Hivi kujiita Mtanganyika ni kosa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kujiita Mtanganyika ni kosa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by baina, Feb 8, 2011.

 1. baina

  baina JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ninashida ya kujua yafuatayo ili nijue jina la nchi yangu;
  1. tanganyika na zanzibar ziliungana, mbona zanzibar bado ipo lakini tanganyika hiyoooooooooo?
  2. mbona zanzibar kuna rais, makamu, jaji mkuu, bendera ya taifa, wimbo wa taifa n.k ?
  3. kimichezo, zanzibar ina timu ya taifa?
  4.mbaya zaidi kuna hata katiba?
  5. kama tanganyika iliungana na zanzibar na kuwa na nchi moja, inakuwaje nchi moja iwe na marais wawili?
  6. kimichezo, eti timu ya taifa ya tanzania na timu ya taifa ya za'bar maana yake nini? tz ni bara visiwani?
  7. je, tanzania ni wapi?
  8. kama wenzetu manazidi kujiita wazan'bar kwanini nami nisijiite mtanganyika? na je nikifanya hivyo nitaeleweka?
  9. kwa kuwa tayari nitajiita mtanganyika je nikisema mimi sina rais nitakosea, kwani rais aliyepo ni wa tanzania?
  Naomba majibu kwani haya mambo yananikera sana.
   
 2. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hakuna nchi inayoitwa tanzania na wala hicho wanachokiita uhuru wa tanzania si kweli, hakuna nchi inayoitwa tanzania hapa duniani ambayo iliwahi kupata uhuru. Huu ni uongo mkubwa!
   
 3. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  na hapo ndipo penye hekima!
   
 4. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaani hii nchi inabidi iitwe FUMBO.......maana inaendeshwa kimafumbomafumbo tu.......huu MUUNGANO ni FUMBO......hii DOWANS nayo ni FUMBO.....UCHAGUZI 2010 nao ni FUMBO.
   
 5. birungi

  birungi JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nchi ya kusadikika.

  ambacho huwa kinanitach mimi ni kuwa kuna raisi wa tanzania na raisi wa zanzibar, what about tanganyika.(take breath)
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tanganyika imezimia ! Na jamaa wakisikia unajiita mTanganyika unaweza wakakufungulia kesi ya uhaini.
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  utakuwa umekosea saana mkuu hakuna nchi inayoitwa tanganyika utauwawa bure!
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hiyo ni kweli anataka kifo!
   
 9. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Jana tulikuwa kwenye udahili katika chuo fulani cha umma, sasa kwenye fomu yao, sehemu ya uraia wa mdahiliwa mimi nikaandika kuwa ni Mtanganyika. cha ajabu ni kuwa mhusika alishangaa ile fomu, kisha kuniuliza mara kadhaa kwamba kimejiri nini hata nijitambulishe hivyo, tena akauliza kwani tunachotaka ni nini hasa, kwani ameona fomu kadhaa zikiwa zimejazwa hivyo. Sasa nauliza wana jamvi, izi zea e problemu na Utanganyika wangu?
   
 10. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kujiita mtanganyika ni kosa kama tu wewe ni mzanzibar. Inawezekana aliyekuwa anaiangalia form yako alidhani wewe ni mzanzibar. Vinginevyo kama wewe si mzanzibar ni sahihi kabisa kujitambulisha ulivyojitambulisha.
   
 11. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  nitake radhi kaka, mimi ni mkakamavu, kisogo ninacho, siyo arab addict, tena huwa silalamiki hovyo, sasa uzanzibar unatoka wapi tena?
   
 12. F

  FUSO JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,878
  Likes Received: 2,343
  Trophy Points: 280
  kumkumbuka marehemu tanganyika ni kosa kisheria, na kama unabisha wewe peperusha bendera ya tanganyika siku ya maadhimisho miaka 50 then utaona kitakachofuata.
   
 13. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Duh kumbe tuko wengi ambao tunajitambua na kuipena Tanganyika yetu sasa itabidi tuianzishe rasmi nchi hii yenye asari na madini yanayoibwa na mabeberu wa kitanzania.
   
