Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Hivi mtu kuingia ofisini na kukuta nchi inakopesheka na yeye kuamua kuendelea kukopa mpaka kuanza kuonywa juu ya ukopaji huo kuwa kuna hatari kwa nchi, na kutumia fedha hizo kugharamia miradi michache huku watakaolipa fedha hizo ni wananchi masikini. Je, huku ndio kuchapa kazi kwa kiongozi?
Yaani wewe unaingia ofisini, na kabla hujafanya jitihada za kuongeza uzalishaji katika nchi yako ili kuongeza mapato ya Serikali, unaanza kukopa halafu wafuasi wako wanatuambia unachapa kazi. Hivi huu sio uongo wa mchana kweupe?
Cha ajabu, baadhi ya miradi unayotekeleza ilibuniwa na Serikali iliyopita au ni ilani ya chama chako. Sasa wewe kukopa kutekeleza hiyo miradi huku watakaolipa fedha hizo ni wananchi masikini wa nchi yako. Je, huo ndio uchapa kazi?
Kama huu ndio uchapakazi. Je, wale viongozi wanaoingia madarakani na kukuta nchi ina hali mbaya kiuchumi na kuja na mipango na mikakati na kuisimamia kuhakikisha uchumi wa nchi na maisha watu wake vinaboreka, viongozi wa aina sasa nao watasemaje?
Na wale ambao nchi zao zinazalisha kutosheleza soko la ndani na hata kuuza bidhaa nje, viongozi hawa na wafuasi wao nao watasemaje?
Tanzagiza inanishangaza sana!!!