Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,960
- 11,222
Nadhani wewe ndio limited sio mimi na sijui unaelekea wapi na hoja zako. Ni hivi hakuna liability bila ya responsibilities, regardless of who is appointing people each position is accompanied with duties before liability fall upon their seniors. Mhusika lazima ajibu his contractual obligation na kama ni makosa yake so is the liability.mkuu tatizo lako ni lile lile la kuwa paronchial...
nikuulize swali, je unamjua mwajiri mkuu na mkuu wa utumishi wa umma nchini ni nani?
unajua kitu kinaitwa vacarious liability na corporate liability?
kwa sentensi hiyo ni kwamba sasa umekubali kuwa Kikwete anateua/anaajiri kila mtu na kwamba kikwete ni mwanasiasa. kwa hiyo sasa futa usemi wako wa mwanzo kuwa si kila mfanyakazi wa umma anateuliwa na mwanasiasa.Nadhani wewe ndio limited sio mimi na sijui unaelekea wapi na hoja zako. Ni hivi hakuna liability bila ya responsibilities, regardless of who is appointing people each position is accompanied with duties before liability fall upon their seniors. Mhusika lazima ajibu his contractual obligation na kama ni makosa yake so is the liability.
Hata kama JK anateua kila mtu lakini wote hao wanamajukumu yanayoeleweka kikazi, tatizo la JK linaweza kuwa kuteua watu wasio na uwezo sehemu zingine. Aindoi accountabiliy ya mfanyakazi, au kiongozi wa kitendo inategemea na kosa lenyewe kama washauri wanasema pale kuna usimamizi mmbovu ina maana CEO ni tatizo; wakisema pale accountants awafuati taratibu za kuripoti zinazopendekezwa na CAG ina maana chief accountant washirika anahusika.
Ndio maana CAG wamelalama sana ata kama wizi mwingi unafanyika bila ya ushirika wa viongozi wao (na watu wanachukuliwa hatua kutokana na makosa yao) bado kuna tatizo la management kwenye kuboresha mifumo yao ya kazi na usimamizi wa rasilimali zao including ppl ili kupunguza tatizo.
That is to say blameworthy is based upon the nature of the illicit act, inaweza kuwa mtu, msimamizi, kiongozi mkuu au shirika.
Lakini hoja hapa ni mfumo hayo mengine sijui unayaleta ya nini.
Sijakataa kwamba kuna tatizo kwenye madaraka ya raisi hila ninachosema teuzi za raisi ni 'small cog in the large wheel'.kwa sentensi hiyo ni kwamba sasa umekubali kuwa Kikwete anateua/anaajiri kila mtu na kwamba kikwete ni mwanasiasa. kwa hiyo sasa futa usemi wako wa mwanzo kuwa si kila mfanyakazi wa umma anateuliwa na mwanasiasa.
na mimi bado nipo hapo hapo kwenye mfuno kwamba mfumo wa ccm na serikali yake una udhaifu na mabaya mengi na kwamba moja ya mabaya hayo ni hilo la kurundika madaraka na nguvu nyingi mno kwa rais, kwa mfano hilo la kikwete kuteua/kuajiri kila mtu.
hapo mimi ndo huwa napata shida na wakawa (cdm) chama kilichoonesha kuwajibishana ni ccm.. mawaziri wangapi mpaka leo wapo gerezani.. mramba, yona.. mgonja, liyumba. Mawaziri wangapi wamewajibishwa ikiwemo huyo lowasa. Hao chadema wanawajibishana kwa mtu kuingilia maslahi ya mhowe tu. Ukitaka kugombea uenyekiti tu unatupiwa vilago na kuitwa msaliti.. zzk na wangwe.Nakuhakikishia Chenge, Rostam wanaweza kuhamia chama kingine chochote na huko wakawa viongozi wazuri kulingana na utamaduni watakaoukuta huko. Kwa lugha nyepesi, kinachoitwa 'mfumo' hapa ni utamaduni uliojengeka chini ya uongozi wa ccm ambapo wakosaji na wezi wa mali ya umma wenye nyadhifa serikalini hawawajibishwi kwa makosa wanayotenda. Badala yake wanalindwa. Wanasiasa hao wakihamia chama kingine ambacho hakina huo utamaduni wa hovyo, hawana jinsi bali kubadilika.
jichunguze mwili wako.jinsi unavyo fanya kazi ni mfumo tosha.lakini maamuzi makubwa yanafanywa na ubongo wako.serikali nayo ni mfumo hakuna mtu anaamua jambo peke yake labda Raisi kwa mamlaka yake.kwa hiyo ukiona kitu flani kinajirudia mara kwa mara ujue mfumo wa serikali umeruhusu kitu hicho kitokee mfano ufisadi.the same kWanasema tatizo la ufisadi ktk nchi yetu ni "mfumo"ndiyo maana hata baada ya lowassa kujiudhuru mwaka 2008,umeendelea..! Me nauliza huo mfumo ni kitu gani sasa ambacho binadamu hawa(watuhumiwa)hawahusiki!??
Mfumo ni uwendeshaji wa serikali, na Mfumo huo wa uwendeshaji ni katiba, hivyo chagueni ukawa iwaletee Katiba mpya itokayo na maoni ya wananchi ambayo ndio Mfumo mzuri munao taka katika kuendesha serikali pamoja na kulinda rasilimali za nchi,na huu Mfumo tulio nao ni Mfumo ulio dumaza na kuwalea viongozi kutokuwa na maarifa badala yake kutuweka katika umasikini na kutuibia mali za umma na kutunyanyasa wananchi.Juhudi za kumsafisha Lowassa zimeshika kasi hasa humu jamvini..!
Viongozi wa ukawa walipoulizwa juu ya ufisadi wa Lowassa,walidai tatizo la ufisadi si lowassa bali ni "mfumo" Tangu hapo wapenzi wa upande huo wamekuwa wakiitetea sana hoja hiyo. Me naomba wanisaidie,hivi kinachoitwa mfumo ni kitu gani,maana tunaaminishwa kana kwamba hicho kinachoitwa mfumo ni kitu hivi cha kushika.
Hata CCM yenyewe huwezi kuishika hivi mkononi,utakuta kuna viongozi,wanachama,sare,katiba nk.
Hivi kwa mfano viongozi wote walioko ccm na serikali yake wote wakihamia chadema,huo unaoitwa mfumo utabaki ccm kwenye majengo au utakuja chadema walikohamia wenye mfumo!??
Yaani eti hata wakija CHADEMA, Rostam Aziz,Nazir Karamagi,Andrew Chenge nk. Eti mfumo utakuwa umebaki CCM na wahusika watakuwa safi!!!
Acheni bhaana..