia njaa kali na ulaji wa mara kwa mara mpaka pale itakapo shuka. Hivyo hatimaye utaishia kwenye ulaji mbaya na kukupelekea kuanza kulea kitambi na uzito ulio kithiri. Hii ndio sababu ambayo napiga vita sana mtu kujinyima anapokuwa anamalengo yakupunguza uzito, maana utakuwa unautesa mwili wako bila mafanikio kabisa.
4. DAWA ZA UZAZI WA MPANGO
Nasema kuwa hili ni changamoto swala la kupanga uzazi, kwani huwezi kupanga uzazi kama mzunguko wako mbovu! Wengi huniuliza swali Je hivi ni kweli njia za uzazi wa mpango zina madhara? Naweza kusema kuwa tiba yoyote lazima iwe na faida pia hivyo angalia malengo yako ni yapi na unataka kutimiza nini kwa wakati huo. Mfano kipandikizi,sindano na vidonge vyote hivi vinaongeza uzito na ndio maana hata vipeperushi vyake vimeeleza kiundani kuhusu hilo ili ujue njia ipi hasa inakufaa? Mimi binafsi nashauri njia moja ambayo endapo ukiwa unajitunza na una mpenzi mmoja ni njia ya KITANZI maana aina hii haina homoni yoyote na hivyo haiwezi kubadili utendaji kazi wa mwili wako na hivyo unaweza kupunguza uzito huku umetumia kitanzi kama una woga kuwa kalenda haukutoshi. Najua nimekujibu wewe pia ambaye ulikuwa labda una changamoto juu ya hilo. Na pia napenda kuwashauri wengi ndugu zangu na wagonjwa wangu kwa sababu ni njia pekee ambayo muda wowote ukitaka mtoto unapata na KINACHO HITAJIKA NI KUJISHIMU NA USAFI BASI. Naongea haya kwani nilipokuwa naelekea kupata degree yangu ya Doctor Of Medicine nilijifunza na kufanya tafiti kwa vitendo kwa muda wa siku 30 ambayo ndio tafiti ambayo ilinifanya nitunikiwe shahada ya kwanza ya magonjwa ya binadamu kutoka chuo kikuu Bugando. Hivyo basi kama unalenga kupunguza uzito huku unapanga uzazi tumia KITANZI njia sahihi ambayo haitaweza kuharibu kiu yako ya kuishi bila kitambi na uzito uliokithiri.
Ndugu yangu njia pekee nyepesi na rahisi ya kuweza kupanga uzazi kwa njia ya kalenda ni KUREJEA KATIKA LISHE AMABYO NIMEKUWA NIKIFUNDISHA KILA SIKU KWA WATU WANAOTAKA KUPUNGUZA UZITO NA KITAMBI, Ni njia rahisi,isiyo na gharama kabisa unachotakiwa na kubadili tabia yako katika ulaji na kuzingatia ninacho kiongea kila siku. Usipokifanya chakula kuwa dawa, basi ipo siku utashuhudia dawa zimekuwa kama chakula maishani mwako. SIO LAKUPUUZA!
Napenda kukukaribisha KUWATUMIA MAKALA HII WATU WENGI WANAOSUMBUKA NA UZITO MKUBWA NA KITAMBI WAUNGANE NASI KATIKA JUKWAA LA AFYA FACEBOOK KUPITIA UKURASA WANGU FACEBOOK: Dr Boaz Mkumbo MD.
NAJUA UMEFURAHIA MAKALA YANGU, NAOMBA MAONI YAKO KAMA UMEJIFUNZA KITU NA KAMA UNA SWALI DONDOSHA HAPA CHINI NITAKUJIBU
NOTE: Kuna watu wanataka kuonana na mimi LAKINI NAPENDA KUWAAMBIA KWA SASA SINA KITUO CHOCHOTE NIMEANZISHA UKURASA HUU KUWAGUSA WOTE MIKOANI NA NJE YA NCHI. NAPOKEA EMAIL NYINGI, SMS INBOX NYINGI SANA HIVYO NINAPOCHELEWA KUJIBU USIJALI NITAJBU NALEMEWA NA WAHITAJI WA HUDUMA HII.
Mwisho nawapongeza kwa UTEKELEZAJI NA SHUHUDA NYINGI NINAZOPATA NJE NA NCHI NA NDANI YA NCHI HUU NI UKOMBOZI ANZA UTEKELEZAJI SASA.
Dr Boaz Mkumbo MD
Healthy and Wellness Coaching Program Coordinator
Email: boazkitundu@gmail.com
DAR ES SALAAM