 14. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  kabisa, hata jina lenyewe lina mvuto. mtikila had a point aisee!
   
 15. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  ubabe wa kijinga, si mwalimu alishasema kama upande hautaki muungano tuuvunje. sasa wanachokumbatia ni nini. MIMI NI MTANGANYIKA!
   
 16. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Mimi nitakuwa wa kwanza kukamatwa au kufa kwa ajiri ya kuidai Tanganyika na kujiita Mtanganyika.
   
 17. F

  FUSO JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,878
  Likes Received: 2,343
  Trophy Points: 280
  kaka upo sahihi kabisa, ila police wa tanzania hawalijui hilo, lazima utalala ndani hadi jtatu mchana unatoka. wapo walioipigania tanganyika ila walifikia pabaya, ngoja nimpigie mtikila anipe msimamo wake.... narudi.
   
 18. N

  Nonda JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu
  Watawala na viongozi wa nchi ya Tanganyika, viongozi wetu "walituwakilisha" na kutupatia Tanzania.
  Sehemu iliyokuwa ikiitwa Tanganyika ilibadilishwa jina kinyemela na Mwalimu na Warioba na kuiita Tanzania bara.

  Kwa hiyo, tuking'ang'ania katiba mbovu ya 1977. Wewe ni mtanzania bara na kwa raia anaetoka Zanzibar, kulingana na katiba hiyo hiyo yeye ni mtanzania visiwani.

  Kwa bahati njema, Zanzibar kama jina la sehemu limebaki hata baada ya juhudi za kulitokomeza kufanyika lakini Tanganyika halikuweza kuhimili usanii na mazingaombwe ya Mwalimu na Warioba na pia viongozi waliofuatia.

  Katika historia ya Miungano, huu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa "baadhi ya mambo" ambayo yanajulikana kama mambo ya muungano, ndio muungano ulioweza kulipoteza katika ramani ya dunia, jina la mshirika mmoja wa muungano.

  Kama unaamini katika kiini macho, mazingaombwe au usanii basi hilo ndilo lililofanyika.
  Na utakapolitaja jina Tanganyika utakumbana na "reaction" kama hiyo ya huyo aliyeipitia fomu yako. Huenda ukaonekana ni mhaini pia na watetea Utanzania na utanzania bara.

  Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara!!! ndio imetufikisha hapa. Hata kulitaja tu jina Tanganyika tunapata kigugumizi.

  Dola ya mrumi haipo, lakini hakuna aliyetafuta jina lengine mbadala...hata kama ni historia litanumika Roman empire lakini hata kutaja uhuru wa Tanganyika inaonekana ni maajabu ya dunia. Tunaambiwa Tanganyika haipo. Yale mambo ya Tanganyika ambayo si mambo ya Muungano, vipi?
  Ni mambo ya Tanzania bara?

  Kama sio msanii au huna utaalamu wa uchawi na mazingaombwe huwezi kuelewa kitu katika hili.

  Tafuta msaada kwa Jaji Warioba au chuo cha usanii na utamaduni Bagamoyo watakusaidia katika hili.
   
 19. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Yamenitokea puani haya ya Utanganyika... Juzi ya Mungu nimeitwa na afisa tawala wa Koleji yangu, akanihoji maswali mengi na kunichimba mkwara wa kuifikisha fomu yangu kwa uongozi wa juu wa chuo...
  Ah... Kosa langu ni lepi mie?
   
 20. M

  Mbonafingi Senior Member

  #20
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haki ya MUNGU Watanganyika lazima tubadilike na kuitukuza Tanganyika yetu. Wazanibar wametupiga bao wanajitambulisha kwa uzanibari na upemba. Mi mzanzibar mi mpemba .Sisi watanzania mpaka ukakasi mi MTANGANYIKA. TAFAKARI BADILIKA CHUKUA HATUA .Jivunie Utanganyika wako
   
Loading...