Hivi kuitwa YATIMA mwisho ni miaka mingapi?

Hivi kuitwa YATIMA mwisho ni miaka mingapi?

puker

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2018
Posts
1,047
Reaction score
2,167
Habari za muda huu wana JF.

Kuna kitu huwa inaniboa sana na kunitia simanzi ambayo haina msingi kwa wakati huo.

Kwa mapenzi ya Mungu, kuna wengine tumepoteza wazazi angali tukiwa wadogo kabisa.

Tumeishi chini ya kivuli cha uyatima kwa kipindi kirefu, tumepitia mengi....Manyanyaso, kutengwa, Kuonekana hatufai, simanzi na kila aina ya maumivu.

Mungu kwa rehema zake ametusaidia tumekuwa wakubwa na maisha yetu yanasonga linatokea limtu kila likikuona anajifanya anakuonea huruma....."Eti maskini mtoto wa fulani, wazazi wako wamekuacha mdogo" Anaongea hivyo kwa masikitiko makubwa as if kuna juhudi zozote alifanya kipindi tunahitaji msaada.

Kiukweli hii kitu inaniumizaga sana inakufanya unarudisha mawazo nyuma na kujiona hujakamilika.

Mtu anamaisha yake hakutegemei kwa chochote kila unapomkuta...neno Yatima halikauki kwenye kinywa chako...mimi nahisi hata Mungu tunamkosea mapenzi yake yalitimia kama nikulia tumelia tukachoka sasa mambo ya kukumbushana machungu sio poa.
 
Navyojua yatima ni mtu aliyepoteza wazazi wake wote

Sijui ni kwa namna gani mtu anafikia wakati anapoteza uyatima
Point yangu hilo neno sio zuri kwa linalomhusu sioni sababu yoyote ya msingi kum identify mtu kuwa ni yatima ikiwa hakuna sababu ya msingi kumuita hivyo ni kama kumnyanyapaa tu, hamjui tu ni kiasi gani inaumiza.
 
Point yangu hilo neno sio zuri kwa linalomhusu sioni sababu yoyote ya msingi kum identify mtu kuwa ni yatima ikiwa hakuna sababu ya msingi kumuita hivyo ni kama kumnyanyapaa tu, hamjui tu ni kiasi gani inaumiza.
Nimeipata point yako
Naimagine itakuwa inakera kweli

Mie nimejibu kutokana na kichwa cha uzi wako
 
Nimeipata point yako
Naimagine itakuwa inakera kweli

Mie nimejibu kutokana na kichwa cha uzi wako
Vizuri kama umeelewa. Na kuongezea hilo neno limekaa zaidi kiuhitaji. Hivyo hutamkwa ili mtu ajisikie huzuni na huruma kuona umuhimu wa kutoa msaada kwa muhitaji( Yatima) hasa akiwa katika umri ambao bado anahitaji kupata malezi ya baba na mama ila kwa wakati huo hawapo hivyo wanahitaji kusaidiwa.
 
Pole sana liverpool FC, kuna mdau kakuita hivyo kwenye thread ya jamaa asiye cheat mke wake kwa miaka 8
 
Aisee kuwa yatima kusikie tu, lakini yakikukuta utaimba haleluya, utalia wee mpaka utachoka, utawaza sana lakini ndio hivyo Tena wazazi hawapo.
Aliyesema yatima hadeki hakukosea kabisa.
Kabisa
 
IMG_20220219_225256.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom